Makosa ya Lissu, Membe ni fundisho chaguzi kuu

Sep 8, 2020
67
150
Na Mwamba wa Kaskazini

Ni dhahiri kuwa tathmini ya kampeni, kura za maoni na matakwa ya wapigakura wengi (election issues) vinahitimisha kuwa ni dhahiri wagombea wawili mashuhuri wa upinzani, Tundu Lissu na Bernard Membe wameadhibiwa na wapigakura kwa sababu zile zile za kimkakati za makosa ya vyama vya upinzani nchini. Hebu tuangalie hizi 10:

1. Bado upinzani nchini hauna umoja wa maana unaoweza kuitikisa CCM;

2. Vyama vya upinzani kukurupukia wagombea ambao ama hawakujiandaa au hawakuandaliwa- Lissu kaja kimzukamzuka na Membe kaja kama kizuka, kazuka tu;

3. Ajenda hasa ya upinzani ni ipi, haikujitokeza katika kampeni hizi;

4. Wapinzani kuendelea na tatizo la kutojipanga kisiasa kabla ya uchaguzi-tuliona hata wagombea wao walivyojaza fomu kimazabemazabe katika chaguzi ndogo na zile za Serikali za mitaa, mtu kwenye anuani anaweka jina!!!

5. Kupinga hata yaliyowagusa wananchi-hili ni kosa linalojirudia sana yani kuwa mpinzani halafu unaponda miradi ya maji, elimu, afya na miundombinu halafu unachoponda ndio unachoahidi katika ilani, inakula kwako;

6. Kutegemea hela za mabeberu wa nje-ukimuangalia Lissu na Membe wote kampeni zao zilipata shida sana kwa kuwa walitegemea sana fedha za nje ya nchi ambazo huenda hawakuzipata;

7. Umoja ndani ya vyama haupo-Muangalie Lissu alifanya kampeni hata bila Mwenyekiti wake, Katibu Mkuu wa Chama wala waasisi wa chama kama kina Mtei hapo unashindaje? Membe ndio kwanza wenzake wote Zitto na Seif walifika hatua si tu kumkacha bali walimkana "mara tatu" hadharani. Hapo unashindaje uchaguzi!

8. Uongo, uzushi na kutokuwa makini kufuatilia mambo. Mgombea kama Lissu anamambo ya harakati sana na hana muda wa kusoma. Katika kampeni hii ameyumba sana katika facts na kujikuta mara kadhaa akiadhiriwa kwa kupewa facts za hakika kutokana na hoja za kuropokaropoka!!!

9. Kutukana au kutoa maneno ya kejeli kwa kila mtu; watumishi wa umma, Tume, viongozi wa dini, wanahabari, wasanii n.k Hapa unataka kushinda uchaguzi gani sasa? Kila uchaguzi hili linajirudia!

10. Kuunga mkono sera za kijinga kama ushoga. Unashindaje uchaguzi Tanzania, Taifa la watu wenye imani zao mbalimbali, kwa kuahidi ushoga??!
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,486
2,000
Sami wewe ni muislam (kutokana na jina lako) na zaidi ni binadamu tunaeamini umeelimika kiasi fulani na isitoshe kama binadamu tunaamini unamuogopa Mungu, sasa nikuulize tu IKITOKEA MMEKAA WAWILI TU WEWE NA MTUME MUHAMAD AKAKUANGALIA MACHONI AKAKUULIZA MWANANGU SAMI WEWE KABISA UNAAMINI MAGUFULI ALIPATA KURA MIL 12 NA LISSU MILIONI 1? Utamjibuje Sami.
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
8,682
2,000
Nitakuwa mstari wa mbele kesho nikiwa na bendera 2, ya ACT na Chadema. Pia nitakuwa na dumu la lita 5 lenye petroli na kiberiti mfukoni. Halafu Siro ajaribu kunigusa.
 

kamba0719

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
468
1,000
images (22).jpeg
 

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
5,751
2,000
Ule haukua uchaguzi hata kidogo, Magufuli katumia nguvu ya dola kujitangazia ushindi ila katika nafsi yake hakunq na hatakua na amani ya huo ushindi, Raha ya ushindi mshindane .
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,451
2,000
Ukweli unauma na ukiwa na akiri unakubali makosa ili uone wapi umekosea ila kwa andiko lako hili utatukanwa na wabinua viuno na kuona kwamba walikuwa sahihi bila kujitafakali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom