Maktaba ya mtandaoni TOVL yafanyiwa marekebisho makubwa ya muonekano na utendaji

RobyMi

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
848
862
Habari wana JF

Maktaba pekee ya mtandaoni Tanzania ( Tanzania Online Virtual Library ) imefanyiwa marekebisho makubwa ya muonekano, sikuwa nimepitia kwa kipindi cha zaid ya wiki moja sasa, ila leo nikahitaji kucheki kama jamaa wameongeza vitabu vingine, ndio nikakutana na ujumbe kuwa wanafanyia mfumo huu maktaba.

Introducing the New and Improved TOVL Look & Feel

Kiukweli nimependa muonekano mpya, nawapa hongera sana, wenzetu hawa wamejitahidi sana. Ni mda mrefu sana maktaba hii ilibaki kuwa stagnant bila ya madaliko yoyote, ila kwa mabadiliko haya, nafikiri tutarajie makubwa kutoka kwao.

Kwa sasa naona website ina muonekano mzuri sana especially kwa sisi tunaotumia simu na tablets. na pia wamejitahidi wameongeza vitabu vingi, kuna baadhi ya pages bado hazijakamilika ila naamini watazifanyia kazi. Nimependa zaid sasa unaweza hata kuacha comment kwenye kitabu.

Sasa unaweza kusoma vitabu kwa kulipia

Sasa kusoma kitabu ndan ya maktaba hii, utahitaji kulipia shilingi Tsh 500/- tu.

Tuwa support hawa wenzetu ili waweze kuleta positive impact na mfumo wao huu mzuri kwenye sekta yetu ya elimu
Unaweza kupitia mfumo wa mpya hapa

Say Hello to TOVL's brand new Look & Feel

Previous Post

TOVL - Maktaba ya mtandaoni inayohimiza matumizi ya kompyuta kwa watoto
 
Back
Top Bottom