Makosa yanayogharimu ujenzi: Nyumba nzuri inayodumu ni ujenzi mzuri

mwakavuta

Member
Sep 22, 2020
99
302
Wakuu salam,

Naomba niweke wazi kuwa kwenye fani ya ujenzi mimi ni kibarua mzoefu kwa muda mrefu nimefanya kazi nyingi na mafundi wengi nimeona mengi. Kwenye hii mada nitatoa uzoefu wangu kuna mtu utamfaa. Twende kwenye mada.

Ujenzi mzuri kwa ajili ya nyumba imara inayovutia unahitaji gharama kubwa za vifaa ufundi mzuri kitu ambacho kwa watu wanakikwepa.

Kuna makosa yanafanyika wakati wa ujenzi wa msingi na ukuta ambayo yanaleta muonekano mbaya baada ya finishing kama hayatagundulika mapema yakatatuliwa. Makosa hayo ni kama,
  • kuta kupindishwa wakati wa ujenzi. Kama kuta ni dhaifu usitindue matumbo kubali kuingia gharama ya sement na mchanga kujaza kuta zinyooke. Kama utatindua tumia wire mesh.
  • kuta na nguzo kujengwa dhaifu sana na kubebeshwa mzigo mzito juu hivyo kusababisha nyufa au kupinda. Hii inaweza kuchangiwa na ubora wa materials au vipimo wakati mwingine ufundi. Njia rahisi ya kuimarisha kuta na msingi ni kuweka wire mesh ndipo upige plasta pia plasta iwe na resho nzuri.

  • Nyumba kukosa sguire (nyuzi tisini) kwenye kona za kuta. Hii husababisa kuwa na muonekano mbaya hasa baada ya kuweka tiles kama wakati wa plasta haitagundulika na kutatuliwa.
  • Kutumia matofali yenye vipimo tofauti husababisha muonekano tofauti baada ya plasta kama hutakubali gharama zaidi ya vifaa na ufundi. Mfano kujengea tofali za inchi 6 chini kisha inchi tano kwenye over-lenta. Kama hutaki kuingia gharama za kujaza ukuta, ukuta wa ndani utakua mwembamba kidogo baada ya lenta. Inategemea maarifa ya fundi.
  • Sakafu kuwa na nyufa, hii inatokana na material uliyotumia kujaza msingi na ufundi wa sakafu yenyewe. Kama umetumia udongo(kifusi) ni vyema kushindilia vizuri, njia rahisi ya kushindilia ni kujaza maji baada ya kifusi mpaka kiwe tope kisha kushindilia ingawa inachukua muda kidogo, kifusi kikikauka kitatia chini rudia zoezi mpaka uridhike.
Kama umetumia mawe na kifusi maji ni muhimu ili ujaze nafasi zilizoachwa wazi kwenye mawe. Baada ya kujaza kifusi ni vyema kupanga mawe Ndio umwage zege. Ni vizuri kujaza zege isiyopungua inchi nne baada ya mawe.

Nyumba kutonyooshwa vizuri wakati wa plasta hasa kwenye kona, milango na madirisha ( coplo). Kwa uzoefu wangu ni mafundi wachache wanaoweza kunyoosha, kubali kuingia gharama upate fundi mzuri. Kama unajiweza ni vizuri kunyoosha madirisha na milango ndipo uweke madirisha na milango.
  • Rangi au skim kubanduka, hii inatokana na aina ya plasta iliyopigwa. Kama fundi amepiga pasi skim haitashika kwa muda mrefu.
  • Msingi kutokuwa na uimara wa kutosha kama jengo ni kubwa. Hii itasababisha nyufa kwenye nyumba ikitokea mtikisiko kidogo. Ni vyema kuchimba msingi mrefu kisha suka hata mondo tatu juu ya msingi mimina zege isiyopungua inchi Sita. Kama unajiweza mwaga zege ya sakafu kwa nyumba yote kabla ya kujenga kuta.
Usiwe na haraka ya kujenga kuta Mara baada ya kujenga msingi. Jaza msingi wako kaa angalau wiki mbili au tatu itakuolea gharama ya kuziba nyufa.

Kwenye ujenzi ni muhimu kugharamika upate kazi nzuri inayodumu na kuvutia. Kama unataka kazi nzuri kuwa makini kwenye.
  • mchanga unatumika kwenye plasta uwe laini, usiwe na mawemawe.
  • ratio ya plasta yako iwe nzuri mchanga usizidi sement. Kama unajiweza tumia ndoo nane za mchanga kwa mfuko isidi.

* Kubali kuingia gharama kumlipa fundi mzuri atakayekufanyia kazi nzuri. Mafundi wazuri wana gharama na ni wachache.
Kama unashindwa kupata mainjinia kwenye ujenzi wako, jitahidi upate fundi mzuri mwenye uzoefu.

Kama nyumba yako ina nyufa usizibe kihuni ingia gharama kujua chanzo cha huo UFA, kisha tindua plasta upana wa kutosha usio pungua inchi saba kisha tumia nondo au wire meshi na plasta yenye ratio nzuri.

Kama unaanza kujenga tafuta fundi mzuri anayejua kusoma ramani na kuiseti, sio kila fundi anajua kusoma ramani wengi wanakosea vipimo na kusahau baadhi ya vitu.

Mwisho kama unataka kazi nzuri kwenye plasta yako na fundi hana vifaa hivi gairi,
  • Timanzi (kobiro\ birigi)
  • Pipe level.
  • Square
  • Rati nzuri ya aluminum(trangel kwa lugha ya mtaani) isiwe ya mbao wala chuma huweza kupinda zikaharibu plasta.
  • Kamba na tape.

Nakutakia kila la heri kwenye kujenga makazi ya ndoto zako.
 
Yaani uliyaandika hapa yalinikuta mimi, kwanza fundi alienda foundation haikuwa level, pili wakati anasimamisha kuta, hakufuata square na baadhi ya kuta zikapinda, then Jamaa waliokuwa wananiuzia tofali sijui aliishiwa nikaagiza tofali wakaleta zianavipimo tofauti. Ilini cost sana.
 
Pole sana mkuu unaweza kurekebisha wakati wa plasta kupata square ya nyumba ndani na nje ila itakugharimu sana kwenye siment
Yaani uliyaandika hapa yalinikuta mimi, kwanza fundi alienda foundation haikuwa level, pili wakati anasimamisha kuta, hakufuata square na baadhi ya kuta zikapinda, then Jamaa waliokuwa wananiuzia tofali sijui aliishiwa nikaagiza tofali wakaleta zianavipimo tofauti. Ilini cost sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom