Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,912
Mwalimu alifanya mengi mazuri kwa nchi hii lakini alijisahau katika mambo mwili ambayo alishindwa kuyaona na hivyo alishindwa kuchukua hatua stahiki kwa wakati.
Mwaka 1984/1985
Mwalimu Nyerere hakupaswa kung'atuka kabla hajabadili katiba. Katiba ya mwaka 1977 ilimfaa yeye labda na marehemu Sokoine tu.
Mwaka 1992
Licha ya Baba wa Taifa kutumia ushawishi wake kuhakikisha mfumo wa vyama vingi unaanzishwa hapa nchini,alisahau kuwa Katiba yetu bado ni ya mfumo wa chama kimoja hivyo ilipaswa kubadilishwa kwanza kabla ya kuruhusu rasimi mfumu huu kuanza hapa nchini.Mabadiliko ya kutambua tu uwepo wa vyama vingi hayakutosha bali tulipaswa kwenda mbali zaidi.
Katiba ya mwaka 77 inampa Raisi wa nchi hii madaraka makubwa mno kiasi kwamba hata mwalimu Nyerere mwenyewe aliwahi kukiri kuwa Katiba hii inaweza kumfanya mtu kuwa na tabia fulani.
Hivyo kwa mtazamo wangu, kinachosemwa na watu leo hii kama ni cha kweli,basi huenda ndio kutimia kwa unabii huu wa mwalimu Nyerere hivyo mimi sishangai sana labda napaswa kushangaa kuwa kuna mtu katimiza ndoto hii ya mwalimu na si vinginevyo.