Makosa yanayofanya watu kuozea jela ndiyo yaliyoachwa katika mabadiliko ya Sheria

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
MAKOSA YANAYOFANYA WATU KUOZEA JELA NDIYO YALIYOACHWA KATIKA MABADILIKO YA SHERIA

Na Bashir Yakub. WAKILI
+255 714 047 241

Makosa ya Uhujumu uchumi, Utakatishaji fedha, Ugaidi, Mauaji, ikiwa ni pamoja na makosa ya Kubaka, wizi wa kutumia silaha, kumiliki silaha kinyume cha sheria, kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, makosa ya kujeruhi sana, kosa la kuhatarisha usalama wa taifa , usafirishaji dawa za kulevya hajaguswa na mswada wa mabadiliko ya Sheria.

Kwa taarifa tu haya ndiyo makosa yaliyowaweka, na ambayo yanaendelea kuwaweka ndani maelfu kwa mamia ya Watanzania.

Makosa haya kuachwa katika mabadiliko ya Sheria maana yake ni kuwa, ukikamatwa kwa kosa kati ya hayo ni ruhusa Mwendesha mashtaka wa serikali au yeyote mwenye dhamana ya kushitaka kupeleka kesi mahakanani bila upelelezi kukamilika.

Maana yake ni kuwa, ukikamatwa kwa kosa kati ya hayo ni ruhusa kuendelea kukaa ndani muda wooote hata miaka 20 mpaka upelelezi ukamilike.

Maana yake ni kuwa , ukikamatwa kwa kosa kati ya hayo aliyekutuhumu, akakukamata, akakushitaki ndiye huyohuyo anayeamua ushitakiwe lini, kesi yako ianze kusikilizwa lini, na iishe lini.

Kwa faida ya kumbukumbu tu ni kuwa kuna Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Na. 7/2021 ambao sasa unalazimisha Waendesha Mashitaka kutopeleka kesi Mahakamani mpaka upelelezi ukamilike ili kuondoa ile danadana ya kuahirisha kesi kila siku kwa kigezo cha upelelezi kutokamilika.

Hata hivyo mabadiliko hayo yameruhusiwa kwa makosa yote isipokuwa haya niliyotaja hapa.

Maoni haya yawafikie Wabunge kuwa ni makosa makubwa ya kiufundi na kimantiki kuyaacha makosa haya niliyotaja humu bila udhibiti na usimamizi.

Makosa haya kwa asilimia kubwa hasa ya Uhujumu Uchumi, Utakatishaji, na Ugaidi ndiyo yaliyoleta hamasa ya Mabadiliko haya hasa ilipozingatiwa historia ya miaka 5 iliyopita.

Sasa iweje Mabadiliko yaje halafu tena yaachwe. Mabadiliko yanabaki na maana ipi. Tunamchezea nani shele.

Kwakuwa haya ni makosa makubwa na pengine hii ndio hofu yenu basi tunaweza kufanya hivi;

Mtu akikamatwa kwa kosa kati ya haya na kwakuwa makosa haya mengi hayana dhamana basi akae ndani upelelezi ukiendelea kwa siku 90(Miezi 3) au hata 180(Miezi 6).

Kama upelelezi utaendelea kutokamilika kwa kipindi hicho basi huyu mtu asifutiwe kesi, bali apewe tu haki ya dhamana na kesi yake sasa iendelee akiwa nje. Ile Kauli yenu nzuri ya upelelezi haujakamilika iendelee katika makosa haya huku akiwa nje. Tuanze na hili linawezekana.

Hii haitasaidia tu Watuhumiwa na familia zao bali pia itawajibisha wapelelezi. Wataacha kusema tu upelelezi haujakamilika huku hajui hata jalada lilipo.

Kwani ni siri tena kwamba upelelezi huwa haukamiliki kwasababu wapelelezi huwa hawafanyi kazi yao zaidi ya kuiambia mahakama kuwa upelelezi haujakamilika na kusubir tarehe nyingine ili waseme hivyo hivyo tena? Nani asiyejua.

Sasa hii itawawajibisha hata kwa kiasi fulani. Atajua ana siku 90 au 180 tu za kupeleleza. Hatuwezi kuiacha hatima ya haya makosa yanayotuumiza hivi mikononi mwa Wapelelezi bila udhibiti na mwongozo wa sheria.

Kuna hii sababu maarufu kuwa mtuhumiwa akiachiwa ataharibu upelelezi. Ni uongo. Kwani hayo makosa yenye dhamana mtuhumiwa akiachiwa hawezi haribu upelelezi.

Hata hiyo iwe sababu ya msingi, bado ndani ya hizo siku 90 ama 180 ambazo mtu atakuwa ndani mpelelezi atumie mwanya huo kuhakikisha mtu akitoka nje hawezi haribu upelelezi.

Mpelelezi ambaye hawezi kufanya hili ndani ya siku 90 au 180 ambazo mtuhumiwa yuko ndani hawezi kuendelea na sifa ya kuitwa mpelelezi.

Maoni haya yawafikie Wabunge Watufanyie hili. Wasitusaidie bali walifanye hili kwani ni Wajibu wao.

Tusicheze na maisha ya watu, tusicheze na familia za watu, maisha hayana rufaa ukiishi hapa ndo umemaliza, ndo imetoka hiyo.

Tuliweke sawa hili kwani kila mtu ni mtahiniwa katika hili. Hakuna aliyesalama nyie nyote mnajua historia iliyopita itakuwa imekufunzeni.
 
Haya makosa yalipaswa yawe na preliminary hearing ili mahakama iamue kama unaruhusiwa kwenda uraiani ukisubiri investigators wanalize upelelezi au ubakie kifungoni kulingana na "gravity" ya makosa mtuhumiwa anayotuhumiwa. Common sense.

Mfano, mimi X, natuhumiwa kuwa ni mhujumu uchumi na DPP na nimeshakamatwa. Hapa, ninatakiwa niiombe mahakama inisikilize "preliminary hearing" kabla ya kesi. Inipime kwa vigezo vyao. Kisha inione kama naweza kukaa nje kwa masharti, huku mahakama ikiwapa muda maalum wa kumaliza upelelezi. Common sense.

Endapo makosa yangu ni makubwa mno, na yanaweza kuhatarisha usalama wa binadamu wengine au mwenendo wa kesi au matokeo ya upelelezi, basi mahakama iamuru nishikiliwe mpaka upelelezi ukamilike. Hii ni common sense.

Ninaamini kwa kufanya hivi, tutapunguza abuses zinazoendelea nchini za watawala kujifanya wao wanaimiliki sheria na wanaweza kuichezea wanavyotaka dhidi ya wapinzani wao wa kisiasa au kwa maadui wengine wanaokutana nao kwenye harakati za kutafuta maisha. Common sense.

Binafsi bado sijui kwanini akili za waafrika wenzangu zina udhaifu wa kufikiri kiasi hiki. Watu walioaminiwa na binadamu milion 60, lakini bado wanashindwa kung'amua mambo madogo madogo na ya kawaida kabisa!

kisha tunapata ujasiri wa kuwaahidi hawa kondoo wa Mungu kuwa tutaweza kuleta maendeleo? Ni maajabu makubwa sana.

GOD HAVE MERCY ON THE FOOLS OF AFRICA.
 
Wanawatungia Chadema. Wakamwulize sabaya.
 
Wanataka kumtungia Lissu akirudi. Ndio manaa unaona wanakimbizana haraka haraka ili wamtungie moja wapo akaozer jela bila ushajidi wala mashtaka.
 
Wabaya wakitaka wakupoteze watakusukumia kwenye makosa haya.

Haya makosa yanawakuta wengi. Kuna haja kuangalia hapa pia.
Wao hapo walipo kwa akili zao wanadhani wanawatungia wapinzani tu. Hayo makosa ya kisheria wanayajua lakini ni mkakati maalum wa kudhibiti watu wanaotishia kutwaa madaraka yao.
 
Na hao wanaofanya ufisadi kwenye miradi ya serikali Ndiyo inaangukia kwenye makosa ya uhujumu uchumi ?
 
MAKOSA YANAYOFANYA WATU KUOZEA JELA NDIYO YALIYOACHWA KATIKA MABADILIKO YA SHERIA

Na Bashir Yakub. WAKILI
+255 714 047 241

Makosa ya Uhujumu uchumi, Utakatishaji fedha, Ugaidi, Mauaji, ikiwa ni pamoja na makosa ya Kubaka, wizi wa kutumia silaha, kumiliki silaha kinyume cha sheria, kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria, makosa ya kujeruhi sana, kosa la kuhatarisha usalama wa taifa , usafirishaji dawa za kulevya hajaguswa na mswada wa mabadiliko ya Sheria.

Kwa taarifa tu haya ndiyo makosa yaliyowaweka, na ambayo yanaendelea kuwaweka ndani maelfu kwa mamia ya Watanzania.

Makosa haya kuachwa katika mabadiliko ya Sheria maana yake ni kuwa, ukikamatwa kwa kosa kati ya hayo ni ruhusa Mwendesha mashtaka wa serikali au yeyote mwenye dhamana ya kushitaka kupeleka kesi mahakanani bila upelelezi kukamilika.

Maana yake ni kuwa, ukikamatwa kwa kosa kati ya hayo ni ruhusa kuendelea kukaa ndani muda wooote hata miaka 20 mpaka upelelezi ukamilike.

Maana yake ni kuwa , ukikamatwa kwa kosa kati ya hayo aliyekutuhumu, akakukamata, akakushitaki ndiye huyohuyo anayeamua ushitakiwe lini, kesi yako ianze kusikilizwa lini, na iishe lini.

Kwa faida ya kumbukumbu tu ni kuwa kuna Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Na. 7/2021 ambao sasa unalazimisha Waendesha Mashitaka kutopeleka kesi Mahakamani mpaka upelelezi ukamilike ili kuondoa ile danadana ya kuahirisha kesi kila siku kwa kigezo cha upelelezi kutokamilika.

Hata hivyo mabadiliko hayo yameruhusiwa kwa makosa yote isipokuwa haya niliyotaja hapa.

Maoni haya yawafikie Wabunge kuwa ni makosa makubwa ya kiufundi na kimantiki kuyaacha makosa haya niliyotaja humu bila udhibiti na usimamizi.

Makosa haya kwa asilimia kubwa hasa ya Uhujumu Uchumi, Utakatishaji, na Ugaidi ndiyo yaliyoleta hamasa ya Mabadiliko haya hasa ilipozingatiwa historia ya miaka 5 iliyopita.

Sasa iweje Mabadiliko yaje halafu tena yaachwe. Mabadiliko yanabaki na maana ipi. Tunamchezea nani shele.

Kwakuwa haya ni makosa makubwa na pengine hii ndio hofu yenu basi tunaweza kufanya hivi;

Mtu akikamatwa kwa kosa kati ya haya na kwakuwa makosa haya mengi hayana dhamana basi akae ndani upelelezi ukiendelea kwa siku 90(Miezi 3) au hata 180(Miezi 6).

Kama upelelezi utaendelea kutokamilika kwa kipindi hicho basi huyu mtu asifutiwe kesi, bali apewe tu haki ya dhamana na kesi yake sasa iendelee akiwa nje. Ile Kauli yenu nzuri ya upelelezi haujakamilika iendelee katika makosa haya huku akiwa nje. Tuanze na hili linawezekana.

Hii haitasaidia tu Watuhumiwa na familia zao bali pia itawajibisha wapelelezi. Wataacha kusema tu upelelezi haujakamilika huku hajui hata jalada lilipo.

Kwani ni siri tena kwamba upelelezi huwa haukamiliki kwasababu wapelelezi huwa hawafanyi kazi yao zaidi ya kuiambia mahakama kuwa upelelezi haujakamilika na kusubir tarehe nyingine ili waseme hivyo hivyo tena? Nani asiyejua.

Sasa hii itawawajibisha hata kwa kiasi fulani. Atajua ana siku 90 au 180 tu za kupeleleza. Hatuwezi kuiacha hatima ya haya makosa yanayotuumiza hivi mikononi mwa Wapelelezi bila udhibiti na mwongozo wa sheria.

Kuna hii sababu maarufu kuwa mtuhumiwa akiachiwa ataharibu upelelezi. Ni uongo. Kwani hayo makosa yenye dhamana mtuhumiwa akiachiwa hawezi haribu upelelezi.

Hata hiyo iwe sababu ya msingi, bado ndani ya hizo siku 90 ama 180 ambazo mtu atakuwa ndani mpelelezi atumie mwanya huo kuhakikisha mtu akitoka nje hawezi haribu upelelezi.

Mpelelezi ambaye hawezi kufanya hili ndani ya siku 90 au 180 ambazo mtuhumiwa yuko ndani hawezi kuendelea na sifa ya kuitwa mpelelezi.

Maoni haya yawafikie Wabunge Watufanyie hili. Wasitusaidie bali walifanye hili kwani ni Wajibu wao.

Tusicheze na maisha ya watu, tusicheze na familia za watu, maisha hayana rufaa ukiishi hapa ndo umemaliza, ndo imetoka hiyo.

Tuliweke sawa hili kwani kila mtu ni mtahiniwa katika hili. Hakuna aliyesalama nyie nyote mnajua historia iliyopita itakuwa imekufunzeni.
kwaiyo na hii sheria mpya kuwa mtuhumiwa akiachiwa na hakimu kwa sijui mnaita kifungu Cha 225) kwamba haruhusiwi kukamatwa tena! Pia haiwahusu hao wenye economic case au money laundering ,nk?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom