Makosa yanayojirudia ya Baba wa Taifa na historia ya TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,253
Ndugu zangu,

Dudu kaandika hayo hapo chini na mimi nimeona nifungue uzi mpya niweke maelezo katika hayo maneno yake ili kusahihisha makosa ya historia ya TANU ambayo yamekuwa yakijirudia sasa nusu karne:

MAKOSA YANAYOJIRUDIA KATIKA HISTORIA YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NA TANU

Dudus said:

''... watu wa pwani walikuwa na advantage ya Kiswahili kwa wakati huo kiliwabeba sana. Ningeletwa mimi mhadzabe na Kiswahili wapi na wapi! Inasemekana hata Nyerere wakati anafanya urafiki na wazee wa Kariakoo hadi wakamkabidhi TANU, Kiswahili kilikuwa kinampa shida to some extent; ila kimalkia ungedhani anaishi kwenye corridor za Buckingham.''

Jibu langu kwake hili hapo chini:

Dudus,
Mwalimu Nyerere hakupokelewa Dar es Salaam na mzee yeyote alipofika mwaka wa 1952.
Hii ni katika moja ya makosa yaliyomo katika historia ya TANU.

Nyerere mtu aliyekuwa anajuananae kwa karibu sana alipofika Dar es Salaam ni Joseph Kasella Bantu.

Kasella Bantu akiishi Temeke.

Ilikuwa wakati mwingine Mwalimu akija mjini basi atalala kwa Kasella Bantu siku ya pili atarejea Pugu.

Kasella Bantu ndiye aliyempeleka Nyerere kwa Abdul Sykes.
Abdul Sykes alikuwa ndiye Secretary na Act. President wa TAA.

Hicho chama cha TAA kimetokana na African Association chama ambacho baba yake Abdul, Kleist Sykes alikuwa katibu muasisi mwaka wa 1929.

Hakuna mzee yeyote aliyempokea Nyerere alipofika Dar es Salaam kutafuta viongozi wa TAA wala hakuna mzee yeyote aliyemkabidhi Mwalimu chama cha TANU.

Wala Mwalimu hakupata kujulikana hadi pale alipokuja kusuhubiana na Abdul Sykes katika siasa za TAA kuelekea kuundwa kwa TANU.

Hii ilikuwa kati ya mwaka wa 1952 - 1954.

Katika historia ya TANU kutokea TAA wazee waliokuwa ndani ya uongozi wa TAA na wao kushiriki katika kuweka msingi wa kuunda TANU walikuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Said Chaurembo aliyekuwa Liwali Mahakama ya Kariakoo.

Hawa walikuwa wajumbe katika TAA Political Subcommittee ilyoundwa mwaka wa 1950.

Wajumbe wa TAA Political Subcommttee walikuwa Dr. Vedast Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Sheik Hassan bin Ameir, John Rupia na Sheikh Said Chaurembo.

Wala si sawa kusema kuwa Nyerere aliunda TANU.

Historia ya TANU inaanza mbali sana kwa karibu ni mwaka wa 1945 Abdul Sykes, Ally Sykes na askari wenzao katika 6th Batallion KAR Burma Infantry wakiwa Kalieni Camp Bombay hapo ndipo katika mkesha wa Christmas, 1945 walipoamua kuunda TANU kudai uhuru wa Tanganyika na jina hili lilitolewa huko.

Hapo Kalieni Camp askari Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki walikuwa wanasubiri kurudishwa makwao baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945).

Urafiki wa Nyerere na wazee wa Dar es Salaam ulianza baada ya TANU kuundwa 1954 na mzee aliyekuwa karibu sana na Mwalimu alikuwa Mzee Mshume Kiyate mwaka wa 1955.

Ukipenda unaweza ukawaongeza na wengine kama Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi na Max Mbwana.

Historia hii nimeiandika kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Kulia ni Mzee Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Mzee Max Mbwana na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi.

Inasikitisha kuwa baada ya uhuru miaka 60 hadi leo hatuijui historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere wala historia ya TANU.

May be an image of one or more people and people standing
Kulia ni Mzee Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Mzee Max Mbwana na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi Uchaguzi wa 1962.
 
Nyerere alikuwa na kadi namber1 ya TANU kado namba 2 na namba 3 za akina sykes,kumtenganisha nyerere na TANU ???
 
Nyerere alikuwa na kadi namber1 ya TANU kado namba 2 na namba 3 za akina sykes,kumtenganisha nyerere na TANU ???
Bado kichwa kigumu Sana mwanalumba swala lakadi yachama kua namba 1 na uazishwaji wa TANU nimambo mawili tofauti
mfano mdogo uchukue ,akati ACT _wazalendo inaazishwa kadi namba moja alipewa zito kabwe ,kuazia siku maalim seif alivojiunga na AcT kilakitu kilibadirika hivyo akapewa kadi nambamoja
 
Achana na zitto msanii,wale wazee wa Tanu wasingempa nyerere ile kadi kama wangekuwa haeatambui mchango wake katika kuunda chama
 
kwa hiyo TANU ilianzishwa Ulaya na Abdul Sykess... Mwamedi bana
Laki...
Fikra ya kuunda TANU ilipata nguvu sana wakati wako Burma wanapigana kwenye vita ambavyo Waafrika havikuwa vinawahusu.

Walipokuwa Kaleini Camp Bombay, sasa Mumbai ndipo walipokuwa wanaagana askari kutoka Afrika wakaambiana kuwa azima wakifika makwao waunde vyama vya ukombozi kupambana na ukoloni.

Askari wa Tanganyika wakiiongozwa na Abdul Sykes ndipo walipoamua kuunda TANU.
Si lazima uniamini.

Unaweza ukabakia na historia ya Kimambo na Temu (1969).
Unaweza pia ukabakia na historia y Chuo Cha CCM Kivukoni (1981).

Mimi hueleza kile nikijuacho ukipinga wala sigombani na wewe.
 
Achana na zitto msanii,wale wazee wa Tanu wasingempa nyerere ile kadi kama wangekuwa haeatambui mchango wake katika kuunda chama
Mdukuzi,
Mchango wa Julius Nyerere katika TANU ulikuwa mkubwa sana.
Lakini hakuweza kufanya yale yote peke yake.

Nyuma yake alikuwa na watu hodari sana.

Hao si wale waliokuwa Dar es Salaam pale New Street kama Iddi Faiz Mafungo na ndugu yake Iddi Tosiri, Mshume Kiyare wengi, wengi, wengi sana.

Kulikuwa na watu majimboni ambao walijitoea sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kilwa kulikuwa na watu kama Abdulkarim Hajj Musa Jemadari, Mikidani walikuwapo akina Msham Awadh, Kamachumu walikuwapowatu kama Ali Migeyo , Tabora akina Bilal Rehani Waikela, Dodoma walikuwapo akina Haruna Taratibu wengi tu wazalendo waliounga mkono TANU.

Bahati mbaya sana kuwa historia za wazalendo hawa hazifahamiki.
 
Bado kichwa kigumu Sana mwanalumba swala lakadi yachama kua namba 1 na uazishwaji wa TANU nimambo mawili tofauti
mfano mdogo uchukue ,akati ACT _wazalendo inaazishwa kadi namba moja alipewa zito kabwe ,kuazia siku maalim seif alivojiunga na AcT kilakitu kilibadirika hivyo akapewa kadi nambamoja
KIna...
Kadi 1000 za kwanza alinunua Ally Sykes kutoka mfukoni kwake na yeye ndiye alisanifu hizo kadi na zikachapwa na Printpak wachapaji wa Tanganyika Standard.

Kadi no. 1 Ally Sykes alimwandikia TANU Territorial President Julius Nyerere.

Baada ya hapo Ally Sykes kwa ile akili yake ya biashara iliyomtajirisha kufru akapiga mnada wa kadi yeye akaweka dau zito.

Hakuna aliyeweza kufikia.
Ally akachukua kadi no. 2 na kaka yake akachukua kadi no. 3 kampita hata ''The Bank'' Dossa Aziz.

Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa.
 
Mzee kilizi..mdini sana..hua akiona Nyerere akifundishwa katika historia ya nchi roho ina muuma sana..alitamani babu zake akina dully sakys..ndio wawe baba wa taifa.

All in all historia itamkumbuka nyerere siku zote za uhai wa dunia hii..alifanya makubwa sana..

Hope bado unahujumiwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Jiwe...
Hapana kama mimi ingegundulika kuwa nia ya kuandika kitabu cha Abdul Sykes ni kumdogosha Mwalimu Nyerere watu wangenipuuza na ningekiua kitabu changu.

Kitabu kinakwenda toleo la tano kuanzia 1998 kwa kuwa wasomaji wamekipenda sana.

Nyerere hataweza kusahaulika kwa kazi kubwa aliyofanya.

Lakini sasa baada ya mimi kuandika historia hii tunayojadili hapa watu wametambua mchango wa wazalendo wengine.

Watu wametambua kuwa historia ya Kimambo na Temu na nyinginezo zina upungufu mkubwa sana.

Ndiyo maana nimealikwa vyuoni Ulaya na Marekani, nimehojiwa na vyombo vingi vya habari ndani na nje.

Kwani wewe uliijua historia hii kabla hujaisikia kutoka kwangu?

Unaeumwa na moyo ni wewe unaekuja hapa kunitukana na kufanya "name calling," jambo ambalo kanuni za JF zinakataza.

Unaeumwa na roho ni wewe unakuja kwangu bila adabu na kujaribu kunifedhehesha.

Juu ya hayo ningeweza nikakataa kujadiliana nawe lakini mimi nasikia raha kuhadithia historia ya wazee wangu jinsi walivyounda TANU na kupigania uhuru wa nchi yetu.
 
Mdukuzi,
Mchango wa Julius Nyerere katika TANU ulikuwa mkubwa sana.
Lakini hakuweza kufanya yale yote peke yake.

Nyuma yake alikuwa na watu hodari sana.

Hao si wale waliokuwa Dar es Salaam pale New Street kama Iddi Faiz Mafungo na ndugu yake Iddi Tosiri, Mshume Kiyare wengi, wengi, wengi sana.

Kulikuwa na watu majimboni ambao walijitoea sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kilwa kulikuwa na watu kama Abdulkarim Hajj Musa Jemadari, Mikidani walikuwapo akina Msham Awadh, Kamachumu walikuwapowatu kama Ali Migeyo , Tabora akina Bilal Rehani Waikela, Dodoma walikuwapo akina Haruna Taratibu wengi tu wazalendo waliounga mkono TANU.

Bahati mbaya sana kuwa historia za wazalendo hawa hazifahamiki.
Hakuna aliyesema alifanya mwenyewe ila alikuwa akili nyingi na kiongozi shupavu mwenye mikakati ndio maana hao wazee wakamuamini,Tanu inazaliwa ubavuni mwa TAA na Nyerere akiwa Rais Wa TAA hakuwa mtu mdogo.leo useme eti bibi Titi slikuwa hamjui Nyerere mpaka Tanu inaanzishwa,???itakuwa ni ujinga wake kutomjua
 
Mimi si mtu wa kubishana na ndiyo kisa nikaandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Siwezi kujiingiza katika propaganda kwani kitabu kipo kina kurasa 416.

Nimeeleza mengi ndani ya kitabu hiki.

Mimi nimetosheka na kuridhika kwa kueleza historia ambayo kabla hakuna aliyeijua.

Kuna mtu alichukuliwa sana na mkutano wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta Nairobi 1950 akaniuliza mbona mambo haya makubwa hayamo katika historia ya TANU na historia ya Nyerere kuwa alikuwa na watu waliofika mbali katika kudai uhuru?

Jibu langu lilikuwa yawezekana hawakuwa wanaijua historia hiyo.

Swali lililofuatia likawa vipi kuhusu uhusiano wa Ally Sykes na Kenneth Kaunda 1953?

Jibu langu sikubadili nikasema hawakuwa wanajua historia hii pia.

Akaniuliza tena nini sasa wanajua katika historia ya TANU?

Nikajibu, "Wanajua kuwa Nyerere ndiye aliyeunda chama cha TANU, "from nothing."

Ukumbi mzima ukacheka.
Hadi leo sijajua nini kiliwachekesha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom