Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Wakuu,
Mpaka sasa inaonekana kama vile Hayati Julius K. Nyerere ndiye "mkosaji pekee" katika kile kinachodaiwa kuwa ni "UBATILI" wa Muungano! Mwenzake Hayati Karume anaonekana yuko innocent kabisa au labda ni kuogopa ile "dhambi" iliyowahi kutamkwa na Baba wa Taifa mwenyewe kuwa ni "kuogopa kuwaudhi Wazanzibari!"
Kwa maoni yangu mzigo wote wa lawama unatakiwa aubebe Karume, kwa nini?
1. Kwa sababu hakupeleka Hati za Makubaliano Ya Muungano kwenye Baraza la Mapinduzi kuridhiwa! Hili hata hivyo kwangu mimi si tatizo kuhusu UHALALI wa Muungano, kwa kuwa kuridhia sio lazima kusaini, hata kwa "conduct" tu inatosha! Kama wengine mnaamini katika kusaini basi mzigo huo anapaswa aubebe Karume!
Sidhani kama ilikuwa kazi ya Nyerere kuanza kuwahoji Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi kuwa mmeridhia au la, hayo yalikuwa yafanywe na Karume!
2. Karume alipokea cheo cha Makamu wa Kwanza wa Rais hata bila kuridhiwa kwa Hati huko Zanzibar! Sioni hapa kosa la Nyerere liko wapi!
3. Kutwaa Mamlaka ya Zanzibar taratibu. Mamlaka haya hayakutwaliwa bila ridhaa ya Karume na Marais waliofuata. Kila kitu kilifanyika kwa makubaliano na kwa ridhaa ya Karume, Marais waliofuata pamoja na Wazanzibari wote! Sasa haya matusi dhidi ya Baba wa Taifa, Mwl Julius K. Nyerere yanatoka wapi?
4. Kwa kweli kama tumeamua "kufunguka" tuwe wakweli, isionekane kwamba Wazanzibari waliduwaa kama kondoo wakati masuala mbalimbali ya Muungano yanafanyika!
5. Sisemi Karume atukanwe kama alivyofanyiwa Hayati Nyerere la hasha bali lawama zilenge mhusika, kama ni lazima sana kulaumu!