makosa ya marafiki wawili(boyz 2 men) yametugharimu jimbo

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kidogo babu yenu nimerudi jamvini kwa mara nyingine tena.
Nilienda arumeru kutetea chama kikongwe cha mapinduzi.
Awali ya yote nachukua fursa hii kuwapongeza chadema kwa uwezo wao mkubwa wa KULINDA KURA kwasababu hili limekuwa ni tatizo lao kubwa hasa ukizingatia hawana miundo mbinu ya kutosha.
Nimeshangazwa ni wapi wapinzani wetu walipopata habari kuwa chupa moja ya chai inaweza kubeba kura 1000.sielewi ni nani aliyekuwa anavujisha siri ya vikao vyetu vya ndani pale hoteli ya gateway na baadaye pale ndesa lodge!!
Yote kwa yote hongereni wapinzani,naona mmeanza kukomaa.

KOSA LA JK
Mwenyekiti wetu ndiye aliyetoa wazo la Siyoi kugombea jimboni huko.(ile siku ya mazishi ya mzee sumari)
Baada ya kuuza wazo hili kwa wazee,tulimsihi kuwa hili ni pigo kwa ccm kwani kijana Siyoi hana uzoefu na hajulikani sana na wapiga kura wa meru.
Ninashukuru alituelewa na kutuma ujumbe juu ya hilo.pendekezo likawa ni willy sarakikya.maazimio yalifikiwa tuhakikishe sarakikya anapitishwa,chiligati na msekwa walijitahidi katika hili lakini......maji yakimwagika hayazoleki!


KOSA LA LOWASA
Baada ya kuona mwenyekiti kateleza ndugu EL aliamua kutumia fursa hii kuhakikisha Siyoi anapitishwa,aliamua kumwaga fedha na baadae kuchukua jukumu la kumuuza Siyoi kwa wameru.
Kabla ya lowasa kupanda jukwaani upepo ulikuwa upande wa ccm lakini kuna tuhuma zilitolewa na wazee wa kimeru kuwa lowasa aliwatukana wakati wa kampeni, hili nimelithibitisha wakati nikiendelea kuwashawishi wazee wenzangu kuichagua ccm.

Kwa ufupi ni hayo tu niliyoweza kuyaobserve huko arumeru mashariki.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
huu ni ukweli mchungu kwa wana ccm.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
kuna dalili za ka ukweli hasa hili la chupa kubeba kura 1000 hii kali ya 2012
hizi ni mbinu za vijana wenzenu.kumbuka ccm hatuishiwi mbinu.najua tutagundua mbinu mpya na za kisasa zaidi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
hizi ni mbinu za vijana wenzenu.kumbuka ccm hatuishiwi mbinu.najua tutagundua mbinu mpya na za kisasa zaidi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!

Mbinu zenu za kuiba kura zimeshindwa, mbinu pekee ni kutangaza mshindi bila kuangalia kura za wananchi, lakini mjue siku hiyo ndio itakuwa mwisho wa amani tanganyika.
 
Tungeshinda tu na hizo mbinu za kuiba kura lazma tuzijue tu manake chadema inapendwa hata na watu wa ccm.
 
Marafiki wawili aka boyz2men hawa hapa
jkel.jpg
 
CCM wanasubiri ''Kwa Msaada wa watu wa Marekani'' ndo washinde
 
CCM wanasubiri ''Kwa Msaada wa watu wa Marekani'' ndo washinde

kwa hiyo ushindi wa chadema ni kwa msaada wa watu wa Tanzania.nakumbuka fundrising iliyofanywa na chadema pale naura springs

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Kama mkakati mkubwa uliokuwa ukitegemewa kuleta ushindi CCM ilikuwa ni kuchakachua, basi ni kweli CCM iko taabani na mwisho wake ushawadia.
 
Natamani uchaguzi urudiwe tena maana tulipata za bure maana january alimwaga noti pale makumira kuna hotel maarufu kila kijana 10,000 kule poli barazani kila toyo 30,000 ya ili kuwa kula CCM kura CHADEMA wenzenu tulifaidi sana
 
Back
Top Bottom