Upo sahihi sana, kitu kimenishangaza kidogo una degrade kusoma coding, coding ndio foundation ya computer science, computer engineering, AI,..lazima watoto wajifunze coding language before anything else, hata Steve Jobs Ali stress umuhimu wa coding kwa kila mmarekani.Jukumu la elimu bora ni la Mzazi mwenyewe kuchagua aina ya elimu. kuendeleza elimu hii ya kikoloni ya kusoma kumaliza miaka au kubadilika kuwekeza kwenye elimu ya utambuzi na uvumbuzi yenye kumjengea mtoto kujiamini
Nipo Dodoma kwa sasa kutafuta PhD kama alama na sio kama uwezo
Wakati huo wenzangu wazazi wao wakiwasisitiza watoto wao wasome mambo ya Forced labour, Trigonometric, Integration by parts. Economics na Uhasibu
Mimi mzazi wangu alinipiga marufuku kusoma mambo hayo bali alininunulia Computer za kizamani sana zenye kutumia Floppy disk sio kama hizi za sasa za CD na Flash Disk
Kwa utu uzima wangu huu sikuwahi peleka watoto wangu Form five na Six hata Mimi sikuwahi soma form five na Six kwani mzazi hakunipitisha kwenye mfumo huo wa elimu na hata Yeye mzazi wangu mmoja wapo hakupitia mfumo huo wa Form five na Six
Miaka miwili ya Form five na Form Six iliniwezesha kufanya mambo kwa vitendo kama kujifunza kuagiza mizigo toka nje, Uwasilishwaji wa document muhimu kama vibali vya kuagiza bidhaa na uwezo wa kuunda Application tofauti
Coding Language ndio elimu ambayo mzazi alinifundisha kwa wakati huo, Niliharibu computer nyingi sana utotoni nikitaka kujua ndani ya computer kuna kitu gani tofauti na Radio au TV ambazo mara nyingi nilijua ndani kuna vitu gani
Coding language ndio kitu pekee nilikitumia kama fimbo ya kuchapia na kuweka mambo sawa kabla ya siasa, Watoto wangu wapo step moja mbele ya mimi hasa kwenye teknolojia
Wazazi smart baadhi Nawapongeza sana watoto wao wanapata hii elimu ya coding shule ya msingi kwa sasa. lakini kwa sasa coding imepitwa na wakati kidogo
Kwanini Mimi na wanangu tupo hapa Udom kwa sasa? Lengo letu ni PhD lakini kilichotuleta ni kuna vijana walipata tuzo kwenye mambo ya computer hasa kwenye "Hacking na Cyber Security" na ni wanafunzi wa kutoka Udom ndaki ya teknolojia hapa UDOM, Tunaamini kama hawa watoto wa wakulima wasio na vifaa na wana elimu ya kata wanajua vitu hivi basi moja kwa moja wana kitu cha ziada ambacho Mimi na wanangu hatuna au tunaweza ongeza nguvu nasi tukapata kitu kipya cha Uelekeo wa wajukuu zetu
Uelekeo wa Dunia sasa kwa wajukuu zetu hapa nyumbani ni Artificial Intelligence( AI). Tunajitahidi kuwekeza kwa watoto wa wanangu mambo ya AI na sio coding sana
Gharama ni kubwa sana sana kwenye haya mambo ya AI bali hatukati tamaa kwani hata Mimi mzazi hakukata tamaa juu yangu wala mimi sikukata tamaa kwa hawa vijana wangu nilionao hapa Dodoma kwa muda
Mambo ya Blockchain watu wanayojisumbua sana sasa ni mambo ambayo miaka ile ya dunia nyeusi akina Professor Mwandosya na baadhi kama Mathew luhanga walijifunza huko ulaya ufanyaji kazi yake na utengenezaji wake, Sorry Prof Mwandosya amestaafu na elimu yake wakati vijana kwanza hawaelewi hata maana ya Blockchain na wanaogopa kuwekeza huko
Artificial Intelligence( AI) ndio inatumika kwenye mambo yote kwa sasa ukiacha bara giza kama Tanzania, Upasuaji sasa umeanza kutumia Robots
Ni muda muafaka wa wazazi wenyewe kufanya maamuzi magumu ya kufundisha watoto mambo ya maisha na teknolojia na sio kupeleka kwenda kujifunza mambo yasiyo na msingi kwenye ulimwengu wa sasa
Nini maana ya mtoto kusoma Grade 1 mpaka Darasa la saba, Kuna kitu gani anaondoka nacho shule kwa miaka hiyo saba, Wazazi badilikeni
Wazazi wenye watoto wadogo bado mna muda wa kufundisha watoto mambo ya msingi kwenye teknolojia
Mwezi huu Desemba zaidi ya wanavyuo elfu tatu wamemaliza vyuo vikuu, Je kwa miaka minne au mitatu wamepata kitu gani cha maisha yao au ndio mambo ya Debit Cash and Credit Motor vehicle a/c
Tuwarithishe watoto wetu elimu yenye msingi mkuu na tuachane na elimu hii ya kusoma soma tu ili kumaliza miaka kadhaa
Kuna tofauti gani kati ya mwanachuo aliyemaliza chuo na mtu aliyeamua kutokusoma kabisa na akafanya biashara au akawa mwanasiasa na mbunge?
Tukiweka siasa pembeni kuna mambo ni jukumu la Mzazi mwenyewe na sio Serikali