MAKUBALIANO YA SIRI: JK aahidi kumrudisha Lowassa madarakani

Sijaona chama cha upinzani TZ cha kumuangusha rais JK KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO.
Hakuna nchi ambayo rais wake anaangushwa na wanachama wa upinzani tu.
Nchi inaangushwa na wananchi. kwa Tanzania si Chama cha upinzani kinachoweza kumuondoa rais bali wananchi.
Hivyo ulipaswa kusema "sijaona wananchi wa TZ watakaomuangusha rais JK KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO"
 
..... nitafurahi sana Mkwere akifanya hivyo maana utakuwa ni utimiifu wa maandiko kwamba anguko la CCM limekaribia. Mkwere take my words, bring him (Eddo) back!!!
 
Luteni,

Tafadhali leta data kudhibitisha machafu na maovu ya Lowasa na si kuja na viswahili vya jikoni vilivyojaa maneno ya taarabu.
Kasome ripoti ya Mwakyembe iliyothibitisha uchafu wa mtu wako. Let me tell you, EL will never ever be the same again you are wasting your time to back a person who was given an opportunity but he wasted it.

Mwalimu Nyerere hakuwa mjinga alipotuambia wazi kuwa hawezi kuiacha Tanzania kwa mabepari kama kina Lowassa. Kosa alilofanya Kikwete ni kumkaribisha Lowassa madarakani kitu ambacho nafikiri JK atakijutia sana maishani mwake.
 
Wadau wanasema kuwa kabla ya kuamua kuchukua tena fomu za kugombea Urais, Jakaya Kikwete alishikwa na hofu kubwa sana na akasita kuchukua uamuzi. Hii ni baada ya kusikia kutoka kwa watu wake wa karibu na vyombo vya dola kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, anataka kum-challenge Kikwete kwenye kupata nomination ya kugombea Urais 2010 yeye mwenyewe au kwa kuweka mgombea wake mwingine.

Ndipo hapo Kikwete akaamua kumuuliza Lowassa mwenyewe iwapo hizo taarifa ni za kweli. Lowassa akajibu kuwa bado hajafanya uamuzi kama agombee Urais 2010 au la.

Lowassa akamwambia Kikwete ingawa makubaliano yao ya awali ni kuwa Lowassa achukue Urais 2015 baada ya Kikwete kumaliza vipindi viwili, hivi sasa yuko gizani kisiasa baada ya kujiuzulu (political wilderness).

Lowassa's fear is that wanasiasa kama Bernard Membe, Prof. Mark Mwandosya, Dr Hussein Mwinyi, Dr. John Magufuli na Lawrence Masha (ingawa yuko kambi ya Lowassa) watampiku kwa umaarufu ifikapo 2015 hivyo ndoto zake za kuwa Rais zitafifia zaidi.

"Unajua msimamo wangu na malengo yangu (ya kuwa Rais 2015) bado yapo palepale," Lowassa alikaririwa akimwambia Kikwete.

Kikwete akamjibu Lowassa kuwa basi asijali. Akamwambia kuwa kujiuzulu kwako kama PM tutasema ilikuwa ni ajali ya kisiasa tu. Akamuahidi Lowassa kuwa atamshangaza kila mtu na kumrudisha serikalini kwa kishindo baada ya uchaguzi wa 2010.

"Don't worry my friend. I will surprise everybody kwa kukurudisha madarakani ili ujiweke vizuri na uchaguzi wa 2015," JK alikaririwa na wadau akimwambia Lowassa.

Haikuweza kufahamika mara moja ni madaraka gani JK atampa Lowassa ili ajiweke vizuri kumrithi Urais 2015.

Kuna tetesi kuwa JK atampa Lowassa a senior Cabinet post (uwaziri) au kumfanya ndiye Katibu Mkuu mpya wa CCM baada ya Yusuf Makamba ili akikamate chama vizuri kuelekea 2015.

Baada ya mazungumzo na Lowassa, Kikwete ndipo akapata nguvu kwenda Dodoma kuchukua fomu za kugombea Urais kama mgombea pekee wa chama.

Ila bado ana suspicion kuwa kundi la mtandao ndani ya CCM lililokuwa loyal kwa Lowassa na Rostam Aziz linaweza kumfanyizia. Ndiyo maana akamtuma mwanae Ridhwani afanye kazi ya kutafuta wadhamini kwa hofu ya kuwa sabotaged na kuwekewa wadhamini feki na hivyo kuwa disqualified kama candidate.

Narudia tena, hizi ni tetesi tu. Ila inapotokea hali ambapo Rais wa nchi anamhofu ex-PM wake, tena aliye lazimika kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ina maana kuwa "this country has gone to the dogs" kama Mwalimu Nyerere alivyowahi kutuonya.

The Informer
4th July 2010 12:26 PM #1

https://www.jamiiforums.com/members/the-informer.html

user-offline.png

Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date Mon Jun 2010
Posts 6
Thanks : 4
Thanked 36 Times in 4 Posts

my take:mwanaume kazini
 
Mungu wetu Mungu wetu Mbona umetuacha?! mbona u mbali na uso wa Tanzania?, Mafisadi wakiachiwa watawale ni nani kati yetu atasimama? Mafisadi wakitutenda mabaya ni nani kati yetu atabakia? Ee Mungu utuokoe na Majeshi ya Farao mkuu. Utuepushe na Mafilisti(Mafisadi) wanaoishambulia nchi yetu ya ahadi.....Wamwage mafisadi wote katika bahari ya sham asisalie hata mmoja.....Na wote watakao pata uongozi kwa ushirikira uwauwe wote....Amina Amina..Amina.....Nono lako linasema mchawi hapasi kuishi hivyo KIONGOZI YEYOTE ANAYEKWENDA KWA WAGANGA NI MSHIRIKINA MCHAWI hapaswi kuishi huyo!
 
Hakuna mwingine aliye bora zaidi ya Lowassa?

I am tired of this Man..

Precisely so do I,

Kama anajiamini si angechukuwa Fomu tuuu maana kunawatu wana mtaka huyu jamaaa arudi mchngishieni na mkachukulie Fomu basi khaaa EL EL EL hawamchokiiii,

Kweli i dont feel his test at all yeye aendelee kuwa mbunge wa Monduli na kuwasimamia watu wa monduli na aendeleze cheche zake zile alizokuwaga nazo basi kwa jimbo lake tuone kama sio uwaziri mkuu ulikuwa wampa kiburi cha kufanya hayo huwaga anayafanya huko monduli
 
Kasome ripoti ya Mwakyembe iliyothibitisha uchafu wa mtu wako. Let me tell you, EL will never ever be the same again you are wasting your time to back a person who was given an opportunity but he wasted it.

Mwalimu Nyerere hakuwa mjinga alipotuambia wazi kuwa hawezi kuiacha Tanzania kwa mabepari kama kina Lowassa. Kosa alilofanya Kikwete ni kumkaribisha Lowassa madarakani kitu ambacho nafikiri JK atakijutia sana maishani mwake.

Luteni, Ripoti ya Mwakyembe nimeisoma vizuri na kuielewa vyema. Bayana imesema haikumpa Lowassa nafasi ya kujieleza ama kuulizwa maswali mbele ya tume husika.
Tume ya Mwakyembe kwanini iliweza kuwaita wahusika wote na kuwauliza maswali lakini ilishindwa kumwita Lowassa ili kupata ukweli halisi?. Inawezekana Lowassa aliwaagiza wahusika kuchukua maamuzi ambayo walichukua, lakini Lowassa alikuwa ni mtu pekee ambaye angeweza kujibu kiundani kwanini alitoa maelekezo hayo kitu ambacho kilikuwa ni muhimu kabla ya kufikia maamuzi.

Lowassa alionewa ama hakutendewa haki hili halina ubishi.
 
Na endapo JK akarogwa tu kumrudisha atakuwa ameichafua nchi hajawai pata kuona, na ninahisi kutakuwa na hatarishi ya CCM kumeguka hapo maaana siju ni nani atataka CCM imegukie kwake?

Mimi nikiwa ndani ya chama nami labda nife kabla ya 2015 sidhani kama EL atapita hata kama atarudishwa kwa uwaziri.

kutakuwa na challenge kubwa sana that time mtu asijidanganye ati atanaka urais yani IKULU kumekuwa mahali pa pango la walanguzi jamani kwanini hawa watu wana uchu na Urais kuna biashara gaaani pale, IKULU ni mzigo mzito sana sasa huyu EL anapataka kuna uwepesi upi wa yeye kupakabiri??

Unless alikuwa ana fanya Jocks tu kwa JK
 
Lowassa alionewa ama hakutendewa haki hili halina ubishi.
Kidatu

Suala la kuongea kwa sasa ni kama anatufaa au hatufai na si kama kaonewa ama hakuonewa. Kama Lowassa alionewa well, nani aliyeandika barua ya kuomba kujiuzuru na sasa analalamika kwa nani au tujue nyie(kidatu) ndio mnalalamika on behalf.

Binafsi kama Lowassa anaona alionewa na hataki kwenda mahakamani basi ajitokeze wazi achukue fomu atangaze kugombea nafasi za juu asitegemee kuja kubebwa na Kikwete. Vinginevyo aridhike na ubunge wake na asiendeleze majungu pembeni kwa kuwafitinisha baadhi ya viongozi wetu wa juu, kwa kuendeleza makundi ndani ya chama kwa misingi ya uanamtandao ambao JK anajitahidi kuuvunjilia mbali, ndiyo maana JK aliona bora ampe mtoto wake jukumu la kutafuta wadhamini kuliko wanamtandao wenye majungu.
 
pamoja na scandal ya Richmond...tukubali tusikubali Lowassa ana mtandao mpana na umaarufu zaidi ya huyu Mkwere
 
Wadau wanasema kuwa kabla ya kuamua kuchukua tena fomu za kugombea Urais, Jakaya Kikwete alishikwa na hofu kubwa sana na akasita kuchukua uamuzi. Hii ni baada ya kusikia kutoka kwa watu wake wa karibu na vyombo vya dola kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, anataka kum-challenge Kikwete kwenye kupata nomination ya kugombea Urais 2010 yeye mwenyewe au kwa kuweka mgombea wake mwingine.

Ndipo hapo Kikwete akaamua kumuuliza Lowassa mwenyewe iwapo hizo taarifa ni za kweli. Lowassa akajibu kuwa bado hajafanya uamuzi kama agombee Urais 2010 au la.

Lowassa akamwambia Kikwete ingawa makubaliano yao ya awali ni kuwa Lowassa achukue Urais 2015 baada ya Kikwete kumaliza vipindi viwili, hivi sasa yuko gizani kisiasa baada ya kujiuzulu (political wilderness).

Lowassa's fear is that wanasiasa kama Bernard Membe, Prof. Mark Mwandosya, Dr Hussein Mwinyi, Dr. John Magufuli na Lawrence Masha (ingawa yuko kambi ya Lowassa) watampiku kwa umaarufu ifikapo 2015 hivyo ndoto zake za kuwa Rais zitafifia zaidi.

"Unajua msimamo wangu na malengo yangu (ya kuwa Rais 2015) bado yapo palepale," Lowassa alikaririwa akimwambia Kikwete.

Kikwete akamjibu Lowassa kuwa basi asijali. Akamwambia kuwa kujiuzulu kwako kama PM tutasema ilikuwa ni ajali ya kisiasa tu. Akamuahidi Lowassa kuwa atamshangaza kila mtu na kumrudisha serikalini kwa kishindo baada ya uchaguzi wa 2010.

"Don't worry my friend. I will surprise everybody kwa kukurudisha madarakani ili ujiweke vizuri na uchaguzi wa 2015," JK alikaririwa na wadau akimwambia Lowassa.

Haikuweza kufahamika mara moja ni madaraka gani JK atampa Lowassa ili ajiweke vizuri kumrithi Urais 2015.

Kuna tetesi kuwa JK atampa Lowassa a senior Cabinet post (uwaziri) au kumfanya ndiye Katibu Mkuu mpya wa CCM baada ya Yusuf Makamba ili akikamate chama vizuri kuelekea 2015.

Baada ya mazungumzo na Lowassa, Kikwete ndipo akapata nguvu kwenda Dodoma kuchukua fomu za kugombea Urais kama mgombea pekee wa chama.

Ila bado ana suspicion kuwa kundi la mtandao ndani ya CCM lililokuwa loyal kwa Lowassa na Rostam Aziz linaweza kumfanyizia. Ndiyo maana akamtuma mwanae Ridhwani afanye kazi ya kutafuta wadhamini kwa hofu ya kuwa sabotaged na kuwekewa wadhamini feki na hivyo kuwa disqualified kama candidate.

Narudia tena, hizi ni tetesi tu. Ila inapotokea hali ambapo Rais wa nchi anamhofu ex-PM wake, tena aliye lazimika kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ina maana kuwa "this country has gone to the dogs" kama Mwalimu Nyerere alivyowahi kutuonya.

Mtandao upo kazini unapima upepo, hakuna kitu cha namna hii
 
Am sorry to differ from many, lakini mi naamini katika kutawala kwa JK, Lowassa bado atakuwa mtendaji mzuri. Sitakuwa na tatizo akirudi...
 
Mbona iko tetesi nyingine kwamba jamaa hawezi kumwachia madaraka mtu wa dini fulani? sijui niseme!
 
Am sorry to differ from many, lakini mi naamini katika kutawala kwa JK, Lowassa bado atakuwa mtendaji mzuri. Sitakuwa na tatizo akirudi...

Tatizo ni busara ndogo. Mwenye Busara, kwa yote yaliyompata hata kama ni uongo, angesema basi! basi!
 
Kidatu

Suala la kuongea kwa sasa ni kama anatufaa au hatufai na si kama kaonewa ama hakuonewa. Kama Lowassa alionewa well, nani aliyeandika barua ya kuomba kujiuzuru na sasa analalamika kwa nani au tujue nyie(kidatu) ndio mnalalamika on behalf.

Binafsi kama Lowassa anaona alionewa na hataki kwenda mahakamani basi ajitokeze wazi achukue fomu atangaze kugombea nafasi za juu asitegemee kuja kubebwa na Kikwete. Vinginevyo aridhike na ubunge wake na asiendeleze majungu pembeni kwa kuwafitinisha baadhi ya viongozi wetu wa juu, kwa kuendeleza makundi ndani ya chama kwa misingi ya uanamtandao ambao JK anajitahidi kuuvunjilia mbali, ndiyo maana JK aliona bora ampe mtoto wake jukumu la kutafuta wadhamini kuliko wanamtandao wenye majungu.

Kinachojadiliwa hapa ni haki ya Lowassa katika kugombea uongozi kama mtanzania. Watu wamekuwa wakipinga sana kwamba Lowassa hapaswi tena kugombea uongozi tokana na yale yaliyotokea. Na ninachojaribu kukuelewesha ni kwamba Lowassa anayo haki kimsingi kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Tanzania kama mtanzania. Pia Ninajaribu kukufafanulia kwamba kujiuzulu kwa Lowassa kusichukuliwe kwamba ni failure ya yeye kuwa kiongozi mzuri, bali aliwajibika ili kuepusha usalama na amani ya Taifa, hata ripoti ya msomi wenu Mwakyembe ilikiri hivyo.

Utatoaje hukumu bila ya kumuuliza na kumsikiliza mtuhumiwa?. Ripoti ya Mwakyembe copy halisi aliyopewa mkuu wa nchi ililazimisha Lowassa awajibishwe ama alazimishwe kujiuzulu, sasa kwanini asipewe nafasi ya kujieleza kama wengine walivyopewa?. Tafadhali msikilize Lowassa katika link za hapo nyuma na utaona mantiki kwanini alichukua maamuzi aliyoyachukua.

Na mwisho ningependa kukueleza kwamba Lowassa ni moja kati ya watendaji na wafuatiliaji wazuri sana wa shughuli, na Tanzania inahitaji mtu kama yeye ili tuendelee.
 
Ukiendelea kung'ang'ania mambo ya ripoti ambayo ilishajadiliwa bungeni na kutolewa uamuzi haitakusaidia kitu maji yalishamwagika kinachotakiwa ni kusonga mbele.

Hakuna mtu anayemzuia kugombea mbona bado ni mbunge na anatarajia kugombea tena, kugombea ni haki ya kila mtu hata majambazi yana haki hiyo hiyo ila mwaamuzi wa mwisho ni mwananchi(watanzania), yeye ajitose kama anafikiri bado ni msafi ila asitegemee kubebwa na JK au kupambwa na wapambe wake yakiwemo magazeti.
 
Hii nadhani ni propaganda ya wanamtandao, ama pia inawezekana wana bipiana....Kama ni kusema ajali ya kisiasa alishasema kabla hata uchaguzi haujawa issue, sasa labda kama alimwambia Lowassa kuwa atasema kwa mara ya pili kwamba ni ajali ya kisiasa...something that isn't an issue at all....Unless ni watu wa JK wanataka kujua kama EL ana mpango gani...Miyeyusho tu hii...

Nani alisema JK atapata baraka zote za kuunda serikali?Pyschological warfare...Yani mna aasume kuwa JK keshashinda Uchaguzi kwa hiyo topic sasa ni baraza lake la mawaziri la term yake ya pili...Mhn Mhn...Ashinde kwanza,kampeni bado,na wagombea wengine bado kujitokeza,haya ni ya ccm,kama ccj ingekuwa valid basi sasa stori ingekuwa nyingine.
 
Hivi ni nani aliyemwambia Lowassa kuwa lazima awe rais wa Tanzania? Unaweza kuwatumikia Watanzania bila kuwa rais wao.
 
Back
Top Bottom