MAKOSA ya matamshi na uandishi.

DEVINE

JF-Expert Member
Mar 11, 2011
536
86
Inabidi tusaidiane wana JF kuhusu hili tatizo la matamshi na uandishi wa baadhi ya maneno ya kiswahili ili tuepuke kuharibu lugha hii,kwa mfano;
...kura chakula,badala ya kula chakula.
...abari zako,badala ya habari zako.
...piga kula,badala ya piga kura.
...kalibu,badala ya karibu.
...hasubui,badala ya asubuhi.
...askali,badala ya askari
...malanyingi,badala ya maranyingi.
...eshima,badala ya heshima.
Yako makosa mengi yanayo jirudia ningependa nawe pia uyaainishe hapa.
 
Inabidi tusaidiane wana JF kuhusu hili tatizo la matamshi na uandishi wa baadhi ya maneno ya kiswahili ili tuhepuke kuharibu lugha hii,...
Yako makosa mengi yanayo jirudia ningependa nawe pia uyaainishe hapa.
Mkuu, tuhepuke nadhani inatakiwa iandikwe tuepuke!
 
Eti jamani kipi sahihi,Kusema 'analinga' au 'anaringa' ?
 
Inabidi tusaidiane wana JF kuhusu hili tatizo la matamshi na uandishi wa baadhi ya maneno ya kiswahili ili tuhepuke kuharibu lugha hii,kwa mfano;
...kura chakula,badala ya kula chakula.
...abari zako,badala ya habari zako.
...piga kula,badala ya piga kura.
...kalibu,badala ya karibu.
...hasubui,badala ya asubuhi.
...askali,badala ya askari
...malanyingi,badala ya maranyingi.
...eshima,badala ya heshima.
Yako makosa mengi yanayo jirudia ningependa nawe pia uyaainishe hapa.

Nilitaka kuanzisha thread kulalamikia usahihi wa waandishi wetu katika matumizi ya lugha ya kiswahili, lakini acha niongezee haphapa kwako mkuu,

1. Masuala mazima..... badala ya suala zima
2. Mazingara badala ya mazingira
2. Lisaa badala ya saa, masaa badala ya saa.
kwa kweli mimi huwa nakereka zaidi pale wana habari ambao ni jukumu lao kuelimisha jamii wanaposhindwa kujua hata vitu basic kama hivi, are they real seroius? au unakuta mtangazaji anasema gari limepata ajali na watu kadhaa wameweza kupoteza maisha, this is rubbish jamani hebu mpende kujifunza.
 
Nilitaka kuanzisha thread kulalamikia usahihi wa waandishi wetu katika matumizi ya lugha ya kiswahili, lakini acha niongezee haphapa kwako mkuu,

1. Masuala mazima..... badala ya suala zima
2. Mazingara badala ya mazingira
2. Lisaa badala ya saa, masaa badala ya saa.
hiyo number 2a hayo ni maneno mawili tofauti yenye maana tofauti, huenda mtumiaji alimaanisha mazingara ktk hali ya ushirikina.
 
Nyimbo: uwingi Wimbo: umoja Kwahiyo sentensi kama: "Hii Nyimbo kali kweli!". Ni afadhali ukasema: "Huu wimbo mkali kweli!"
 
Amefariki tarehe 22/07/2003 badala ya alifariki tarehe 22/07/2003 ili kuonyesha wakati uliopita yani past tense, ama amelala badala ya analala kuonyesha kitendo kinaendelea wakati huo (Present continuous tense).
 
Back
Top Bottom