Makosa ya Magufuli na afanye nini

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,723
9,029
Kuna vitu ambavyo Magufuli anakosea na sio vibaya kukosoana kimaendeleo.


1. Viongizi unao wachagua: Uongozi na usomi ni vitu viwili tofauti. Kitendo cha Magufuli kufikiria kwamba watu waliosoma sana ndiyo watakuwa viongozi wazuri itarudisha nchi nyuma. Ni lazima aelewe vitu vichache kwenye hili. Mfumo wa uchumi wa dunia ya sasa ni wa kibepari hata hao China, Korea, Japan ... na nchi nyingine zimeanza kuendelea baada ya kuanza kufuata mfumo huu . Ni lazima uweke watu ambao wana historia ya kuleta matokeo ya utendaji badala ya kubahatisha na wasomi ambao wengi wao hawajawahi kufanya kazi ambazo ni za kisimamia vipato, watu na sera kwenye mfumo huu wa kibepari. Ukiweka watu wengi kama unavyofanya sasa ambao ni wasomi mpaka PHD lakini hawana vipaji na wala ujuzi wa kuongoza ni sawa na kuwapa ramani watu ambao ni vipofu. Ni lazima ieleweke hizi degree za juu advance master na PHD ni degree za utafiti na sio za uongozi mfano unaweza kuwa na bigwa daktari lakini haina maana ndiyo atajua kuendesha Hospitali kwasababu uendeshaji wa hospitali na utaalamu wa magojwa ni vitu viwili tofauti na ni vipaji tofauti!. Usiko angalia hili utaangashwa na hao hao wasomi!. Ukipata wasomi na wakawa na vipaji vya viongozi ni nzuri lakini ukweli ni kwamba wasomi wengi sio kama wewe wakati wanasoma walikuwa hawafanyi kazi nyingine hivyo hata uzoefu hawana. Jiulize mpaka sasa pamoja na wasomi kuna master plan gani ya mifumo kama afya, elimu, land, uwekezaji.. hakuna ni kila waziri kuamka na chake kila siku na kujaribu kutafuta sifa badala ya kuja ma master plan endelefu Waziri kuja na kubadilisha mfumo wa sekondari kwa fikra zake binafsi sio sera endelefu, wazira kuja na kubadilisha mfumo wa viwanja na mashamba sio mfumo endelefu kunatakiwa kuwe na mfumo endelefu wa miaka mingi ambao sio wa kubahatisha

2. Serikali haitumii takwimu: Serikali imekuwa inafanya vitu kutokana na matokeo badala ya kufanya vitu kwa matokeo endelevu. Kuna mifano miwili ya kuelezea hili. Serikali yako imeweka sera nzuri ya elimu bure na kwasababu hiyo unasema kwasasa kuna wanafunzi wengi sana watoto wameongezeka kwenye mashule na kuna uhaba wa madawati swali la kwanza je serikali ilikuwa haijui kwamba kuna watoto wa umri wa shule hawako shule? Na kama hawajui ni tatizo kwasababu sensa ya nchi nzima imefanyika miaka michache tu iliyopita sasa je data za sensa hazijaonyesha hao watoto! Au hao wasomi uliyowaweka hawajui na hakuna utamaduni wa kutumia data!. Mfano mwingine ni kuhusu sukari wakati una kataza sukari kutoka nje na kusema viwanda vyetu vitatengeneza sukari kuna mawili moja inawezekama waliokupa idadi ya matumizi ya watanzania walikuwa hawajui matumizi ya kweli au viwanda vimedanganya kwa uwezo wao wa kuzalisha sukari na ndiyo maana kukatokea upungufu. Lakini kibaya zaidi ni kwamba inaelekea takwimu ni za kubahatisha na zinafanya na kuleta sera za kubahatisha sasa serikali imeingia kwenye biashara ya sukari wakati waototo hawana madawati! Hizo pesa zingetumika kwa shughuli nyingine. Ni lazima uelewe kwamba hakuna pesa isiyo na kazi hivyo kutumia pesa kununua sukari bila kuwa na ulazima ni makosa hiyo pesa ingetakiwa iwe sehemu ambayo inaleta faida au kuwekeza kwenye miradi ujue madeni ya nchi yanaenda kwa muda ukilipa gharama za riba nazo zinapungua.

Demokrasia: Vitando vya serikali kuzuia mikutano ya siasa sio nzuri kwasababu Tanzania imefikiwa wakati wananchi wanajua demokrasia hivyo kuongea ni kitu kizuri. Huwezi kurudi nyuma kwenye demokrasia!. Kuzuia mikutano hakitasaidia chochote sio kwamba watu kuongea ndiyo hawafanyi kazi ! vilevile siku hizi **** whatup group, mitandao huwezi kuzuia watu kuongea ni kujidanganya. Lakini kibaya zaidi ni kitendo kinacho onyesha kwamba tuna raisi ambaye hataki mtu yeyote amseme vibaya kwa lolote ni bora ujue kwa uwazi kuliko watu kuweka ubaya kwenye moyo. Watu wasiko ongea haina maana wanakupenda.Nitaendelea kutoa mawazo yangu ….baadae
 
Hakuna aliye mkamilifu na hata akikuridhisha wewe haimaanishi hatapingwa tena
 
Back
Top Bottom