Makosa yanatokana na kitabu kimoja

View attachment 1143324
Shikamoo wakuu. ningetaka kuwauliza kuwa "wamekuwa kuona sisi" ni sawa au la? lakini kwa kawaida tuseme "wamekuwa kutuona".
View attachment 1143325

zaidi ya hayo, "yako majirani karibu zaidi" ni sawa au siyo sawa? majirani ni mojawapo kati ya aina za watu, lazima tutumie "wako majirani karibu zaidi", je ni kweli?
asante sana
Ndugu Bakari China nikupe faida ya maneno hapo kidogo.

neno "WAMEKUWA" linatumika kuonesha viumbe hai kutoka hali fulani na kuwa katika hali fulani
hiyo herufi ya kwanza ambayo ni "W" inajulisha uwingi wa hao unaowazungumzia,yaani wakiwa kuanzia wawili ndo unatumia "WA"

Mfano : watu wamekuwa weusi.
Mbwa amekuwa mwembamba sana

Alafu neno hilo hilo ukiondoa "W" Itabaki AMEKUWA hii pia inatumika kwa kiumbe hai chochote lakini kiwe kimoja visiwe viumbe hai vingi

Mfano . Bakari China amekuwa mjuzi Wa kiswahili
Mbuzi amekuwa mnene.

Sasa sentensi "WAMEKUWA KUTUONA" neno wamekuwa hapo halioneshi kubadilika kwa hali ya watu kutoka katika hali moka kwenda nyingine.hivyo limekaa pahala sio pake.

Hapo usahihi ni kusema "WAMEKUJA KUTUONA"

Kama kuna swali Ndugu bakari unaweza uliza bila shida.
 
Nashukuru Ndugu Safuher, nimefahamu
 
Back
Top Bottom