MAKUBALIANO YA SIRI: JK aahidi kumrudisha Lowassa madarakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAKUBALIANO YA SIRI: JK aahidi kumrudisha Lowassa madarakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Informer, Jul 4, 2010.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Jul 4, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau wanasema kuwa kabla ya kuamua kuchukua tena fomu za kugombea Urais, Jakaya Kikwete alishikwa na hofu kubwa sana na akasita kuchukua uamuzi. Hii ni baada ya kusikia kutoka kwa watu wake wa karibu na vyombo vya dola kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, anataka kum-challenge Kikwete kwenye kupata nomination ya kugombea Urais 2010 yeye mwenyewe au kwa kuweka mgombea wake mwingine.

  Ndipo hapo Kikwete akaamua kumuuliza Lowassa mwenyewe iwapo hizo taarifa ni za kweli. Lowassa akajibu kuwa bado hajafanya uamuzi kama agombee Urais 2010 au la.

  Lowassa akamwambia Kikwete ingawa makubaliano yao ya awali ni kuwa Lowassa achukue Urais 2015 baada ya Kikwete kumaliza vipindi viwili, hivi sasa yuko gizani kisiasa baada ya kujiuzulu (political wilderness).

  Lowassa's fear is that wanasiasa kama Bernard Membe, Prof. Mark Mwandosya, Dr Hussein Mwinyi, Dr. John Magufuli na Lawrence Masha (ingawa yuko kambi ya Lowassa) watampiku kwa umaarufu ifikapo 2015 hivyo ndoto zake za kuwa Rais zitafifia zaidi.

  "Unajua msimamo wangu na malengo yangu (ya kuwa Rais 2015) bado yapo palepale," Lowassa alikaririwa akimwambia Kikwete.

  Kikwete akamjibu Lowassa kuwa basi asijali. Akamwambia kuwa kujiuzulu kwako kama PM tutasema ilikuwa ni ajali ya kisiasa tu. Akamuahidi Lowassa kuwa atamshangaza kila mtu na kumrudisha serikalini kwa kishindo baada ya uchaguzi wa 2010.

  "Don't worry my friend. I will surprise everybody kwa kukurudisha madarakani ili ujiweke vizuri na uchaguzi wa 2015," JK alikaririwa na wadau akimwambia Lowassa.

  Haikuweza kufahamika mara moja ni madaraka gani JK atampa Lowassa ili ajiweke vizuri kumrithi Urais 2015.

  Kuna tetesi kuwa JK atampa Lowassa a senior Cabinet post (uwaziri) au kumfanya ndiye Katibu Mkuu mpya wa CCM baada ya Yusuf Makamba ili akikamate chama vizuri kuelekea 2015.

  Baada ya mazungumzo na Lowassa, Kikwete ndipo akapata nguvu kwenda Dodoma kuchukua fomu za kugombea Urais kama mgombea pekee wa chama.

  Ila bado ana suspicion kuwa kundi la mtandao ndani ya CCM lililokuwa loyal kwa Lowassa na Rostam Aziz linaweza kumfanyizia. Ndiyo maana akamtuma mwanae Ridhwani afanye kazi ya kutafuta wadhamini kwa hofu ya kuwa sabotaged na kuwekewa wadhamini feki na hivyo kuwa disqualified kama candidate.

  Narudia tena, hizi ni tetesi tu. Ila inapotokea hali ambapo Rais wa nchi anamhofu ex-PM wake, tena aliye lazimika kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ina maana kuwa "this country has gone to the dogs" kama Mwalimu Nyerere alivyowahi kutuonya.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  naweza kukubali na kuthibitisha haya kwani hata mimi nimesikia kutoka vyanzo makini kabisa kuwa Lowassa lazima ataukwaa uwaziri katika serikali ijayo.hilo la ukatibu wa CCM sina uhakika nalo
   
 3. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Itakuwa upuuzi kama yatatokea. Ni jukumu letu kuzuia hali hiyo.
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Bado ni tetesi na zitabaki ni tetesi. Lakini JF huwa inapata siri nzito . Yaweza kuwa kweli. Mzee wa datas yuko ndani ya shughuli nzito za uchaguzi kiasi haonekani hapa kuleta this sort of datas. Labda naye anasubiri uchaguzi ukiisha ndipo atuletee datas zake.
   
 5. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nguvu ya watu itachukua mkondo wake, kwa uhalisia kwa nchi iliyo makini kulinda watu wake na rasimali zake swala liliomfanya EDO kujiuzulu u PM wake lilitakiwe lisiishie kuamuliwa kisiasa tu, hili swala lilitakiwa lipelekwe mahakamani na haki kuchukua mkondo wake. So kama ni kweli sidhani kama yeye Rais ana akili ningi kuliko The rest of Watanzania. Mwisho wa kulindana unakuja...Hakuna Marefu Yasiyo na ncha
   
 6. M

  Mpingo1 Member

  #6
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mpaka Oktoba 31 yatasemwa mengi sana.
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Yupo Field Marshall jamani!!! tunamuhitaji sana katika kipindi hiki muhimu
   
 8. F

  Fareed JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mimi pia nimesikia maneno haya yakizungumzwa na watu wakubwa serikalini. Wanasema kuwa Lowassa na Rostam Aziz walimweka madarakani Kikwete mwaka 2005 kupitia Mtandao kwa makubaliano kuwa Rais Kikwete atamteuwa

  Lowassa kuwa PM na kumrithisha Urais 2015. Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa habari iliyoandikwa na MwanaHalisi hivi karibuni kuwa "Kikwete amtosa Lowassa" si sahihi hata kidogo.

  Yanazungumzwa pia kuwa wamiliki na wahariri wa vyombo vikuu vya habari hapa Tanzania sasa hivi wameshaingia upande wa Lowassa na kuanzia sasa hakuna habari yoyote mbaya itakayoandikwa kuhusu Lowassa ili kumwekea mazingira ya kurudi kwenye uongozi wa kitaifa.

  Magazeti ya New Habari Corp. yanayo milikiwa na Rostam Aziz - Mtanzania, Rai, The African, Dimba, etc yamepewa amri ya kuhakikisha kuwa kuna habari na picha za kumpamba Lowassa kila siku ili asisahaulike na wananchi.

  Ukweli au uongo wa tetesi hizi tutazijua Novemba mwaka huu Rais Kikwete atakapofanya uteuzi wa Baraza lake jipya la Mawaziri!
   
 9. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Yes huo ndio ukweli ...sidhani kama the so called 'wanamtandao' wanampikia MUNGU CHAI
  mix with yours
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimemuota Lowassa leo akiwa amezungumza kwa undani sana. Ilikuwa ni siku ya mwisho ya Kikao cha Bunge ambapo hatimaye aliamua kuzungumza kwa "vipengele".

  Hotuba yake Bungeni (katika njozi yangu, na huwa nina sababu za kumuota huyu jamaa) ilichukua muda kuanza kuzama kwa wasikilizaji na matokeo yake ni aliweza kuonekana akishangaliwa na wabunge mbalimbali ambao walitambua nguvu yake na kuswitch allegiances zao. Watu wawili wakawa casualties wa move hiyo ya kisayansi ya Lowassa...

  It was just a dream but it is more than a dream.
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe kuwa itakuwa ni upuuzi lakini kwa vile Jakaya ni mpuuzi na ameshafanya mambo mengi tu ya kipuuzi kwa mfano kumteua mtu kama Sofia Simba kuwa waziri wa utawala bora wakati yeye ni mwizi wa maji ya DAWASCO basi haitashangaza Lowassa kuteuliwa kuwa waziri wa tawala za mikoa!!
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Inaelekea kama vile uzalendo umemshinda Field Marshall kwani kapotea kabisa!!
   
 13. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #13
  Jul 4, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Una uhakika gani kama atarudi madarakani,watu kama nyie mna ni kera sana yan...hamstahili hata kuishi hapa Tanzania
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  yule hawezi kurudi ndani wala kupewa uwaziri
   
 15. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Watu wenyewe akina nani? Unamaanisha watanzania? Itachukua muda mrefu sana kama siyo Karne, kwa watanzania kujua haki zao na kuzisimamia. Watanzania asili yetu ni watu wa kujipendekeza kwa wakubwa hata katika mambo ya kipuuzi. Nawaambieni hata kama Kikwete ataamua kumpa Lowassa uwaziri mkuu, wabunge wetu watampigia tena kura za kumpitisha. Waandishi wa habari watapiga blabla kwa siku mbili au tatu, halafu kimya. Kikwete alishasema, watanzania wanaojua cha kufanya ni asilimia 5 tu, asilimia 20 msimamo wa kati, na asilimia 75 ni mavuvuzela tu. Hapo ndo utarajie kwamba kuna mtu atakayepinga uteuzi huo?
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mazingaombwe ya TZ hayo.
  Akadabra akadabraaaa!
   
 17. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Akiwa katibu mkuu wa hicho chama chao chawala, mbona wasio na harufu za uanamtandao watapata tabu kidogo, huh!! Kama msambaa tu utendaji ndo huo, sasa huyu anayewekwa pale purposely kujiimarisha na c kuimarisha chama chao itakuwaje?
   
 18. D

  Domisianus Senior Member

  #18
  Jul 4, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  But we have to pay in mind Mr Edward is still very powerful and he is a leader having very strong authority, so anything it can happen at any time.Stay alerted!
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tunavyozidi kumzungumzia Lowassa na hata kumuota inamaanisha sisi wenyewe ametukaa akilini.Tuna mapenzi naye isipokuwa htunashindwa kuyasema hadharani..JK anaweza kuwa mjinga lakini sidhani kama ni mjijga kiasi cha kumrudisha Lowassa madarakani.

  Lowassa almost cost his Presidency na maadam kisha rekebisha mambo, Lowassa will remain where he is kama Mkapa na wengineo.. hao walioko madarakani leo hii wengi wao walikuwa maadui wa Lowassa toka Pinda, Mwanri, Membe hadi makatibu wakuu leo hii mnataka kunambia JK amekuwa kichaka cha kumrudisha Lowassa ambaye mwaka mmoja tu wa Utawala wake ilikuwa scandal baada ya scandal arudi tena madarakani!....

  Kumbukeni baraza la mawaziri lote la kwanza lilipitishwa na Lowassa na RA, hivyo bado wapo watu wana imani naye warudi kutawala lakini isiwe sababu ya kumweka meza moja na JK.. Jamaa kisha temwa atafanya kila alifanyalo kamaLowassa kurudi madarakani na hakika washabiki wake wapo wengi tu..
   
 20. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  mambo yanaenda yakibadilika siku hadi siku. usikate tamaa hizi ni rumours tu lakini hata kama suala hili litafanikiwa mafanikio ya chama yatapungua na itakuwa ni mwanzo wa kifo cha chama ambayo wana JF wengi wanaombea iwe hivyo
   
Loading...