Maktaba ya Kitaifa ya Kenya yaandaa shughuli za lugha ya Kichina

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
微信图片_20220412142852.jpg


微信图片_20220412142857.jpg


微信图片_20220412142901.jpg


"Ni maua ya kupendeza ya asumini, yanachanua na kutoa harufu nzuri na kuwavutia watu..."

Tarehe 8 Aprili katika Maktaba ya Kitaifa ya Kenya jijini Nairobi, mhitimu wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi alikuwa akifundisha jinsi ya kuimba wimbo wa Kichina "What a Beautiful Jasmine".

Hii ni moja ya shughuli za lugha ya Kichina iliyoandaliwa na Maktaba ya Kitaifa ya Kenya, na kuhudhuriwa na wafanyakazi kutoka Maktaba hiyo na Ubalozi wa China nchini Kenya, pamoja na walimu na wanafunzi kutoka Taasisi za Confucius katika vyuo vikuu vya Nairobi na Kenyatta, na wakazi wa huko.

Bango lenye maneno "Jifunze Kichina, pata marafiki duniani kote" liliwekwa kwenye eneo la shughuli hiyo. Charles Nzivo, naibu mkurugenzi wa Maktaba ya Kitaifa ya Kenya, alisema hafla hiyo ilifanyika katika muktadha wa kushamiri kwa mawasiliano ya kitamaduni kati ya watu wa Kenya na China, na kwamba kukuza lugha ya Kichina na utamaduni wa China ni muhimu katika kuhimiza ushirikiano wa pande hizo mbili katika maeneo muhimu kama vile biashara na miundombinu.

Hilda Mwanji anayejishughulisha na utalii alisema: “Watu wa nchi hizi mbili wanapokutana katika shughuli kama hii, maelewano ya kitamaduni yataongezeka na uhusiano utaimarika.” Pia alisema atajifunza kuimba nyimbo nyingine za kichina. .

Wanafunzi kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Kenyatta walisoma shairi liitwalo " Thoughts On a Quiet Night" na maonyesho ya Wushu, ambapo video fupi inayotambulisha Opera ya Beijing ilionyeshwa kwenye skrini, huku shughuli za kuandika Kichina na uchoraji vinyago vya Opera ya Beijing pia zikiwavutia washiriki.

Maandiko ya Kichina si jambo geni kwa mwalimu wa Kichina Justus Kamamo, lakini ilikuwa ni mara ya kwanza kuchora vinyago vya Opera ya Beijing kwa mikono, na alivutiwa sana. "Hii ni shughuli nzuri sana, na nimetangamana na watu wengi kupitia utamaduni wa Kichina" alisema.

Habari zinasema Maktaba ya Kitaifa ya Kenya ilijiunga na Muungano wa Maktaba Duniani wa Njia ya Hariri ulioanzishwa na China mnamo 2021. Pande hizo mbili zitatumia vitabu kama chombo kutekeleza shughuli mbalimbali za kitamaduni ili kuimarisha kiwango cha ushirikiano wa kitamaduni kati ya China na Kenya.
 
Safi sana, acha wale ambao wana nia ya kweli wajifunze lugha za aina hii. Ambazo bila shaka zitakuwa za faida kubwa sana kwao. Mimi mwenyewe najuta sana kwamba nilipokuwa chuoni hapo UON sikuchangamkia hiyo fursa. Kujifunza lugha ya Mandarin ni course work ya bure bila malipo kwenye taasisi hiyo ya Confucius, Main Campus.
Niliingia darasani mara kadhaa, baada ya kujisajili, ila sikuweza kuendelea. Kisa presha za course ambayo nilikuwa naisomea, pamoja na biashara ambayo nilikuwa naifanya part-time.
 
Ndio mojawapo wa chachu ya maendeleo yetu, ujanja wa kujifunza lugha nyingi, sio unaganda kwenye moja........
 
Back
Top Bottom