MAKUBWA!!!!CCM Dar nao walalamikia kupanda kwa bei ya vyakula. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAKUBWA!!!!CCM Dar nao walalamikia kupanda kwa bei ya vyakula.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MIGNON, Mar 8, 2011.

 1. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Ninaangalia taarifa ya habari kupitia Channel Ten na naona CCM Dar wakitoa tamko la kulalamikia kupanda kwa bei ya vyakula. Hawa ni wenye serikali ambao wangeweza kuelezena ndani kwa ndani.

  Kunapofuka moshi,
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  bei haipandishwi na ccm kamwe....! tuwaambie watu ukweli ili kwa pamoja tutafute suluhisho la matatizo yanayotukabili...!
  "WRONG INFORMATION LEADS TO A WRONG CONCLUSION/RESEARCH"
   
 3. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Dear Mahesabu
  Kupanda kwa sukari kumehusishwa na baadhi ya wafanyabiashara kuhodhi bidhaa hiyo ili wa create artificial scarcity na bei ipande.
  Sheria ya uhujumu uchumi ipo na inaelezea kuhusu mambo haya.Serikali hii ni ya chama gani?
  In short serikali ya CCM imeshindwa kusimamia mambo ya msingi kwa kukosa watu waadilifu.
  Raisi na Waziri mkuu wamesema bei ishuke,jee imeshuka?
  Nini kinawapa jeuri wafanyabiashara hawa kama si michango yao kwa CCM?
  Sikutegemea CCM kuitisha kikao cha wanahabari nao kulalamika kwa hili otherwise tutawaona nao wanataka kuangusha serikali halai.
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kupanda kwa bei ya bidhaa ni mambo yao ndani ya ccm na serikali yake. Wasituudhi kwa kutoa tamko la kipuuzi ili kutuzuga tu. Wakaweke kwenye agenda zao za kifisadi na kuliongelea huko huko.
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mmmh.
  Senema inaanza, ngoja nitafute popcorn kwanza.
   
 6. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 506
  Trophy Points: 280
  Ndio wanajibu mapigo ya CHADEMA.ha ha ha! Too late.
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kama RAIS (Mwenyekiti wa CCM) na Waziri Mkuu wanafahamu fika kwanini bei ya SUKARI imepanda halafu wanakuja majukwaani kutuelezea kuwa wanafahamu hivyo na kutoa maagizo kwa wafanaya biashara kushusha bei, BUT, siku saba baadaye bei ipo pale pale na haionyeshi kushuka.

  And, all of sudden, kundi la watu wanaojihita wana-CCM wanakuja kwenye Media na kuanza kulalama, What does that tells you? Pre-emption at work? Banana Republic?
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  According to RAIS na Waziri Mkuu, kupanda kwa bei ya SUKARI hakuna uhusiano na kupanda kwa mafuta na bidhaa zitokanazo na mafuta!
   
 10. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama walitaka kuvuta bilioni 94 kupitia kivuli cha DOWANS wananchi wakashtuka sasa wafanyeje, wanadunduliza kwenye sukari na vitu vingine ambavyo hamtaweza kugundua mapema. Gharama walizotumia kwenye uchaguzi wa Oktoba 2010 ni lazima zilipwe kwa njia yoyote iwayo!!!!
   
 11. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  mKUU Mahesabu, tunapozungumzia CCM ina maana ya Serikali iliyochini ya CCM, wao ndio waoendesha uchumi kwa kufuata sera zao (Za chama chao)
  Uongozi wa nchi uliochini ya Chama Tawala ambao unatumia sera za chama Tawala ndio chanzo cha haya maisha mabovu yaWatanzania,
  Hivi Mkapa aliwezaje kudhibiti uchumi wa hii nchi?
   
 12. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,176
  Likes Received: 1,901
  Trophy Points: 280
  Mbwa anakula mwanaye! kivyenu mwana;
  Wengine tumeshakuwa sugu.
   
 13. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi naiona kama series vile inayofanana na Days au Isidingo.
   
 14. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Tujiunge pamoja tununue sukari nje!.....bila import tarrifs!
   
 15. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wanafiki hao! Wanataka kuwazuga wananchi. kwanini hawakuongea kabla ya cdm kuanza maandamano na kuwambia wananchi ukweli.? Research zinaonesha kuwa kila baada ya uchaguzi mafuta na bidhaa zote zinapanda bei ili kulipa gharama zilizotumiwa na ccm kwenye kampeni. So huwezi kutofautisha mfumuko wa bei na ufisadi wa ccm then hawa mambwisi wanasema hawajui na wanaitaka serikali isolve tatizo. Miaka hii hatudanganyiki kizembe. Go to hell ccm
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  siasa ndiyo iliyoharibu nchi

  tunashindwa kuwaruhusu technical person wafanye kazi kutwa kamati za bunge zinakua na nguvu kwenye maamuzi ya kitaalam wakati wabunge wengine ni wanakwaya, wamama wa nyumbani, wavuta bangi na mavuvuzela

  siasa imeharibu nchi, na kiranja wa siasa tanzania ni CCM na hivyo basi huwezi kukwepa hilo

  CCM imetufikisha hapa
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kweli sasa naamini kifo cha CCM,kimekaribia sana!
   
 18. F

  FENI Member

  #18
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona bei ya sukari wameishusha kama sio ccm inayosababisha kupanda kwa bei
   
 19. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Cha kushangaza chadema wanalalamikia mambo hayo hayo halafu wanawaita wachochezi. Mbona wao hawaitwi wachochezi kwa kulalamikia vitu ambavyo cdm wanalalamikia?
   
 20. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Lazima ipande, bei ya mafuta inapanda kwa sababu ya conflict za Libya na oil producers wengine, umeme hakuna, productivity lazima ishuke.
  Tatizo kubwa Serikali imezoea uwongo na siri mpaka wanajikanyaga wenyewe, hawataki kuadmit chochote. Utaamuru vipi bei zishuke? Hii ni nonsense, wafanye kazi yao wahakikishe umeme unapatikana.
  Na Saudi Arabia nayo maandamano yakishika moto ndo tutakoma.
   
Loading...