Makubwa! Kuibuka kwa Matatizo ya Muungano-kipindi cha Hayati Magufuli sikuyasikia haya

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,723
28,261
Wana JF,
Nimepatwa na mshangao kumuona Mama Samia Jana anaongelea changamoto za Muungano kwenye masuala ya fedha, nilidhani ni masihara nashangaa leo tena yameibuka kwenye speech ya Makamu wa Rais.

Ama kweli hamna mtu mbaya au mzuri moja kwa moja-kipindi cha Magufuli haya mambo sikuwahi kuyasikia au hawa Wazanzibar wanataka ku-take advantage ya Mama kuwa kwenye nafasi.
 
Yawezakuwa mwanzo mpya,unatoa mwanga hata kwa wasioona wanapata muujiza wa kuanza kuona,ama mahaba yalizidi kiasi cha kusema chongo,au asiyeweza kabisa kuona ni kengeza tu,na litapona.
 
CCM Magufuli mna matatizo sana,kwahiyo hutaki kero za muungano zitatuliwe?

Kama ni haki yao waache wapewe,haki kwa haki zama za ubabe ziliisha Machi 17 ,2021.
 
Wana JF,
Nimepatwa na mshangao kumuona Mama Samia Jana anaongelea changamoto za Muungano kwenye masuala ya fedha, nilidhani ni masihara nashangaa leo tena yameibuka kwenye speech ya Makamu wa Rais.

Ama kweli hamna mtu mbaya au mzuri moja kwa moja-kipindi cha Magufuli haya mambo sikuwahi kuyasikia au hawa Wazanzibar wanataka ku-take advantage ya Mama kuwa kwenye nafasi.
Matatizo ya muungano hayajawahi kwisha bali sema wangeyasemea wapi wakati alishasema hataki kushauriwa?
 
Unafiki wa kiwango cha standadigeji , wakati wa Jiwe matatizo yalikuwepo lukuki ila hawakuthubutu kusema walimuogopa dikteta uchwara .
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom