Wadau wanasema kuwa kabla ya kuamua kuchukua tena fomu za kugombea Urais, Jakaya Kikwete alishikwa na hofu kubwa sana na akasita kuchukua uamuzi. Hii ni baada ya kusikia kutoka kwa watu wake wa karibu na vyombo vya dola kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, anataka kum-challenge Kikwete kwenye kupata nomination ya kugombea Urais 2010 yeye mwenyewe au kwa kuweka mgombea wake mwingine.
Ndipo hapo Kikwete akaamua kumuuliza Lowassa mwenyewe iwapo hizo taarifa ni za kweli. Lowassa akajibu kuwa bado hajafanya uamuzi kama agombee Urais 2010 au la.
Lowassa akamwambia Kikwete ingawa makubaliano yao ya awali ni kuwa Lowassa achukue Urais 2015 baada ya Kikwete kumaliza vipindi viwili, hivi sasa yuko gizani kisiasa baada ya kujiuzulu (political wilderness).
Lowassa's fear is that wanasiasa kama Bernard Membe, Prof. Mark Mwandosya, Dr Hussein Mwinyi, Dr. John Magufuli na Lawrence Masha (ingawa yuko kambi ya Lowassa) watampiku kwa umaarufu ifikapo 2015 hivyo ndoto zake za kuwa Rais zitafifia zaidi.
"Unajua msimamo wangu na malengo yangu (ya kuwa Rais 2015) bado yapo palepale," Lowassa alikaririwa akimwambia Kikwete.
Kikwete akamjibu Lowassa kuwa basi asijali. Akamwambia kuwa kujiuzulu kwako kama PM tutasema ilikuwa ni ajali ya kisiasa tu. Akamuahidi Lowassa kuwa atamshangaza kila mtu na kumrudisha serikalini kwa kishindo baada ya uchaguzi wa 2010.
"Don't worry my friend. I will surprise everybody kwa kukurudisha madarakani ili ujiweke vizuri na uchaguzi wa 2015," JK alikaririwa na wadau akimwambia Lowassa.
Haikuweza kufahamika mara moja ni madaraka gani JK atampa Lowassa ili ajiweke vizuri kumrithi Urais 2015.
Kuna tetesi kuwa JK atampa Lowassa a senior Cabinet post (uwaziri) au kumfanya ndiye Katibu Mkuu mpya wa CCM baada ya Yusuf Makamba ili akikamate chama vizuri kuelekea 2015.
Baada ya mazungumzo na Lowassa, Kikwete ndipo akapata nguvu kwenda Dodoma kuchukua fomu za kugombea Urais kama mgombea pekee wa chama.
Ila bado ana suspicion kuwa kundi la mtandao ndani ya CCM lililokuwa loyal kwa Lowassa na Rostam Aziz linaweza kumfanyizia. Ndiyo maana akamtuma mwanae Ridhwani afanye kazi ya kutafuta wadhamini kwa hofu ya kuwa sabotaged na kuwekewa wadhamini feki na hivyo kuwa disqualified kama candidate.
Narudia tena, hizi ni tetesi tu. Ila inapotokea hali ambapo Rais wa nchi anamhofu ex-PM wake, tena aliye lazimika kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ina maana kuwa "this country has gone to the dogs" kama Mwalimu Nyerere alivyowahi kutuonya.
Jamani, Lowasa kwani si mtanzania kama walivyo watanzania wengine?. Ina maana hana haki ya msingi ya kugombea uongozi ndani ya Tanzania?.
Tusiwe kama wayahudi waliokuwa wanashangalia na kushabikia kwamba YESU asulubiwe bila kujua hali halisi ya mambo.
Hivi hapa jamvini kuna mtu anaweza kuja na facts kuonesha na kudhibitisha mabaya na machafu ya Lowasa?.
Bila shaka ni wachache sana hapa jamvini wanaojua ukweli kwanini Lowasa alijiuzulu uwaziri mkuu na pia kwanini hakupewa nafasi ya kujieleza mbele ya kamati ya Mwakyembe.
Jamani shilingi ina pande mbili, hivyo kuweza kujua urembo wa shilingi ni hekima kuangalia pande zote.
Wengi mlifurahi sana kuona Lowasa amejiuzulu uwaziri mkuu, lakini mliweza kujiuliza kujiuzulu kwake katika nafasi hiyo kuliwapa faida gani hapa jamvini ama ndani ya Tanzania?. Mnaimba kwamba Lowasa alikuwa ni fisadi, sasa amejiuzulu uwaziri mkuu je ufisadi umekoma ama umeisha ndani ya Tanzania?.