Makubaliano ya kamati ya jumuiya ya madaktari na madaktari bingwa wa mnh

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
madaktari wanavyoendelea kujipanga na mgomo.kulikuwa kuna mashaka kwamba kungeweza kutokea mgongano kati ya jumuia ya madaktari iwapo kungeundwa kikundi kikingine cha kufuatilia madai yao.hivyo wamejipanga upya na sasa wamepata nguvu zaidi ya maspecialists.

MAKUBALIANO YA MKUTANO KATI YA KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI NA ‘TASK FORCE’ YA MADAKTARI BINGWA WA MNH
1. TUMEKUBALIANA KUWA KAMATI YA KUSHUGHULIKIA MADAI YA MADAKTARI NI MOJA NA HAKUNA YEYOTE MWENYE MAMLAKA YA KUKUTANA, KUJADILI AU KUKUBALIANA NA SERIKALI JUU YA MADAI HAYO ISIPOKUWA KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI AMBAYO INAJUMUISHA MADAKTARI BINGWA PIA KAMA WANAJUMUIYA.
2. TUMEKUBALIANA KUWA NA... TAARIFA YA UPOTOSHAJI JUU YA MALENGO YA TIMU HIYO YA MADAKTARI BINGWA, KIMSINGI LENGO LAO HASA ILIKUWA NI KUISHINIKIZA SERIKALI KUCHUKUA HATUA HARAKA ILI KUNUSURU HALI YA AFYA NCHINI.
3. PIA TUMEKUBALIANA KUWA KUTOKANA NA HALI YA UZOROTAJI WA HUDUMA YA AFYA TUNATOA MWITO KWAMBA KAMATI KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA MADAKTARI KUWA IPO TAYARI HATA LEO KUKAA NA SERIKALI MEZANI ILI KUFIKIA HITIMISHO YA MGOGORO HUU.
4. TUNGEPENDA SERIKALI KUACHA KUTOA VITISHO NA KUKAMATA NA KUWEKA RUMANDE BAADHI YA MADAKTARI HAPA NCHINI. KITENDO HICHO HAKITOI SULUHU YA TATIZO HUSIKA.
5. MWISHO SERIKALI ISIJARIBU KUKWEPA KUWASILIANA NA KAMATI SABABU KAMA KUNA NJIA YOYOTE YA KUFIKIA SULUHU YA TATIZO HILI NI KUPITIA KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI IMEISHATOLEWA IKIWEMO STAR TV, ITV, CHANNEL TEN, TUMAINI TV… MAGAZETI KAMA VILE THE CITIZEN, DAILY NEWS, JAMBO LEO, HABARI LEO, MWANANCHI NA KADHALIKA.
SOLIDARITY FOREVER
 
naona unafanya bidii kweli ili kuwe na machafuka nchini..it seems you are the agent of machafuko Tanzania..lol



Tatizo umekalili kwamba machafuko ni vita, mapigano n.k.; kimsingi machafuko Tanzania yapo tayari, njaa, ufisadi, elimu duni, serikali isiyo na fedha n.k.

Nikupe homework, tafuta nchi chache ambazo ziko kwenye vita kisha ulinganishe idadi ya vifo na Tanzania ( # of death/1000 kwa ujumla wake, yaani vinavyotokana na magonjwa pamoja na vita hivyo) utashangaa kuona pamoja na amani yetu tunaongoza kwa vifo kuliko baadhi ya nchi zilizo kwenye vita. Hii maana yake ni kwamba Machafuko yapo, japo sio kwa tafsiri unayoifikiria wewe!

Fanya hiyo HW!
 
tupo pamoja mdactari wwetu ila leo nimesikitishwa sana na kitendo cha wabunge wa ccm kushangilia baada ya kutoungwa mkono hoja ya inayohusu mgomo wa mdaktari.
 
naona unafanya bidii kweli ili kuwe na machafuka nchini..it seems you are the agent of machafuko Tanzania..lol
...hivi wewe Topical kwa-upeo wako huo mdogo unaona Tanzania imetulia?,achana na hizo ndoto zako za mchana,hapa hakuna utulivu bali ni uvumilivu wa kijinga ndo salama ya hawa wahuni walioko serikalini tofauti na hivyo kungukuwa kumeisha chimbika siku nyiiiiiiiiiingi...
 
toka mwanzoni madaktari wamejitahidi kukwepa swala hili kuangukia kwa wanasiasa,hawakupenda kuona chama chochote cha siasa kinateka madai yao.wameweza kwa hiyo kesho hatutegemei wabunge wagawanyike kiitukadi bali wasimame kama watanzania.
 
Back
Top Bottom