Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Baada ya kusoma bandiko la Zitto hapa JF,nashauri Zitto either yeye kama yeye au kwa kushirkiana na waziri kivuli anaehusika na madini, kwa pamoja, wawaite waandishi wa habari na wawaeleze uchambuzi wao wa kina ikiwa ni pamoja na kuwapa vielelezo vya ushahidi wa watakayoyasema juu ya nini serikali ilikubaliana na wanaume wa Barrick au wawape link ingawa ni wajibu wa waandishi kutafuta habari hizi na kuwaeleza watanznia.
Nashauri hivi kwasababu yaliyokubaliwa yanapaswa kuwafikia watanzania ili wajue ni namna gani watu waliowapa dhamana wanatumia nafasi walizopewa katika kusimamia maliasili za nchi hii ili wasiendelee kudanganywa na hizi propaganda za kuwa tumepata watu wazalendo kumbe hali ni tofauti kabisa.
Sababu ni nyingine ni kuwa si watanzania wote wanaopita hapa JF au katika mitandao mingine kusoma Zitto kaandika nini au wana interest na kufuatilia mambo ya siasa na uchumi mitandaoni hivyo ni vyema kutumia vyombo vya habari kuwafikishia ujumbe huu muhimu kwani hii nchi ni yao na maliasili hizi ni mali ya watanzania na wana haki ya kujua zinatumikaje.
Naelewe kuwa,mnaweza kuongea na waandishi ila baadhi ya media ama zisiandike chochote huku baadhi zikiandika kidogo tu na kukwepa kuandika mambo ya msingi ama kutokana na hofu,kukosa uzalendo na wengine wakifukuzia uteuzi na mambo kama hayo.
Hata hivyo,vikwazo hivi visiwarudishe nyuma kwani haitakuwa sawa na kutowaita(kuna watakaondika na kusamba clip mitandaoni) na zaidi mtakuwa mmetimiza wajibu wenu kwa Taifa.
Mwisho,msiongee mambo yatayowapa sababu au visingizio vya kuwakamata(zaidi anikeni nyaraka).