Maktaba yangu ya nyumbani

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,646
Nimekulia katika mazingira ya uanazuoni.

Toka nimeanza kujitambua nilizungukwa na kila aina ya vitabu nyumbani.

Niseme tu kuwa nyumbani kulikuwa na maktaba ndogo.

Ukubwani napo nimejitahidi kwa kiasi chake nami kuwa na kiji maktaba changu cha uongo na kweli.

Sasa basi, hebu tutupie picha hapa za maktaba zetu za nyumbani.

Na si lazima hizo maktaba ziwe ni vitabu tu. Yaweza kuwa chochote kile kama wewe ni stripper tupia stripper outfits zako, stripper heels, nk.

Kama wewe ni mganga wa kienyeji/ mchawi kama Mshana Jr, tupia matunguri yako tuyaone.

Kama wewe ni mbeba maboksi kikweli kweli basi tupia hizo steel-toed boots zako na helmet tuzione.

Naanza kwa kuonyesha njia. Je, kwa kuangalia aina ya vitabu vilivyopo hapo kwa maktaba yangu, waweza kukisia fani yangu?

Here we go....

8AF2E87F-9F44-4E15-B913-074FE31C6061.jpeg
848950DB-0838-40B4-8DC5-48B60A8F92E7.jpeg
 
Heshima kwako Mkuu, kwa upande wangu sikubahatika sana kupata elimu katika mfumo wetu wa kawaida, mbaya zaidi kutokea mazingira ya kijijini ndani huko yalikua na kila sababu kudidimiza ndoto na matamanio yangu.

Lakini nashukuru Mungu niliitumia vizuri fursa ya kuwa mtoto wa Mwalimu. Nilisoma vitabu vingi sana, vikaniongezea upeo wa mambo mengi lakini kubwa zaidi lugha na misamiati ya kiingereza.

Huo ukawa ni utaratibu wangu wa maisha na sijawahi kujuta kamwe. Kabla hawajavunja Novel Idea pale Samora nilikua nanunua vitabu kila mwezi ikabidi wanipe uanachama na punguzo la asilimia kumi.

Niliwahi kusoma mahali jamaa akisema kuna vitu viwili kama sio vitatu vitakubadilisha, watu unaokutana nao na vitabu unavyosoma.

Nimeipenda Maktaba yako Kapteni.
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom