Chini ya hizi sheria kandamizi za kinyangogo kiukweli lazima wakae karibu na swichi hasa pale MWANAUME LISSU AKIONGEA, hizi sheria za kipuuzi ni za kuongozea ng'ombe na siyo watu na akili zao kama LISSU ndo maana wanapata taabu tangu bwana wa burigi akamate usukani li nchi limekuwa la hovyo hovyo ngoja wanyooshwe na mnyooshaji mh. LISSU keshatia maguu.Nafikiri ITV na vyombo vingine vya mitandaoni siyo wanajipendekeza au wanajituma kumfurahisha JPM.
Kinachotokea hivyo vyombo vinamjua Lissu hachelewi kutoa kauli zinazoweza kupelekea kuwaingiza matatani vyombo usika kwa kurusha matangazo ambayo yanaweza kutafsiriwa kama uchochezi au ya uvunjifu wa sheria kwa mujibu wa leseni za urushaji matangazo. Ngumu kuhariri matangazo yanayorushwa mubashara (live), na Lissu is very unpredictable kwakweli, muda wowote anaweza kurusha maneno makali sana.
Mhariri wa gazeti flani ana kesi ya kujibu mahakamani sababu ya kuchapisha kauli au maneno flani ya Lissu. Kila siku kushinda mahakamani na kuwalipa wanasheria sababu ya kutaka kuwafurahisha watu wa chama flani ni uzembe katika biashara. Mara kadhaa tumesikia vyombo kama Clouds FM wakipigwa faini sababu ya maneno au simulizi flani ya mmoja wa watu walio alikwa kwenye kipindi cha njia panda!!
Kila mtu anajua jinsi TCRA inavyo zilima faini kubwa vyombo vya habari kwa kurusha vitu vinavyo tafsiriwa kama uvunjivu wa sheria na maadili.
ITV na media zote they are playing smarty kama ujuavyo sasa biashara ngumu na faini wanazolipa zinawaumiza zaidi wao kama biashara.
Ukumbuke mwisho wa siku zile ni biashara kama biashara zingine siyo charity organizations.