Makosa ya Tanzania yameinufaisha Msumbiji

Taifa lisilojua linakopaswa kwenda basi kila njia ni njia tu ilimradi awamu zinabadilika na safari inaendelea!!
 
August, Wewe kama unazijua hizo sababu za kuchelewesha, ulistahili kuweka hapa. Ndiyo faida ya jukwaa hili. Wewe unaweza kuwa unajua kimoja, na mimi nakijua kingine, na mwingine anayajua mawili.

Lakini mimi ninachokiongea ni kutokana na maelezo ya kutoka upande wa wawekezaji - kwa nini waliamua kwenda kuwekeza Msumbiji. Msumbiji ilikuwa tayari kwa huo uwekezaji, na walikuwa wanawataka wajenge hiyo LNG haraka wawezavyo wakati hapa kwetu walizuiwa kwa kuambiwa wanatakiwa kusubiri.

Lakini kilicho dhahiri ni kuwa wawekezaji hawa wapo Pemba, Msumbiji wakiendelea na shughuli mbalimbali ambazo hata kabla ya uzalishaji, tayari uchangamfu wa uchumi wa mji huo unaonesha mwanga uliopo katika uchumi wao.

Nimekwenda miji yenye miradi ya uchimbaji makaa ya mawe, idadi ya wakazi katika miji hiyo ni kama mji wa Singida lakini rasilimali za uchumi, na huduma za kiuchumi baadhi hazipo hata jiji la Dar. Ukifika tu unaona hapa kuna fedha, hapa kuna uchumi unaokua kwa kasi. Ndiyo maana sikushangaa kuona kuwa kwenye projections za ukuuaji wa uchumi wa mwaka huu, Msumbiji ni miongoni mwa nchi zinazoongoza, huku sisi kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 10, hatumo.

Fursa za kiuchumi ni time opportunity. Unamshangaa mtu anayesema eti madini au gesi haviozi. Hizi ni hoha za mbumbu katika uchumi. Dunia haisimami, kama nchi unahitajika kushindana na mataifa mengine. Unashundana kwa kutumia nini zaidi ya rasilimali zako ambazo zinaweza kutumika kama capital kwenye sekta nyingine kama vile viwanda?

Someni historia ya US, UK, Australia na Canada ili mjue ni sekta zipi zilijenga sekta nyingine - ni extractive industries. Sisi tunategemea kujenga sejta ya viwanda kutoka kwenye mapato ya sekta gani?
 
Bams,
Unarudia kule kule wewe unajali time, bila kujali content ya hiyo time yako.
Nyerere aliposema madini haya ozi na wengineo sio kwamba hawa oni au kujali time na opportunity bali the consequences za kukimbilia hiyo time.

Na Nyerere au wengineo sio kwamba hawajui usa, Australia na canada walivyofanikiwa, lakini wenzako alienda mbali zaidi na kuangalia Na jinsi gani Norway walifanya.

Sasa nenda kajielimishe hilo la Norway na pia hilo la time yako na experience ya Angola, Nigeria, Gabon na DRC kwenye maeneo ya mafuta na madini
 
Pascal Mayalla,
Nakubaliana na wewe. Hatuweki Priority kwenye vitu vinavyomgusa kila raia wa kawaida ila tunalazimisha kutafuta sifa.

Kama ulivyosema, wasichana wengi wamepata mimba za kubakwa au kulazimishwa sababu ya mfumo wa elimu ya kata ambapo wanatembea km. 10 inabidi wajitoe ili wapate lift za baiskeli. What next, mimba.

Kweli kulikuwa na ulazima wa kuanza kutoa maji kwenye mbuga wakati tumeshapata gas? Unasweka watu lupango ambao wangeweza kuinitiate how to utilise the natural gas to get electricity halafu unawanyang'anya wanayama maji? Why not Victoria or Tanganyika kama mtu alikuwa desparate kutumia maji? My days are numbered ila nawalilia wajukuu zangu.
 
Kuna wenzetu huaga wanawekeza sehemu kufuatia fursa zilizotangazwa na serikali, wakati wa sakata la gas ile ya Mtwara, nawafahamu baadhi ya watu Fulani walikwenda Mtwara kutafuta viwanja ili wajenge walau hotel (vitega uchumi) na hata nyumba kadhaa kwa maana ya kwamba Mtwara itakua na watu wengi wenye mahitaji hayo.

Kitu ambacho ni Kizuri sana, binafsi nilisita kidogo, na hata sasa kuna Rafiki zangu wana kasi ya ajabu kununua viwanja Dodoma ili wajenge nyumba za kupangisha, again nimesita; serikali zetu za Kiafrika/Kibongo hazina what's called consistency, huenda rais ajae anaweza kurudisha kila kitu Dar then mikopo yetu ya bank ikawa hailipiki tena.
 
August, Tatizo ni kwamba, hutaki kueleza unachokijua. Na siyo Norway tu lakini nchi nyingi za Ulaya, America, Australia, Asia na Africa, nazifahamu sheria zinaozoongoza sekta ya madini, mafuta na gas.

Kinachohitajika ni perfection. Perfection ni function ya time and accuracy.
 
Hizi Hydrocarbons zitakuwa ni mali hadi karne hii tu lkn kwenye karne ijayo kama utakuwa hukuitumia ya kwako, basi utakuwa umewaka.

Technology inaenda kasi sana na haisubiri mjinga yeyote na kiburi chake kwani mchuma janga hula na wakwao.

Leo hii nchi zilizoendelea zinaanza kuachana na matumizi ya mbao ili kuokoa mazingira pamoja na ughali wa mbao na wameingia kwenye "Synthetics" kama Polyvinyl Chloride nk ambayo inaweza ikatumika vizuri badala ya mazao ya mbao na tena ni cheap and environmentally friendly.

Kufikia mwisho wa karne hii, mashirika kama Tanesco yatakuwa yamekufa kwani teknolojia ya nishati ya jua itakuwa imeboreshwa mno kiasi kwamba kila mtu atakuwa na solar na inverter yake nyumbani kwake.

Vitu vyote vinavyotengenezwa kutokana na Hydrocarbons kama mafuta na gesi vitatengenezwa kutokana na Synthetics zingine na kuzifanya nchi zinazotegemea mafuta na gesi kufirisika...!!! Saudi Arabia tayari wamelitambua hilo.

Hivyo watanzania kama leo tulitegemea tuokolewe na gesi na ndio hivyo tumepata rais asiye na upeo kaamua atakavyo yeye basi ndio mkosi umetuandama hivyo tutaendelea tu kuchoma mahindi make hamna namna.
 
Nyanjomigire, Umenena vema. Hakuna wakati ambao Dunia itasimama eti kwa sababu kitu fulani kimekuwa depleted.

Mpaka mwaka 1967, Tanzania ndiyo nchi iliyokuwa anazalisha madini ya ulanga (sheet mica) yenye ubora kuliko nchi yoyote. Wakati huo kilo moha ya sheet mica, clear 1 type, ilikuwa inafikia £2,000.

Tukawafukaza wazungu kupitia Azimio la Arusha. Migodi yote wakakabidhiwa STAMICO. Waulize leo hii wanauza kilo ngapi? Ni zero.

Baada ya Tanzania kuringa na mica yake, wazungu waliingia kwenye tafiti. Leo hii viwanda karibia vyote vinatumia synthetic mica. Natural mica, hupati hata dola 50 kwa kilo.

Tanzania imekuwa Askari mmoja ambaye kila siku alikuwa anavaa buti ya jeshi, akawa anasema kuwa raizoni yake ya ngazi 6 itadumu hata miaka 20 maana haivai mara nyingi. Lakini ilipopita kama miaka 4 tu, siku alipovaa watu wakaanza kumtazama kwa mshangao na kumcheka. Kiatu kilikuwa kizima lakini kilikuwa out of fashion.

Kuna wakati makaa ya mawe yalikuwa ndiyo kila kitu. Yaliendesha meli na train. Leo yamebakia tu kwenye kuzal8sha umeme lakini yanapigwa vita hasa kutokana na uchafuzi wa mazingira. Sijui kama yale ya mchuchuma, yatakuja kuwa na faida kama hayatachimbwa ndani ya miaka 10 - 20.
 
Kalamu1, Kwanini mpaka kina Zitto na CHADEMA? Hapa ndipo Watanzania wanapikosea, kudhani ni tatizo la wapinzani!!. Mara ngapi wapinzani wamewaonya wananchi dhidi ya CCM? Je, wananchi wamewaunga mkono? Kosa si wapinzani ni wananchi wenyewe na style yao ya maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
tatizo sio CCM WALA MAGUFULI, TATIZO NI WATANZANIA WENYEWE..
HII NCHI KUNA MAPOPOMA WENGI SANA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LNG ni Liquefied Natural Gas.


Tunahitaji a medium size LNG processing plant.

Na ni vizuri tutumie LNG nyingi ndani ya nchi. Tuzalishe umeme over 10,000 MW per year.

Annual natural gas production iwe medium scale ili gesi idumu kwa muda mrefu sana.

Very large scale natural gas production combined with weak regulations, mara nyingi hunufaisha wageni kuliko wenyeji.

Na hisi kama wananchi wa Msumbiji hawata nufaika sana na gesi yao.
 
Umenena vema. Hakuna wakati ambao Dunia itasimama eti kwa sababu kitu fulani kimekuwa depleted.

Mpaka mwaka 1967, Tanzania ndiyo nchi iliyokuwa anazalisha madini ya ulanga (sheet mica) yenye ubora kuliko nchi yoyote. Wakati huo kilo moha ya sheet mica, clear 1 type, ilikuwa inafikia £2,000.

Tukawafukaza wazungu kupitia Azimio la Arusha. Migodi yote wakakabidhiwa STAMICO. Waulize leo hii wanauza kilo ngapi? Ni zero.

Baada ya Tanzania kuringa na mica yake, wazungu waliingia kwenye tafiti. Leo hii viwanda karibia vyote vinatumia synthetic mica. Natural mica, hupati hata dola 50 kwa kilo.

Tanzania imekuwa Askari mmoja ambaye kila siku alikuwa anavaa buti ya jeshi, akawa anasema kuwa raizoni yake ya ngazi 6 itadumu hata miaka 20 maana haivai mara nyingi. Lakini ilipopita kama miaka 4 tu, siku alipovaa watu wakaanza kumtazama kwa mshangao na kumcheka. Kiatu kilikuwa kizima lakini kilikuwa out of fashion.

Kuna wakati makaa ya mawe yalikuwa ndiyo kila kitu. Yaliendesha meli na train. Leo yamebakia tu kwenye kuzal8sha umeme lakini yanapigwa vita hasa kutokana na uchafuzi wa mazingira. Sijui kama yale ya mchuchuma, yatakuja kuwa na faida kama hayatachimbwa ndani ya miaka 10 - 20.

Uko sahihi sana mkuu. Kile ambacho wengi tunashindwa kuelewa na kuzingatia ni kuwa sio rasilimali zinazotuwekea ukomo kwenye maamuzi bali maamuzi yetu ndiyo yanayotumilikisha hizo rasilimali.
Karne kadhaa zilizopita wazungu wa Ulaya waliamua kujimilikisha Africa na mpaka leo wanaimiliki kwa kiasi kikubwa kupitia machinations mbalimbali licha ya kutoa huu uhuru bandia ambao wengi wasiojua bado wanajivunia. Hii ni kutokana na maamuzi tu tena ya watu wachache.
Katika kipindi hicho pia mtangulizi wa ukoloni wa Afrika ya kusini, Cecil Rhodes aliamua kuwa dhahabu yote ya eneo hilo iwe ya kwake yeye na washirika wake na vizazi vyao. Na ndivyo ilivyo mpaka leo. Maamuzi tu ya mtu mmoja, lakini maamuzi sahihi.
Majirani zetu Kenya ambao Mwl Nyerere aliwaita nyang’au waliamua kuwa mlima Kilimanjaro ni wa kwao na kwa kiasi kikubwa ukawa wa kwao angalau kwa kipindi fulani ingawa kilitosha kuchuma faida si haba.
Majigambo ya kuwa tumejaliwa rasilimali nyingi na kwamba eti madini au gesi ni vitu visivyooza ni vichekesho tu visivyo na maana yoyote kwenye dunia ya leo.
Ni binadamu walioamua kuwa madini ya dhahabu yawe kipimo cha thamani na hivyo kuufanya umiliki wake kuwa tamanio kubwa la mataifa, mashirika na hata watu binafsi.
Kizazi kijacho kinaweza weka kitu kingine kuwa mbadala wa dhahabu na huo ukawa ndio mwisho wa thamani yake. Nishati nyingine yoyote kama umeme, mwanga wa jua n.k yaweza chukua nafasi ya gesi asilia na hivyo kuishusha thamani yake achilia mbali uwezekano wa watu wengine kuamua kujimilikisha hiyo gesi.
Ni vizuri tukafahamu kuwa inahitaji nguvu kubwa kumiliki kitu ambacho hukifanyii kazi au kukitumia.
Kwa suala la gesi asilia katika bonde la mto Ruvuma kutokana na mada, kwa uwiano, maamuzi ya jirani zetu yana manufaa zaidi.
 
Back
Top Bottom