Makubaliano yaliyofungua ukodishaji mkubwa Ardhi Mpanda (Unaotetewa na Mizengo Pinda)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
Unaposoma makubaliano haya kuna vitu viwili vya kuangalia; sehemu ya kwanza kuhusiana na feasibility study na pili kuhusiana na possible terms za mkataba wa makubaliano. Vizuri kuangalia terms hizo na kuona je haziwezi kuweka sehemu yetu kubwa ya ardhi mikononi mwa wageni. Jisomee kwa uchungu.
 

Attachments

  • Agrisol MOU with Mpanda (11 August 2010).pdf
    4.6 MB · Views: 127

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
931
Kuna tatizo gani hapo..kuwekeza ishakuwa dhambi?

Ni sawa na wewe ulivyowekeza kwenye JF unakula matangazo kwa ulaini

Mwenzako ameamua kulima..

Wewe embu ongelea symbion kwanza achana na wazawa..
 

Dar_Millionaire

JF-Expert Member
Aug 6, 2008
227
79
Unaposoma makubaliano haya kuna vitu viwili vya kuangalia; sehemu ya kwanza kuhusiana na feasibility study na pili kuhusiana na possible terms za mkataba wa makubaliano. Vizuri kuangalia terms hizo na kuona je haziwezi kuweka sehemu yetu kubwa ya ardhi mikononi mwa wageni. Jisomee kwa uchungu.

Hahahaaaa Mwanakijiji hebu angalia statistics za hiyo attachment yako. ZERO VIEWS!

Yaani watu hawasomi vielelezo (exhibits) lakini wamekazana kuroopoka na kulaani kwenye discussions balaa.

By the way inaweza kuwa deal nzuri au mbaya kutegemea na other benefits (esp. financial). Bado hatujaona business plan, feasibility study report, na land lease agreement. Hii ni memorandum tu, sio mkataba wenyewe.

Ila madudu kwenye memorandum (ambayo I hope hayatarudiwa kwenye mkataba) ni hapo wanapolimit hiyo ada ya Tshs. 500 kuwa isiongezeke. Wanasema kuwe na infllation related adjustment to, hivyo effectively wanailimit iendelee kuwa Tshs. 500/- milele.
 

ugali

Member
Mar 31, 2010
25
2
kukodi eka moja ya kulima ni kati ya shilingi 10,000 hadi 50,000 kienyeji. sasa sijui hizi rate zao wametoa wapi.
 

Petu Hapa

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
714
55
0. Argrisol - kutakano na utafiti wa awali wanataka kulima nini? Serikali inadhani hilo ineo linapaswa kulimwa nini kutokana na uzoefu wa wakazi wa eneo hilo ama mahitaji ya taifa lenyewe? Je kunamahusiano kati ya lengo la mwekezaji na nchi yetu zaidi ya hizo asilimia za pesa?

1. hivyo vijiji vya jirani katika 2.13 vinamatumizi gani na hayo maeneo, na jeo sio katika eneo lao la vijiji? Kama ndivyo, ukodishwaji huu kwanini ufanywe na serikali kuu peke yake. Je maingizo ya uwekezaji huu yanaenda kufanyiwa nini?

2. Ukodishwaji wa ardhi wa miaka 99 - kwanini iwe 99. Kama ni uzalishaji wa mpunga ama mahindi hauhitaji kuwe miaka 99. Nadhani tunahaja ya kufanya marejeo juu ya miaka ya umiliki. Tuanze kuangalia aina ya shughuli, na ukodishwaji urejewe pale inapoonekana stahili.

3. Ajira kwa wananchi - huwa ni kipengele kigumu sana kwa wawekezaji. Hivyo inapaswa serikali yenyewe ihakikishe iwapo kampuni hii itakayolima "mawe", inahitaji wachimbaji, basi watu waanze kutayarishwa kabisa.

4. Wajemeni, hii ni biashara sasa hivyo viwango vya kukodi ardhi vya shilingi 200 na miatano kwa mwaka sio sahihi kabisa! vipitiwe upya - kwa kuthaminisha thamani ya ardhi, rutuba yake, na matumizi yatakayofanyika!

5. Hii Iowa university katika kipengele cha 4.7 inamahusiano gani na Agrisol - ? Wamekubali haya?

6. Sijaona mazingira ama sharti linaloelekeza uzalishaji wao! tunataka wazalishe kwa kiwango gani!
 

Dar_Millionaire

JF-Expert Member
Aug 6, 2008
227
79
Petu Hapa,

Kupata majibu mazuri kwa mswali kama hayo ndo hapo kuna umuhimu wa kupata:

1. Ripoti ya feasibility study

2. Ripoti ya Environmental Impact Assessment

3. Business plan ya Agrisol
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom