Makosa ya January Makamba ni yapi haswa, Watanzania tuache majungu natujikite kufanya kazi

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Toka January Makamba achaguliwe na Mh Rais mwaka jana kuwa Waziri wenye dhamana ya Nishati kumekuwa na mijadala ya hovyo dhidi yake...

Wizara ya Nishati kwa miaka nenda rudi imekuwa ni wizara yenye changamoto kwa kila Waziri anayechaguliwa

Na matatizo haya yalianza kwenye awamu ya pili pale mikataba mibovu iliposainiwa lenye lengo la kuondoa matatizo ya Umeme Nchini..

Watanzania wote tunaelewa shida ya kukatika umeme ni nini pia tatizo la sasa kupanda kwa gharama za mafuta ni nini,

Inasikitisha sana kuona matatizo ya miaka mingi yote lawana zote anapewa JM

Ndio kwanza ana mwaka mmoja toka akabidhiwe wizara hii, Vizuri tumpe muda wa kutosha na badae ndio tuje kumhukumu

Kingine watanzania tuache roho ya "Wivu kila uchao majungu muda wote. Nadhan ni wakati mzuri tuwe tunatoa ushauri ambao utasaidia kuboresha changamoto za wizara ya Nishati kuliko lawama ambazo hazina tija

Mwisho, Mh Rais Samia anajua uwezo mkubwa wa Mh JM kuwa changamoto zote za wizara hii zitapatiwa ufumbuzi, Tumpe muda wa kutosha..

Alex Fredrick
 
Mkopo wa Bumbuli SACCOS toka NSSF ambao haujawahi kulipwa unaokadiriwa kufikia $1,000,000

Kashfa ya dadaake ya kuomba $2,000,000 toka kwa mzungu kwa ajili ya kumsaidia kakaake kwenye kampeni za urais 2015 kwa ahadi ya kupewa migodi

Kuanza kampeni za kujijenga kuelekea 2025 kupigia kugawa mitungi ya gas mikoani kwa gharama za serikali

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Punguza wivu
 
Wanaomlaumu na kumahutumu Makamba, wote hawana hoja za msingi zaidi ya wivu, majungu na kufuata mkumbo wa wanasiasa wa upinzani wanaomchafua kwa maslahi yao ya kisiasa. Makamba ni kiongozi kijana smart, mbunifu, mchapakazi na mwenye malengo makubwa kisiasa.
 
Hapana utakuwa una beliefs zako mkuu. Zile software za wahindi hela zetu 70Bn na bado umeme unakatika kusikohesabika. Ujanja janja tu. Kwani hakina wengine wenye uwezo mbona Kama wao tu ndio wanaorudishwa rudishwa. Let say mbona Muhongo prof hajawahi kurudishwa ama kupewa wizara yyte. Sio huyo tu Ina Mana Ni hao hao na nape ,tumeshawajua mnabebana mnalazimisha kupendwa. Vipi Lukuvi amekosea Nini akatolewa Ile wizara akapewa wa misheni town Ni makamu Ila Kama yeye ndiye ana sauti Mana kila akitakacho lazima atatendewa.
Pia Ni kwa Nini maraisi wakristo tu ndio wanaokufa ama ndio Mungu anawapenda Jamani,kila Jambo Lina malipo karma is the real ama huamini. Kila kitu unapanda mbegu utaivuna lazima ukubali uikatae.
Kibali Cha kuagiza mafuta wamepewa kibali kiswahiba,wenye uwezo wote waambiwe waagize ili wote wafaidike.
Pia dart watu walete magari ya kiwango kinachotakiwa msifikiri ni nyie tu manweza kula.

Ni kwa Nini alipinga bwawa lisijengwe ili gesi ya babaye iuzike tuumie na huku ulitakiwa tupate umeme cheap kidogo kuliko hii gesi Mana kjt amechukua shares anatuumiza mno watanzania.
Mbolea ndiye muagizaji. Jpm alitaka kufanya mapinduzi kwa nishati akapendwa na babaye.

Punguza wivu
 
Dart serikali ijenge barabara halafu wafanyabiashara waagize magari Kama Yale Yale ya kiwango ili ushindani uwepo ,ama hizo njia ziruhusiwe daladala zingine zitumie.

Yaani

Mbona kuagiza mafuta wangepewa wote wenye uwezo.

Zile 70bilioni zimefanya Nini.

Mbona akiweka bodi ya kipigaji

Yaani umasikini na ujinga wa watanzania wachache wananufaika nao.
Kuna bomu linalipuka..saivi wapinzani wamehatuliza wamelamba asali hata hawana kelele wametulia.
Eti mchakato wa katiba mpya mpaka miaka Tisa ipite
 
Ni mtihani kipindi cha Hayati hatukuwa na mgao wa umeme sasa ni tofauti..
Mafuta mhh ngoja wajuzi waje..
 
Mkopo wa Bumbuli SACCOS toka NSSF ambao haujawahi kulipwa unaokadiriwa kufikia $1,000,000

Kashfa ya dadaake ya kuomba $2,000,000 toka kwa mzungu kwa ajili ya kumsaidia kakaake kwenye kampeni za urais 2015 kwa ahadi ya kupewa migodi

Kuanza kampeni za kujijenga kuelekea 2025 kupigia kugawa mitungi ya gas mikoani kwa gharama za serikali

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
Asante kwa muongozo wako,kakuelewa muuliza swali
 
Toka January Makamba achaguliwe na Mh Rais mwaka jana kuwa Waziri wenye dhamana ya Nishati kumekuwa na mijadala ya hovyo dhidi yake...

Wizara ya Nishati kwa miaka nenda rudi imekuwa ni wizara yenye changamoto kwa kila Waziri anayechaguliwa

Na matatizo haya yalianza kwenye awamu ya pili pale mikataba mibovu iliposainiwa lenye lengo la kuondoa matatizo ya Umeme Nchini..

Watanzania wote tunaelewa shida ya kukatika umeme ni nini pia tatizo la sasa kupanda kwa gharama za mafuta ni nini,

Inasikitisha sana kuona matatizo ya miaka mingi yote lawana zote anapewa JM

Ndio kwanza ana mwaka mmoja toka akabidhiwe wizara hii, Vizuri tumpe muda wa kutosha na badae ndio tuje kumhukumu

Kingine watanzania tuache roho ya "Wivu kila uchao majungu muda wote. Nadhan ni wakati mzuri tuwe tunatoa ushauri ambao utasaidia kuboresha changamoto za wizara ya Nishati kuliko lawama ambazo hazina tija

Mwisho, Mh Rais Samia anajua uwezo mkubwa wa Mh JM kuwa changamoto zote za wizara hii zitapatiwa ufumbuzi, Tumpe muda wa kutosha..

Alex Fredrick
Ni wapuuzi tuu hao.Huwa nawaambia mnataka nani ateuliwe Ili tuone kama umeme hautakatika..

South Africa inahangaiaka na umeme kukatika sembuse Tanzania?
 
1.Kwenda kuchukua fomu ya urais 2015 bila kumjulisha JK ambaye alikuwa mshauri na mtu wake wa karibu.

2. Kutumia zaidi ya millioni 300 mwaka 2010 kumtoa william shelukindo jimbo la bumbuli kinyume na utaratibu. Na hii alihonga hadi akapita bila kupingwa. Baba yake akiwa katibu mkuu alijua hili na akabariki.

3. Kumsema Magufuli baada ya sauti kuvuja akisema wanatafuta uhuru wao baada ya kuona Magu anawabana. Hii iliendana na kifo cha Magu mwaka 2021.
 
Back
Top Bottom