Elections 2015 Makubaliano ya Jakaya na Lowassa na hatari ya Taifa kuanguka, Onyo kwa wajumbe wa CC

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243

Makubaliano ya wawili hawa ambayo ni yamdomo chini ya viapo (Gentlemen agreement) ni suala linalotazamwa na wahusika hawa kwa jicho kali sana, msingi wa aina hii ya makubaliano unasimama katika TAMAA.

Mchezo wa mkataba huu ulianza 1995, marafiki wawili waliojulikana kwa
jina maarufu “Boys II Men” walipokodi ndege pamoja, wakaenda pamoja kuchukua fomu za kugombesa urais kwa pamoja, wakajaza pamoja, wakakodi tena ndege pamoja, wakarudisha fomu pamoja!, na wote wakapigwa chini pamoja!. Mkapa akapigiwa Upatu na Mwalimu!, akachukua nchi na kuwa rais.


Kutoka hapo, wakaunda kitu kilichoitwa Mtandao wa 2005!. Kwanza walishughulika na kilichowakwamisha wasipate ile 2005!, Kikwazo hicho ilikuwa ni Mwalimu!, na nawahakikishia 2005 mwalimu angekuwepo kundi hili
lisingegombea, angewakwamnisha tena! Mungu si Yericko wala sio Apson, Mwalimu akatangulia mbele ya haki, chini ya King Maker ambae ushindi wa umoja huo, huenda Mungu
alisikia kilio cha Jakaya na Lowasa, ni ukweli mchungu, Mwalimu alikuwa ni kikwazo kikuu kwao
na kikaondoka!.

Ndani ya CCM kuna secret code ya zamu za kupokezana Bara na Zanzibar,
na Mkristu na Musilamu, hivyo ikaamuliwa kwa vile “Mr. Clean” ni
Mkristo, then kwenye team ya “Boys II Men”, then wata mfield
Muislamu!, ila kwa vile yule Mkristo alikuwa a bit older kuliko
Muislamu,wakakubaliana “gentlemen’s Agreement” Muislamu ataingia “One
Term Presidency” ile 2005 na kumpisha mwenzake 2nd term, 2010!.

Secret code ya pili ya CCM ni akitoka rais wa Bara, anayefuatia lazima atoke Zanzibar!, mtu aliyekuwa “groomed” kumpokea
Mkapa ni yule “Daktari”, kwa vile 2005 mgombea wa CCM ilibidi
lazima awe ni Muislamu na lazima atoke Zanzibar!, hivyo huyo Mzanzibar aliyeandaliwa Dr Omar Ally Juma nae alikuwa tayari amefariki, hivyo mpango wa mtandao huo ukawa akitoka mtu wa bara, arudi
mtu wa bara kwa kisingizio hakuna mtu sahihi toka Zanzibar!,


Hivyo 2005, njia ikawa nyeupe kwa Jakaya wa Mtandao, yule Daktari
mwingine wa OAU Salim A. Salim alipoingizapua,alishughulikiwa “kikamilifu” na magazeti ya Rai na Mtanzania, aliyokuwa chini ya mtandao huo

Historia inatukumbusha kuwa aina hii ya makubaliano haijawahi kuwa na matokeo chanya tangu kuumbwa kwa ulimwengu, hii inamaana kuwa mkataba wa Jakaya na Lowasa ni taraji la mauaji mtawalia.

Tujikumbushe sehemu ya mikataba ya aina hiyo kwakuuangalia mkataba wa kuiumba Israel na chanzo cha vita ya Israel na Palestina.

adai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu kwa Wakristo na Wayahudi), kitabu cha kwanza cha nabii Musa kiitwacho Mwanzo sura ya 12 inaonesha jinsi Ibrahim anavyoitwa na mwenyezi Mungu ili kumtumikia.

Eneo hilo la Palestina (zamani lilijulikana kama Kaanani)ndiyo chimbuko la dini kuu tatu zenye msingi wa Ibrahim ambazo ni dini ya Wayahudi, Ukristo na baadaye Uislam.

Dini ya wayahudi yenye misingi ya Biblia Agano la Kale likianza na vitabu vitano vya Musa (Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la torati), Ukristo ukianza misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislam ukishika vitabu vinne Tourat ya nabii Musa (a.s), Zabur ya nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Quran ya Muhamad (s.a.w)

Ibrahim mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia) leo Iraq wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran Syria na baadaye kutelemkia Kaanani (Uyahudi) ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa baraka yaani kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia.

Pamoja na ahadi hiyo Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani Misri kwa miaka mia nne hadi kizazi cha nne ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani (Palestine).

Mizizi ya ugomvi huo inaanzia karne ya 19 wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu (Arab nationalism) vuguvugu la wayahudi (Jewish National Movement) lilianzishwa kuwa la kisiasa mwaka 1892 dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa wayahudi wote popote walipo kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndiyo nchi yao ya asili.

Katika kutimiza azma yao World Zionist Organization na Jewish National Fund walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza katika Palestina.

Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza kwa kile kilichafahamika kama Hussein-McMahon Correspondence na Balfour Declaration of 1917, na kufuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara kati ya Wayahudi na Waarabu katika eneo la Palestina.

Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Wanazi Adolf Hiltler alivyowafanyia wayahudi kwa maangamizi makuu ya Nazi Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo..

Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947 liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa wayahudi na wapalestina ambapo wayahudi walikubali na wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za kiarabu wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao.

Vita hivyo viliwafanya wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba.

Israeli ilijitangazia uhuru wake Mei 14 mwaka 1948 kufuatia uhuru huo mataifa ya kiarabu Misri, Lebanon, Syria, Jordan na Iraq yaliivamia Israeli na kuzuka vita ya iliyojulikana kama 1948 Arab-Israel war. Israeli iliibuka kidedea ikiyateka maeneo zaidi ya ramani ya awali na kugawa mji wa Yerusalem.

Mwaka 1964 wapalestina walianzisha chama cha Palestinian Liberation Organization (PLO) ambacho hakikutambuliwa na Israeli.

Katika vita vya Siku Sita 1967 vya Israeli na waarabu ambavyo Israeli ilishinda kwa kishindo ikiacha hasara kubwa kwa maadui zake viliifanya nchi hiyo kujiongezea ukubwa mara tatu ya ule wa awali.

Siri ya ushindi wa vita hivyo ulitokana na mbinu na maandalizi mazuri yaliyokuwa yamefanywa na hasa ni kule kuvamia kabla ya adui hajakushambulia. Kama wangesubiri washambuliwe basi Israeli ingefutwa katika ramani ya dunia kama waarabu walivyokuwa wameazimia.

Vita hiyo ya 1967 Israeli ilipigana na Misri, Syria, Lebanon, Jordan zikisaidiwa kijeshi na Sudani, Iraq, Algeria nchi zilizopeleka askari na silaha, Urusi ikisaidia mataifa hayo kwa wingi wa silaha.

Kabla ya vita mataifa ya Marekani, Uingereza na Ufaransa yalipeleka silaha kwa Israeli na kuifanya isiwe na wasiwasi katika matumizi ya silaha.

Nini chanzo cha vita hiyo? Israeli na majirani zake walikuwa wakiishi katika hali ya uhasama tangu 1948 baada ya azimio la umoja wa mataifa la mwaka1947, lililoamuru kugawanywa kwa nchi hiyo, waarabu walikuwa bado wanayo hasira juu ya uwepo wa taifa hilo mashariki ya kati.

Viongozi mbalimbali wa nchi za kiarabu waliazimia kuifuta Israeli kwenye ramani ya dunia. Israeli iligombana na Syria ilipoanza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji kuyatoa mto Jordan na kusambaza katika nchi hiyo. Jeshi la Syria likatumia milima/miinuko ya Golan ilinayopata futi 3000 juu ya Galilaya kushambulia vijiji na mashamba.

Mashumbulio ya Syria yaliongezeka sana mwaka 1965 -66, Israeli ikilalamika Umoja wa Mataifa ambao ulisisitiza kuacha mapigano bila kuchukua hatua yoyote kwa Syria ambapo hata ulipotoa azimio la kulaani mashambulizi hayo yalipingwa kwa kura ya veto na Urusi.


Mashambulizi hayo yalienda sanjali na vitendo vya kigaidi dhidi ya taifa hilo ambapo mwaka 1965 Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser alisema “hatutaingia Palestina nchi ikiwa imefunikwa kwa mchanga bali damu”. Baada ya miezi michache Nasser alisema tena kuwa azma ya waarabu ni kuona wapalestina wanakombolewa, kwa kifupi ni kuiondoa dola ya kiyahudi kwa maangamizi.
Aprili 7, 1967 Syria ikitumia ndege aina ya MiG21 ilizokuwa imepewa na Urusi ilishambulia vijiji (kibbutzim) kutokea Miinuko ya Golan, Jeshi la Israeli lilitungua ndege sita za Syria.


Urusi iliipa taarifa isiyo sahihi Syria kuwa Israeli inajiandaa kwa vita licha ya Israel kukanusha lakini Syria ilijipanga ikiweka makubaliano ya ushirikiano na Misri.


Tarehe 15 Mei, 1967 siku ya uhuru wa Israeli, majeshi ya Misri yalivuka kuelekea Sinai karibu na mpaka na Israeli ambapo siku tatu baadaye tarehe 18 jeshi la Syria likajipanga kwa vita katika milima ya Golan.


Baada ya majeshi ya Misri na Syria kujipanga kwa vita, Gamal Abdel Nasser aliamuru jeshi la umoja wa mataifa UN Emergency Force (UNEF), lililokuwa Sinai likiikinga Israeli tangu 1956 kuondoka mara moja bila kushirikisha umoja huo.


Mei 22, Misri ilifunga mlango bahari wa Tiran na kuzuia meli zote za kutoka mashariki kuingia Israeli na kuzuia meli za Iran zilizokuwa zinapeleka mafuta ya petroli na kuifanya nchi hiyo kutokuwa na njia inayopitika (uamuzi wa Misri ulikiuka sheria za kimataifa).


Radio Sauti ya Waarabu ikisema “kwa kuwa sasa jeshi la kimataifa lililokuwa linaikinga Israeli limeondoka hatutavumilia zaidi wala kulalamika umoja wa mataifa ila jambo moja tutakalofanya ni kuipiga vita na kutokomeza siasa za kizayuni”.


Naye waziri wa ulinzi wa Syria Hafez Assad alisema “majeshi yetu yako tayari kuifuta Israeli” nakuu kwa kimombo ‘Our forces are now entirely ready not only to repulse the aggression, but to initiate the act of liberation itself, and to explode the Zionist presence in the Arab homeland. The Syrian army, with its finger on the trigger, is united....I, as a military man, believe that the time has come to enter into a battle of annihilation” alisema hayo Mei 20, 1967.


Rais wa Marekani Johnson alilaani na kusema kitendo cha Misri ni kinyume na sheria ya bahari iliyopitiwa mwaka 1958 ambapo umoja wa mataifa ulitambua haki ya Israeli kutumia mlango bahari wa Tiran (Straits of Tiran) kupitisha meli.


Nasser aliendelea na vitisho akiitaka Israeli kuingia vitani akidai kuwa hawatasikiliza shauri lolote la masikilizano kwani wao wako vitani na Israeli tangu mwaka 1948. Aliongeza kusema kuwa majeshi ya Misri, Jordan, Syria na Lebanon yametulia mipakani mwa Israeli na nyuma yao yapo majeshi ya Iraq, Algeria, Kuwait, Sudan, Saudi Arabia na ulimwengu wote wa kiarabu. Alijigamba zaidi kwa kusema kwa tendo hili dunia yote itastaajabia na kujua kuwa waarabu wapo wamejizatiti kwa vita.


Rais wa Iraq Abdur Rahman Aref alisema “Uwepo wa taifa la Israeli ni kosa ambalo ni lazima lirekebishwe, huu ni wakati wa kufuta aibu ambayo tumekuwa nayo tangu 1948, lengo letu ni kuifuta Israeli kwenye ramani”. Iraq ilipeleka majeshi yake Juni 4 kujiunga na Misri, Jordan na Syria.


Majeshi ya kiarabu yanayokadiliwa askari 465,000, zaidi ya vifaru 2,800, na ndege 800 viliizunguka Israeli.


Kipindi hicho Israeli ilikuwa kwenye hali ya tahadhari kwa wiki tatu muda huo iliutumia kuingiza silaha toka mataifa ya magharibi Marekani, Ufaransa na Uingereza. Silaha zilishushwa katika mji wenye bandari wa Haifa.


Israeli kwa kuwafahamu adui zake walivyo waliwafanyia kamchezo ka hadaa, kwanza ilifungua mpaka wake na Misri ili kuruhusu wapelelezi wa Misri kuingia na kutoka. Pili oparesheni ya kuhamisha silaha zilizowasili katika mji wa Haifa wakazipeleka ghuba ya Aqaba eneo lenye pori na miamba wakati wa mchana na kuzirudisha Haifa usiku na kuzihifadhi kwenye mahandaki.


Jambo jingine lililowasaidia Israeli ni hadaa iliyofanywa, Waarabu walipotangaza vita na kuitisha Israeli, iliwaita makamanda wote waliokuwa likizo kurudi kazini na mawaziri waliokuwa ziarani kurudi mara moja, jambo lililofanywa na Misri pia.


Baada ya wiki hizo tatu za maandalizi ya nguvu Israeli ikatangaza kuwa makamanda waliokuwa likizo waendelee na likizo zao inaonesha waarabu walikuwa wanawatisha tu hakutakuwa na vita.
Kipindi hicho Marekani ilijaribu kuzuia vita kwa kuishauri Misri kusitisha mpango wa vita lakini haikuwezekana kumshauri raisi wa Misri Gamal Abde Nasser hali iliyomfanya Rais wa Marekani Johnson kuonya kuwa “Israeli haitakuwa pekee vitani labda ikitaka kuwa hivyo”


Juni 5, 1967 waziri mkuu wa Israeli Levi Eshkol aliamuru kuishambulia Misri, hapo Israeli ilikuwa peke yake, lakini yenye makamanda waliojizatiti kwa mkakati maalum. Jeshi lote la anga la Israeli ukiacha ndege 12 tu ziliachwa kulinda anga la Israeli, majira ya saa 1.14 asubuhi (saa moja asubuhi) walipiga mabomu viwanja vyote vya ndege za kivita vya Misri wakati marubani wa ndege hizo wakipata kifungua kinywa.


Ndani ya masaa mawili ndege 300 za Misri zilikuwa zimeshapigwa mabomu na kuharibiwa kabisa, masaa machache baadaye ndege za Israeli zilishambulia majeshi ya anga ya Jordan na Syria na kiwanja kimoja cha Iraq.


Jioni ya siku ya kwanza ya vita ndege zote za Misri na Jordan na nusu ya ndege za Syria zilikuwa zimeharibiwa zikiwa viwanjani. (ujanja wa kuzipiga zikiwa kwenye hanger kabla hazijaruka ulitumika).


Misri iliyokuwa na nguvu za kijeshi na jeshi kubwa la ardhini lenye vifaru na magari ya vita ilianza matayarisho ya kuyavusha kwenye mfereji wa Suez (madarajani) likafauru kuvusha askari 20,000 hadi penisula ya Sinai.


Israel ikiwa inaangalia mwenendo wote wa majeshi ya Misri iliacha operesheni hiyo ifanyike ya uvushaji askari na silaha kuelekea Sinai na kisha ikatuma ndege zake kuvunja madaraja ya Suez na kuhakikisha hakuna msaada wa kijeshi wala chakula utakaovuka kusaidia kikosi kilichokwisha vuka.


Kisha vilianza vita vya ardhini ambapo mapigano makubwa ya kihistoria ya vifaru yalitokea baina ya majeshi ya Misri na Israeli katika jangwa la Sinai.


Baada ya Jordan kushambuliwa wapalestina wapatao 325,000 walioishi Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan walilazimika kukimbia na kwenda nchini Jordan kuepuka vita.


Kikosi kidogo cha mashujaa wa Israeli kiliwekwa kuzuia majeshi ya Syria wakati vita vikali vikiendelea baina ya Israeli na Misri na Jordan hadi walipoona wamedhoofisha majeshi hayo ndipo kikosi kizima cha jeshi la anga kiliposhambulia ngome ya Syria kwenye milima Golan, Juni 9, baada ya siku mbili za mashumbulizi ya nguvu (heavy bombardment) walifaulu kupenya safu ya Syria.
Baada ya siku sita za mapigano Israeli ilikuwa na uwezo wa kuingia Cairo, Damascus na Amman bila kikwazo, wakati huo lengo la kuiteka Sinai na Miinuko ya Golan lilikuwa limefikiwa. Viongozi wa Israeli hawakuwa na nia ya kupiga miji mikuu ya nchi hizo, jambo ambalo walikuwa na uwezo nalo.
Zaidi ya hayo Urusi ikiwa imechanganyikiwa na mafanikio ya Israeli ikawa inatishia kuingilia vita. Wakati huo waziri wa Mambo ya nje (Secretary of State kama wanavyomwita) wa Marekani Dean Rusk aliishauri Israeli kukubali wito wa kusimamisha mapigano, Israeli ilikubali Juni 10 ilisimamisha mapigano.


Ushindi wa Israeli uliigharimu. Katika kushambulia milima ya Golan wanajeshi 115 wa Israeli walipoteza maisha ikipoteza ndege 46 kati ya 200 wakati upande wa waarabu Misri askari 15,000, Syria 2500 na Jordan 800.


Mwisho wa vita Israeli ilikuwa imejiongezea ukubwa wa eneo mara tatu kutoka maili za mraba 8000 hadi 26,000, ushindi huo uliifanya Israeli kuutwaa mji wa Yerusalem, mkono bahari wa Sinai, Golan Heights, Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.


Licha ya vita hiyo Israeli iliwashauri wapalestina kuendelea kuishi chini ya utawala wa Israeli ambapo baadhi ya familia za wapalestina zilizokuwa zimetengana waliweza kuungana na wengine hawakuwa na imani na Israeli.


Mwezi Novemba 1967, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio na 242 lililowataka Israeli na Waarabu kuwa na amani ambapo Israeli ilitakiwa kuondoka katika Ardhi ilizoteka kwa makubaliano ya kuwa na amani na majirani zake.


Mwandishi maarufu wa habari za Waarabu katika Israeli Don Peretz aliyetembelea Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan siku chache baada ya vita alithibitisha kuona jinsi Israeli ilivyojitahidi kurejesha hali ya kawaida ya maisha na kuzuia kuhama kwa waarabu maeneo hayo.

Mgogoro mwingine uliibuka mwaka 1973, vita vilivyojulikana kwa jina la Yom Kippur, waziri mkuu wa Israeli akiwa Golder Meir (Iron Woman) ambavyo Israeli ilipigana bila ya maandalizi yoyote kwani ilishambuliwa kwa kustukizwa.

Golder Meir ambaye alichaguliwa kuchukua nafasi ya Levi Eshkol kufuatia kifo chake cha ghafla Februari 26, 1969 na Meir kuanza kazi hiyo Machi 17 mwaka huo akiwa na sifa kem kem ikiwepo ya kufanikisha serikali ya mseto mwaka 1967 baada ya vita ya siku sita chama cha Mapai kilijiunga na vyama vingine vya Rafi na Ahdut HaAvoda na kuunda Israel Labour Party.

Ni katika kipindi cha Golder Meir kabla ya vita ya Yom Kippur yalitokea mauaji ya wanamichezo wa Israeli huko Ujerumani waliposhiriki michezo ya Olimpiki 1972 (1972 Summer Olympics) mauaji yaliyojulikana kama Mauaji ya Munich (Munich massacre) ambapo jumla ya wanamichezo 11 waliuawa na kikundi cha wapalestina kiliichoitwa Black September Organization.

Kwa ujasiri mkubwa baada ya kuona jumuia ya kimataifa haijachukua hatua stahili, Golder Meir aliamuru shirika lake la kijasusi Mossad kuwasaka na kuwaua wote walioshiriki kupanga mauaji hayo ambayo watekaji nyara walidai kuachiwa huru kwa wafungwa 363 wa kipalestina na wengine walioshikiliwa katika magereza ya Israeli. Operasheni hiyo ilijulikana kama Operesheni Ghadhabu ya Mungu au Operesheni Singe. ( Operation Wrath of God au Operation Bayonet)

Katika operesheni hiyo ambayo ililenga kulipiza kisasi kwa wote waliohusika kupanga mauaji hayo wakiwepo baadhi ya wanachama wa kundi la PLO na Black September Organization ambapo mauaji yalitekelezwa kwa siri na kundi la watu 15 waliogawanywa katika squad tano.

Vita ya Yom Kippur au Ramadhan war au vita vya Oktoba kama vinavyojulikana vilipiganwa toka Octoba 6 hadi 26 mwaka 1973 umoja wa mataifa ulipoilazimisha Israeli kusimamisha vita na hasa baada ya Israeli kukizingira kikosi kikubwa cha tatu cha Misri (Third Army).

Mwanzoni waarabu walionekana kushinda vita na kusababisha hasara kubwa kwa jeshi la Israeli lakini upepo uligeuka ambapo Israeli iliwapiga adui zake na kupenya hadi ukingo wa magharibi wa bahari ya Shamu (walivuka mfereji wa Suez)

Hata hivyo Idara ya Usalama ya Israeli ililaumiwa kwa kutokuwa makini kwani walionywa mara kadhaa kuhusu kusudio la waarabu la kuishambulia Israeli.

Vilianza kwa mashambulizi ya ghafla ya Misri na Syria siku ya sikukuu kubwa ya wayahudi ya kidini ambapo mataifa hayo mawili yaliishambulia Israeli kwa nguvu na kuonekana kama watashinda vita katika masaa 24 hadi 48 ya kwanza baada ya hapo hali iligeuka.

Katika wiki ya pili ya mapigano Syria ilikuwa imesukumwa kutoka milima ya Golan na kwa upande wa Misri vikosi vilisukumwa hadi kusini mwa Sinai na kisha kikosi cha Israeli kikapenya kati ya vikosi viwili vya Misri na kuvuka mfereji wa Suez na kukizingira kikosi cha tatu (Third Army) cha Misri.


Jeshi la Misri lililokuwa limevuka mfereji wa Suez (mpaka wa vita vya 1967, mstari wa kusimamisha mapigano) likajigawa Ukanda wa Gaza na kusini ukingo wa mashariki wa Suez likavunja ngome iliyojengwa iliyoigharimu Israeli USD 500 ambayo ilipewa jina la Bar Lev Line kwa heshima ya Jenerali Chaim Bar-Lev.


Kuzingilwa kwa kikosi huko kuliipa nguvu Israeli wakati wa mazungumzo yaliyokuwa kiini cha mkataba wa Camp David, Israeli ilitaka kukiangamiza kikosi hicho ambapo Misri ilibidi ijisalimishe ili kuokoa maisha ya wanajeshi wapatao 20,000.


Marekani ilitumia mwanya huo kuilazimisha Misri kufuta maombi ya msaada iliyokuwa imeomba toka Urusi na kuahidi kuisaidia na hivyo kupunguza ushawishi wa Urusi eneo hilo ambapo mambo yalihitimishwa kwa mkataba wa Camp David uliopatanisha Israeli na Misri hadi leo.
Baada ya kifo cha Gamar Abde Nasser rais wa Misri alitawala Anwaar Sadat ambaye alikuwa ametangaza mwaka 1972 kuwa ameamua kuingia vitani na Israeli na kwamba ameandaa wanajeshi milioni moja ambao wako tayari kujitoa muhanga ili kukomboa maeneo ya Sinai.


Kwa kauli hiyo mwishoni wa 1972 alinunua ndege za kivita MiG-21, makombora ya kutungulia ndege ya SA-2, SA-3, SA-6 na SA-7 , na vifaru aina ya T-55 na T-62, silaha za kulipulia vifaru RPG-7 na makombola ya vifaru ya AT-3 kutoka Urusi.


Sadat akiipa jina la Operesheni Badr (neno la kiarabu lenye maana ya mwezi mpevu) akilinganisha na Vita vya Badr ambavyo waislam waliwashinda Wakuraish wa Maka akikusudia kurudisha heshima ya Waarabu waliyopoteza katika vita ya 1967.


Habari za kijasusi ziliifikia Israeli kuwa Misri ilipanga kuivamia Israeli lakini isingefanya vile bila kupokea ndege za MiG-23 na makombola ya Scud ambayo yangetumika kuibomoa miji ya Israeli.
Taarifa hiyo iliifanya Israeli isiwe makini na kudhani vita isengetokea katika muda mfupi hivyo.
Mikakati ya vita iliyofanywa na Sadat na mwenzie Assad wa Syria ilikuwa kuivamia Israeli siku ya sikukuu kubwa ya Yom Kippur ambapo ilikuwa ni siku ya mapumziko, hakuna kuwasha mioto wala kuendesha magari na hivyo kufanya kila kitu kuwa kimya kabisa.


Hali hiyo iliwasaidia Israeli kwani walipovamiwa ghafla iliwawia rahisi kutumia barabara kujipanga haraka kwani hakukuwa na msongamano wa magari barabarani, pia iliwakusanya maaskari wa akiba kirahisi kwani wengi walikuwa kwenye masinagogi wakisali.


Mbinu nyingine iliyotumiwa na Misri ni kuwapa likizo maaskari wa akiba ambapo Nasser aliruhusu askari 20000 kwenda mapumzikoni na wengine kwenda Hija.


Usiku wa Septemba 25 mfalme Hussein wa Jordan aliruka kwa ndege kwa siri hadi Tel Aviv kumwonya waziri mkuu wa Israeli Golder Meir juu ya shambulio lililopangwa dhidi yake jambo ambalo walipuuza.


Mwezi huo Israeli ilipata maonyo kumi na moja toka vyanzo vya kuaminika lakini mkuu wa Mossad Zvi Zamir alipuuza. Lakini Golda Meir, Moshe Dayan, na Jenerali wa Israeli David Elazar walikutana saa 2:05 asubuhi ya siku ya Yom Kippur, masaa sita kabla ya shambulio.


Golder Meir alikataa kuanzisha shambulio akihofia kutopata msaada wowote toka nje. Wakati huo nchi za Ulaya zilikuwa zimeacha kuisaidia Israeli silaha. Mara waziri huyo alipotoa uamuzi alipokea ujumbe kutoka kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Henry Kissinger kuwa Israeli isishambulie isubiri tu.

Vita hiyo ambayo kwa sehemu kubwa Israeli ililemewa na kupata hasara kubwa kwani katika masaa 27 ya kwanza ilikuwa imepoteza ndege 30 na vifaru 300 katika shambulio la Misri la Bar-Lev huku jeshi hilo la Misri likiwa limesonga mbele kwenye jangwa la Sinai kilomita tano.

Israeli ilibidi ibadili mbinu za kivita kwani makombora ya ulinzi wa anga ya SAM yaliwazidi nguvu, wakaamua kutumia jeshi la miguu (Infantry), kikosi hicho kilifaulu kwa sehemu kubwa hadi kupenya hadi kwenye safu yalikowekwa makombola hayo na kuyaharibu na hivyo kudhoofisha mfumo wa kujikinga wa Misri.

Baada ya kudhoofisha mfumo huo wa ulinzi ndipo jeshi la anga la Israeli likazidisha mashambulizi. Siku iliyofuata, Oktoba 15, Israeli ilianzisha Operesheni Abiray-Lev (yaani stout-hearted men au operesheni ya majasiri/mashujaa).

Divisheni iliyoongozwa na Meja Jenerali Ariel Sharon ilishambulia safu za jeshi la Misri eneo la Ismailiya kati ya kikosi cha pili kilichokuwa kaskazini na cha tatu kusini (Second and Third Army) na kufaulu kupenya hadi Suez na kuvuka.

Baada ya siku chache Israeli ilijenga madaraja manne kuvuka mfereji wa Suez mwisho wa vita Israeli ilikuwa ndani ya Misri kilomita 101 kutoka mji mkuu wa Misri Cairo.

Kwa upande wa Syria hali ilikuwa tofauti kidogo, pamoja na kuwa na silaha kama zile za Misri vita vilikuwa vikali ambapo ndege za Israeli zikikwepa kutunguliwa zilikuwa zikipita uwanda wa chini wa Jordan kisha kuibukia Syria na vifaru vingi vilipelekwa huko.

Viongozi wa Israeli waliithamini sana milima ya Golan na hivyo kupeleka nguvu zote hapo kwani jeshi la Syria lingefaulu kuteka milima hiyo ingelikuwa rahisi kupita hadi Tiberias, Safed, Haifa, Netanya, na Tel Aviv.

Askari wote wa akiba walipelekwa milima ya Golan wakipewa vifaru na kuendelea na mapambano, hapo ndipo alipoibuka shujaa wa vita hivyo Luten Zvika Greengold ambaye alifika jioni hiyo kwenye uwanja wa mapambano, alikuwa peke yake akitumia kifaru chake kupambana na majeshi ya Syria akiyapiga hadi msaada ulipofika.

Masaa 20 baadaye Zvika Force jina alilobatizwa alitumia kifaru chake kuingia katikati ya vifaru vya Syria na kuvipiga huko na huko ambapo alibadili vifaru sita, wakati mwingine akijichanganya na kikosi cha vifaru mara nyingine peke yake, alijeruhiwa, aliunguzwa moto lakini aliendelea na mapambano kwa kitendo hicho Zvika alitangazwa kuwa shujaa wa vita hivyo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio namba 338 la kusitisha vita baada ya Marekani na Urusi kukubaliana Oktoba 22 ambalo lilianza kutekelezwa masaa 12 baadaye.

Baada ya kuanza utekelezaji wa azimio hilo Misri ilishambulia mara kadhaa vikosi vya Israeli ikiharibu vifaru 9, kwa kulipiza kisasi Israeli ilielekeza majeshi yake kusini na kukizingira kikosi cha tatu cha Misri baada ya Jenerali David Elazar kuomba idhini toka kwa Moshe Dayan kwani zoezi la kusimamisha mapigano lilianza kutekelezwa wakati Israeli imebakiza mita chache kufikia malengo wakateka barabara kuu ya Cairo kwenda Suez.

Asubuhi ya Oktoba 23, Urusi iliilaumu Israeli kwamba majeshi yake yalionekana yakielekea kusini Henry Kissinger akampigia simu Golder Meir kuwa unawezaje kutambua mstari wa kusimamisha mapigano jangwani ambapo Meir alimjibu kuwa wote watajua tu akiwa na maana watajijua na jeuri yao, muda mfupi baadaye Kissinger alipata taarifa za kuzingirwa kwa kikosi cha tatu (Third Army).


Kissinger aligundua kuwa hiyo ni nafasi ya pekee kwa Marekani kuibana Misri ili kuiondoa kwenye ushawishi wa Urusi, kwa kweli Misri haikua na ujanja wowote zaidi ya kuitegemea Marekani kuizuia Israeli isikiangamize kikosi kilichozingirwa ambacho hakikuwa na chakula wala maji.

Wakati huo Rais wa Urusi Leonard Brezhnev alimtumia barua Rais wa Marekani Richard Nixon akisema kuwa Urusi na Marekani kwa pamoja visimamie usitishaji huo wa mapigano vinginevyo Urusi ingeingilia kuisaidia Misri.
Urusi ilikuwa imeshaandaa vikosi na baadhi yake ikawa imevisafirisha toka Urusi hadi kwenye kituo chake cha kijeshi cha Yugoslavia na kupeleka kikosi cha wanamaji 40,000 kwenye bahari ya Mediterrenea.


Kwa bahati mbaya barua hiyo ilifika Nixon akiwa amelala hivyo Kissinger na maafisa wengine wa Ikulu akiwemo Katibu wa ulinzi James Schlesinger, Mkurugenzi wa CIA William Colby na Mkuu wa WhiteHouse Alexander Haig (Kashfa ya Watergate ikiwa kileleni) waliishughulikia.


Wakubwa hao bila kumshirikisha Rais Nixon wakajibu kwa jina la Nixon kwa Urusi na kuiambia Misri ijitoe katika ushawishi wa Urusi vinginevyo Urusi ikiingilia na wao wataingia vitani, hilo likawa tishio la vita ya tatu ambayo ingekuwa ya Nuclear.



Urusi ilishangaa na hofu iliyowakumba Marekani hata mkuu wa KGB Yuri Andropov akasema hali ni tete hatuwezi kuruhusu vita ya tatu.


Asubuhi yake Misri ilikubali ushauri wa Marekani na kutangaza kufuta ombi la msaada iliyokuwa imeomba awali na Urusi ikakiri kushindwa vita kwa waarabu na huo ukawa ndiyo mwisho wa mgogoro.


Kutekelezwa kwa wito wa kusimamisha mapigano baina ya Misri na Israeli kuliichanganya Syria iliyokuwa imejiandaa upya kuishambulia Israeli tarehe 23 Oktoba baada ya kutafakari ikajua kuwa nguvu yote ya Israeli ingehamia kwake na kupiga Damascus hivyo Assad akatangaza kusimamisha mapigano Oktoba 23, na Iraqi ikawarudisha nyumbani askari wake.


Hata hivyo baada ya vita hiyo Golder Meir alijiuzulu kufuatiwa lawama za kutojiandaa kwa taifa hilo kivita (utayari wa vita) baada ya tume ya Agranat Commission kuelekeza lawama zote kwake na Yitzhak Rabin akamrithi mnamo Juni 3, 1973.


Mwaka 1975, Meir alituzwa Tuzo ya Israeli ( Israel Prize ) kwa mchango wake maalum kwa taifa la Israel. Alifariki Disemba 8, 1978 kwa saratani mjini Jerusalem akiwa na umri wa miaka 80.

Kwanini nisiunge mkono taifa teule, nchi ya ahadi yenye maziwa na asali?

Atakaye ubariki uzao wa Israel naye atabarikiwa, atakayeulaani uzao wa Israel naye atalaaniwa daima.


Baada ya hapo sasa tuangalie aina nyingine ya mfano wa mkataba huo, hapa tunaangaza barani Afrika katika mkataba wakuunda taifa teule la Watusi chini ya Lemera.


Kinachoitwa vita vya sasa nchini Kongo ni utekelezaji wa “Makubaliano ya Lemera” ya mwaka 1996 yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa kuliko yoyote ile Afrika Mashariki na Kati.

Makubaliano yalifanywa kati ya Laurent Desire Kabila, akiwa kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” kutoka utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja; na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo.

Makubaliano ambayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na kujulikana kwa jina hilo, yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi.

Taarifa zilizopo zinaonyesha makubaliano yaliandaliwa mapema mjini Kigali na pale Lemera yalikuwa yanazinduliwa tu. Ilikubaliwa wakati huo kwamba hiyo ndiyo ingekuwa “asante” kwa Rwanda “kwa ukombozi wa Kongo.”

Desire Kabila alikuwa tayari amechoka. Kwa takriban miaka 20 alikuwa akipambana na utawala wa Mobutu Sese Seko. Alikuwa amefikia hatua ya kukata tamaa na kutulia jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1996, mjini Kigali, Rwanda kilikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita “wapinzani wa dikiteta Mobutu.” Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengine waliokuwa wakiishi mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo.

Katika kundi hilo alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kisasi Ngando; askari mtaalam wa kusomea. Anadaiwa kupata mafunzo nchini Cuba, Ujerumani na Bulgaria. Alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho.

Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji. Mungu akupe nini! Hakuna uthibitisho wowote, lakini taarifa zinaeleza kiliomba ushauri wa Mwalimu Julius Nyerere “ambaye aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji.”

Mwanzoni mwa vita ya kumg’oa Mobutu kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge. Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa “maasi ya Wanyamulenge.”

Wanyamulenge ni watu wanaodaiwa kutoka kwenye vilima vya Mulenge vilivyoko wilaya ya Uvira katika mkoa wa Kivu Kusini. Makabila ya asili ya hapa ni Wavira na Wafuliro. Wanaojiita Wanyamulenge ni Wanyarwanda wakuja.

Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo; inawanyanyasa na inawanyima uraia. Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji.

Wapinzani, chini ya Jenerali Andre Kisasi Ngando, na msemaji mkuu wao Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma. Wakavuka Ziwa Kivu na kuingia Kivu Kusini.

Ilikuwa baada ya kukamata mji wa Bukavu, makao makuu ya Kivu Kusini na sehemu nyingi za mkoa huo, wapiganaji wa Kinyarwanda waliingiza pendekezo la rais ajaye wa Kongo, kutoa Kivu Kaskazini na Kusini kwa Rwanda.

Lakini kabla suala hilo nyeti kupewa uzito unaostahili, wapiganaji wa Kinyarwanda, baada ya kuteka Bukavu, wanadaiwa kuanza kupora mali – magari, vifaa vya nyumbani, dawa katika maduka – hatua ambayo ilielezwa kuwa uhamishaji wa mali za wakazi wa Bukavu na maeneo mengine.

Alikuwa Jenerali Ngando anayeripotiwa kupinga uporaji usiomithilika, jambo ambalo lilimletea uhasama kwa baadhi ya wapiganaji. Kuona hivyo, Laurent Kabila akamwasi Ngando.

Ngando anasemekana kuuawa siku chache baada ya kutofautiana na wapiganaji juu ya uporaji. Inaelezwa kuwa alimiminiwa risasi na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto katika mbuga ya wanyama ya Virunga.

Kabila aliulizwa mara nyingi juu ya Ngando. Alikuwa na majibu tofauti. Akiwa bado msituni alisema Jenerali Ngando amekamatwa na majeshi ya serikali na mara ametekwa na wanamgambo wa Mai Mai.

Baadaye Kabila alisema Ngando alijeruhiwa na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu. Na wakati akiwa rais, aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa Ngando alikuwa askari kama askari wengine na kwamba alikufa kwenye mapambano.

Ilikuwa baada ya kifo cha Jenerali Ngando ndipo Kabila aliingizwa kwenye makubaliano ya kumega Kongo. Kwanza, kikundi cha wapiganaji kiligeuzwa kuwa chama – AFDL – Alliance de front Democratique pour la Liberation du Congo.

Kabila akapanda cheo na kuwa kiongozi wa chama cha ukombozi wa Kongo kutoka kuwa msemaji tu wa wapiganaji.

Baada ya kuundwa kwa AFDL, jina la Wanyamulenge likatoweka kabisa. Wapiganaji wakaitwa waasi wa Kongo. Taarifa zinasema kabla wapiganaji kutoka Bukavu na kuanza safari iliyomfikisha Kabila madarakani, waliingia katika mkataba ambao ndio umekuja kuitwa “Makubaliano ya Lemera.”

Kuna madai kwamba viongozi wakuu wa wakati huo wa baadhi ya nchi walipata nakala ya makubaliano hayo ya kumega Kongo. Miongoni mwa nchi hizo ni Namibia, Uganda, Burundi, Zambia, Ethiopia, Eritrea, Zimbabwe, Angola, Namibia, Sudan na baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani.

Imeelezwa kuwa makubaliano ni pamoja na kufanya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini kutawaliwa na Wanyarwanda wa Kitutsi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda; na kwamba utawala huo ambao ungefanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Kabila, ungetekelezwa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 1998.

Chini ya mpango huo, raia wa Kongo, wakazi wa Kivu Kaskazini wangehamishiwa Kivu Kusini, “taratibu na kwa utulivu huku makazi yao yakichukuliwa” na wavamizi.
Imeelezwa kuwa hatua ya kwanza isingekuwa ngumu kwani Rwanda ingedai kuwa inapambana na wanamgambo wa Kihutu walioitwa Interhamwe ambao itaelezwa kuwa wanatishia amani nchini Rwanda. Hivyo ndivyo imekuwa ikifanya hadi sasa.

Makubaliano yanadaiwa kueleza kuwa kuchukuliwa kwa miji ya Goma na Butembo mkoani Kivu Kaskazini, sharti iwe hatua ya kwanza kwa kuwa hayo ndiyo maeneo yenye upinzani mkubwa. Kufanikiwa kwa awamu ya pili, kungetegemea mafanikio ya awamu ya kwanza, makubaliano yanadaiwa kueleza.

Wafuatiliaji wa mahusiano ya Rwanda na Kongo wanasema ingawa mpango huo ulishindikana kutekelezwa kuanzia mwaka 1998, kuingia kwa majeshi ya Rwanda nchini humo hivi sasa, ni utekelezaji wa hatua ya kwanza ya Makubaliano ya Lemera; na tayari miji ya Goma na Butembo iko chini ya kile kinachoitwa “majeshi ya ushirikiano” ya Rwanda na Kongo.

Kwa mujibu wa masimulizi juu ya makubaliano hayo, awamu ya pili ingekuwa kujaza wakazi wa Kaskazini katika Kivu Kusini na kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wazawa wangeenguliwa, kukosa uongozi na hivyo kunyimwa sauti.

Hatua nyingine ilikuwa kuanzisha benki ya kusaidia wavamizi katika Kivu mbili, kujenga nyumba zipatazo 600,000 na kujiimarisha katika nchi ya kigeni – Kongo.

Imeelezwa kuwa Kabila alikubaliana na masharti ya makubaliano kwa kuwa lengo lake lilikuwa moja tu: Kuingia ikulu ya Kinshasa kwa msaada wowote kutoka kwa yeyote; Mungu au shetani.

Ilikuwa baada ya makubaliano hayo, Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo mkuu wa sasa wa majeshi wa Rwanda, James Kabarebe.

Baada ya kuingia ikulu, Kabila anadaiwa kuwageuka wenzake. Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa jeuri, kuwa wageni wote waondoke nchini. Aliongeza kwa kufafanua, kwamba Wanyarwanda warudi kwao na kusema anawashukuru kwa kazi waliyofanya.

Kabila alikuwa tayari amesoma mwelekeo wa makubaliano yake na kuona kuwa yanatoa mwanya kwa kile kilichoitwa “Nchi ya Ahadi” ya Watutsi kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Somalia, Ethiopia, Eritrea na Tanzania.

Alitakiwa atangaze, akiwa rais, kuwa Kivu mbili zote ni makazi ya Watutsi; ili hata wananchi wa Kongo watakaobaki humo, wawe wanafahamu kwamba siyo kwao.

Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni “makubaliano ya porini” na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi. Alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo “lipelekwe kwa wananchi – kupitia bungeni – ili wananchi wenyewe waamue.”

Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri wake wa mambo ya nje aliyeitwa Bizima Karaha (Bizimana Karahamuheto).
Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema, “Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje alikuwa Mnyarwanda?”

Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na sasa mkuu wa majeshi ya Rwanda. Hatua hizi na nyingine, ndizo zilisababisha kutotekelezwa kwa Makubaliano ya Lemera.

Lakini wachunguzi na wafuatiliaji wa mahusiano ya nchi hizi mbili wanasema, makubaliano yameandikwa na yapo; hayajafutika. Kilichofanyika ni “ukaidi wa Kabila” wa kutotaka kutimiza ahadi yake baada ya kuingia ikulu.

Kabila anasemekana alikuwa amesoma kitabu cha Raphael Ntibazokiza kikieleza mahusiano ya Watutsi na wabantu, kiitwacho Plan de la colonisation tutsi au Kivu et region centrale de l’Afrique – Mpango wa ukoloni wa Kitusi katika Kivu na eneo la Afrika ya Kati.

Raphael anaandika, “Mhutu ameumbwa kufanyia kazi watu wengine; hawezi hata kujaribu kupata uongozi. Chukua nafasi zote za mikoa na wilaya na atakayekuwa mtawala ahakikishe kuwa analinda maslahi yetu... Baadaye watakapokuja kustuka, watakuwa wamechelewa…”

Mmoja wa waliokuwa karibu na Laurent Kabila amenukuliwa akisema hakuna kitu kilichomsononesha Kabila kama kauli ifuatayo ndani ya kitabu cha Raphael:
“Tutumie ukarimu wao. Tujinyenyekeze kwao kama sisi ni watumishi wao.

Tukiishachukua nafasi zao tuwatelekeze na ‘kuwalipa ujira wa nyani’- payez-les en monnaie de singe pour montrer leur incapacite – ili kudhihirisha kuwa hawana uwezo.”

Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na Rwanda. Aliuawa na mmoja wa “watoto” wake – vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni.

Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo chake. Kuna wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera; lakini wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi.

Kwa kuwa Jonas Savimbi aliuawa katika mwaka moja tu baada ya kifo cha Kabila, inadaiwa kulikuwa na mkono wa mataifa makubwa; hili likitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku likiwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi. Siasa hizi hazijafafanuliwa.

Kuingia kwa Joseph Kabila, anayedaiwa kuwa mtoto wa kufikia wa Laurent Kabila, kunaonekana kuleta mgeuko mwingine kuelekea kule ambako “baba” yake alikataa.
Kinachoitwa makubaliano kati ya serikali ya Rwanda na ile ya Kongo kinaonekana wazi kuwa utekelezaji wa mpango wa awali ambao Laurent Kabila alikataa.

Aidha, kukamatwa kwa Jenerali Laurent Nkundabatware na kuhifadhiwa nchini Rwanda kunaelezwa kuwa sura kamili ya “kuheshimu kazi ya maandalizi aliyokuwa akifanya nchini Kongo.”

Kuna madai kuwa Nkundabatware, Mnyarwanda kutoka Rwanda, lakini Rwanda inasema ni Mkongomani, hakuwa na jeshi lolote nchini Kongo. Aliongoza majeshi ya Rwanda hadi hapo ilipoonekana kuwa mazingira yamekuwa mazuri kwa Rwanda kuingilia kwa kisingizio cha “kufukuza Interhamwe na kuweka usalama mpakani.”

“Hata akipelekwa Kongo leo hii, Kabila atamlinda Jenerali Nkundabatware, labda kama wakuu wa Kongo na Rwanda watakuwa wamegundua kuwa amewasaliti,” kimeeleza chanzo cha habari hizi mjini Goma.

Rwanda imeingia Kongo. Nani ataiondoa? Baadhi ya nchi jirani zimekuwa watazamaji tu wakati nyingine zikiwa katika maandalizi ya kunufaika kutokana na mgogoro wa nchi hii.

Moses Byaruhanga, waziri katika ofisi ya rais (Siasa) nchini Uganda, amesema nchi yake inaunga mkono “shirikisho la Kivu na Kisangani” na kwamba wanasubiri kuona serikali ya Kinshasa inalionaje suala hilo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa za kukamilisha kumegwa kwa mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kutoka Jamhuri ya Kongo na kuzifanya muungano wa Jamhuri ya Kivu.

Kauli ya msemaji wa ikulu Uganda inaongeza uwezekano wa kuimega Kongo pale inapohusisha jimbo jingine la Kisangani ambako majeshi ya Uganda yanadai kuwinda waasi wa Lord’s Resistance Army (LRA).

Kiongozi wa LRA, Joseph Kony amekuwa akipambana na majeshi ya serikali ya Yoweri Museveni kwa zaidi ya miaka 15. Uganda sasa inadai kuwa Kongo inatumika kama kichaka cha waasi hao.

Kauli ya Uganda haipishani na mipango inayodaiwa kufanywa na Rwanda ingawa Rwanda, kupitia balozi wake mjini Dar es Salaam ilikaririwa ikisema haina mpango wowote wa kuigawa Kongo.

Jumuiya ya kimataifa imetekwa kwa propaganda za Interhamwe, Wanyamulenge, waasi wa LRA na kumbukumbu za mauaji ya kimbari.

Isipokuwa Barrack Obama ambaye angalau amesema anataka Kongo tulivu na kwamba atasaidia kuleta hilo, mataifa mengine, pamoja na Ufaransa, yanataka kuimega Kongo.


Nini tutarajie katika hiki kiitwacho makubaliano ya Jakaya na Lowasa?

Tanzania ni ya Watanzania, makupe wawili hawana kibali wala dhima yakuuziana nchi hii kama pipi, Lowasa na Jakaya iwe usiku ama mchana, kiangazi ama masika, kamwe hawataruhusiwa kuuziana hata kipande cha nusu futi cha ardhi ya Tanzania hii kwa minajiri ya kututawala, labda pale Musoga nyumbani kwao!

Ni laana kwa Watanzania kuruhusu ccn itawale hata kwa sekunde tu baada ya 25/10/2015.

Hata aje Mtume Mohamed au Yesu Kristu atake kugombea uongozi nchini Tanzania kupitia ccn, ilimradi iwe kupitia ccm basi hao HAWAFAI na ni Laaana kuu!.
 
Jk hawezi kuingia makubaliano na mtu fisad pengine umesahau atakuwa na makubaliano na mafisadi wenzake.
 
Asante Mkuu Yerico, uchambuzi mzuri wa kina lakini haya ya JK na EL kutokutana barabarani hayawezi kutufikisha huko. Na sidhani kama hii ni agenda ya ccm kama chama, vinginevyo tuwakatae ccm kwa ufisadi wao uliotufikisha hapa tulipo kama Taifa.
 
Asante Mkuu Yerico, uchambuzi mzuri wa kina lakini haya ya JK na EL kutokutana barabarani hayawezi kutufikisha huko. Na sidhani kama hii ni agenda ya ccm kama chama, vinginevyo tuwakatae ccm kwa ufisadi wao uliotufikisha hapa tulipo kama Taifa.

Asante sana mkuu, pamoja sana
 
Makubaliano ya wawili hawa ambayo ni yamdomo chini ya viapo (Gentlemen agreement) ni suala linalotazamwa na wahusika hawa kwa jicho kali sana, msingi wa aina hii ya makubaliano unasimama katika TAMAA.

Historia inatukumbusha kuwa aina hii ya makubaliano haijawahi kuwa na matokeo chanya tangu kuumbwa kwa ulimwengu, hii inamaana kuwa mkataba wa Jakaya na Lowasa ni taraji la mauaji mtawalia.

Nini tutarajie katika hiki kiitwacho makubaliano ya Jakaya na Lowasa?

Tanzania ni ya Watanzania, makupe wawili hawana kibali wala dhima yakuuziana nchi hii kama pipi, Lowasa na Jakaya iwe usiku ama mchana, kiangazi ama masika, kamwe hawataruhusiwa kuuziana hata kipande cha nusu futi cha ardhi ya Tanzania hii kwa minajiri ya kututawala, labda pale Musoga nyumbani kwao!

Ni laana kwa Watanzania kuruhusu ccn itawale hata kwa sekunde tu baada ya 25/10/2015.

Hata aje Mtume Mohamed au Yesu Kristu atake kugombea uongozi nchini Tanzania kupitia ccn, ilimradi iwe kupitia ccm basi hao HAWAFAI na ni Laaana kuu!.
Mkuu
Yeri Yeri, (sorry kutokutumia imposter title yako), kwanza asante kwa hadithi nzuri, japo ni cut and paste, ila umefanya kazi nzuri kuwaongezea Watanzania wengi ufahamu kwa vile sisi Watanzania wengi ni wavivu kusoma!.

Sorry to say hiyo ni simulizi imeandikwa na mtu timamu ambaye kichwa kimetulia! na sio wewe master spin doctor!.

Simulizi ya Mashariki ya Kati, umenyofoa kutoka Mgogoro wa Mashariki ya Kati - Maisha ni Vita - Blogger wakati simulizi ya Congo, umenyofoa kutoka hapa Mkataba wa kuuza Kongo huu | Gazeti la MwanaHalisi huu ni wizi wa mchana kweupe!, wizi ni wizi tuu, anayefanya wizi ni mwizi tuu, wizi wa literary work ukajifanya umeandika wewe unaitwa plagiarism, mwizi huyo anaitwa plagiarist!, japo ukiiba in good faith kwa ajili ya kuwasaidia wengine kuelimika ni wizi mzuri, ulipaswa utoa haki kwa just to mention the source!, yaani kutoa attribution, unless kama hizo kazi zote mbili, mwandishi wa kwenye original source ni wewe, then ungesema!, contrast kati ya vichwa vya ulichocopy na kichwa chako humu jf kinafahamika wazi!.


Tatizo dogo la maelezo yako yote hayo, ni kukosekana tuu kwa linkage kati ya masimulizi yako na the real case scanerio ya makubaliano ya JK na EL, kama uweza kutuwekea details za makubaliano mengine yote kwenye simulizi yako, umeshindwaje kupata hayo makubaliano ya JK na umeshindwa vipi ku link sumulizi zako na hali halisi ya JK na EL?!.

Ni ushauri tuu, next time akiamua kuwa spin doctor mzuri, don't just cut and paste, but also find the linkage itakayoweza ku link pande zote mbili ili kutengeneza a good spinning circle, ili hiyo spinning yako iwe round so that you can be abble to spin it round and round like a record ya santuri!.

Ni ushauri tuu, otherwise umenikumbusha enzi za Jason Borne!, the master copy cut wa jf!.

Pasco
 
Porojo porojo unashindwa kuitetea hoja yako unaleta mambo ya congo israel na misri.......Lowasa ndie pekee ukawa wanamu ogopa sana atawasambaratisha vibaya sana ...
Hoja yako umeiharibu kwa kuleta porojo na hadithi za paukwa pakawa
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom