Salum Mayanga ni kocha ambaye amekonga mioyo ya Watanzania kwa muda mfupi kutokana na kuunda Taifa Stars mpya ya vijana wadogo wenye vipaji vikubwa na ari ya kucheza soka. Amebadilisha mfumo kutoka ule wa kubutuabutua hadi kuweka mpira chini kwa pasi nyingi na kucheza kwa kushambulia zaidi. Kifupi binafsi nimetokea kuwa shabiki wake, japo katika mechi 3 alizosimamia Tiafa Stars amenifanya hofu niliyokuwa nayo baada ya mechi zile mbili za kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi ithibitike leo. Pamoja na mpira kuwa na matokeo 3 sikuzote lakini sare ya leo ya Taifa Stars vs Lesotho imechangiwa kwa kiasi kikubwa na makosa makubwa matatu aliyofanya Salum Mayanga kama kocha.
1. UPANGAJI MBOVU WA KIKOSI
Nimekuwa nikishangaa sana Taifa Stars kucheza bila kuwa na mchezaji au mfumo wa kumchezesha Samatta. Tangu alipotoka Haruna Moshi Boban, tumekuwa hatuna mshambuliaji mzuri wa pili ili anayeweza kupangua ngome au kupiga pasi za kuifungua defence ya timu pinzani na kutoa pasi za magoli kwa Samatta. Ajibu angeweza kufanya hili lakini bado anakaa sana na mpira bila sababu, lakini yeye ni afadhali kuliko wengine. Navutiwa sana na Kichuya akicheza kulia kama anavyotumika akiwa Simba na alivyokuwa Mtibwa. Wanapangwa Mao Mkami na Muzamiri Yahaya lakini wote licha ya commitment zao kuwa kubwa, hawalainishi mipira ndio maana inabidi Samatta atumie muda mwingi kukaa na mpira atoe pasi kisha awahi mbele yeye mwenyewe kutafuta nafasi za kufunga! Mayanga jaribu kuwachezesha Mao, Muzamir na mmoja kati ya Ndemla au Sureboy halafu ushambuliaji waache Samatta na Mbaraka na winga mmoja tu kati ya Kichuya na Msuva.
2. KUCHELEWA KUBADILISHA MBINU ZA MCHEZO
Mayanga umeona kabisa Taifa Stars ilikuwa ikitawala mchezo lakini bila kutengezea nafasi za kutosha. Ulimwengu aliyecheza leo sio yule tunayemjua, Msuva alipoteza uelekeo toka mwanzo wa mchezo na idara ya kiungo ilizidiwa idadi na maarifa na kiungo cha Lesotho. Timu imecheza mfumo huohuo hadi zaidi ya dkk 75 huku ikiwa imedhibitiwa kabisa eneo la kiungo lakini Mayanga hakuonesha ile urge ya kulazimisha ushindi. Ajabu ni kuwa Majanga amesubiri hadi karibia dkk za mwisho wa mchezo kufanya mabadiliko tena yasiyokuwa ya kiufundi kabisa. Alitoa winga akaingiza winga, akatoa kiungo akaingiza kiungo, akatoa mshambuliaji akaongeza mshambuliaji! Kimsingi kwa jinsi Lesotho ilivyokuwa inacheza kwa kukaba njia alipaswa kuondoa winga mmoja mapema kabisa kati ya Kichuya na Msuva na kuingiza kiungo aina ya Salumu Abubakari au Said Ndemla ili idadi na pia kuongeza ubunifu eneo la katikati ya uwanja. Pia Mayanga anajua silaha ya Msuva ni kasi maana si mpigaji chenga mzuri, alipaswa kupanua uwanja ili kutengeneza nafasi za yeye kukimbia na kupiga krosi-pasi. Msuva leo hajatengeza nafasi hata moja, kitu ambacho ni habari mbaya mno. Ulimwengu alikuwa mzito kiasi, na Lesohto wanakasi kutokana na maumbile yao, Mbaraka Yusufu alipaswa kuingia mapema zaidi.
Mayanga ongeza ufanisi wa kikosi chako kwa kufanya Msuva na Kichuya wagombanie namba, wasicheze pamoja. Ule utofauti wao unaweza kuleta kitu kipya ndani ya mechi kwa mfano anapoanza mmoja na baadae akaingia mwingine inaweza kuleta utofauti mkubwa.
3. KUKAA KIMYA MUDA WOTE WA MCHEZO
Mayanga ni kocha mwenye uwezo mkubwa ila uko too quite, too passive! Ukikaa umekaa utadhani unasimamia timu iliyosheheni professionals! Kama Zidane anaweza kusimama kuwaelekeza wachezaji aina ya Christiano Ronaldo na Ramos, itakuwa Taifa Stars? Defence imefanya makosa mengi sana ya kujirudia, hadi hatimaye wakafungwa goli wewe ukiwa umekaa tu. Kwa Taifa Stars hii na wachezaji wa Kitanzania kwa ujumla subiri majanga zaidi kama utaendelea na utamaduni huo. Wanahitaji kukumbushwa mara kwa mara na wakati mwingine kuwapanga kabisa na hata kufoka. Hakuna kocha yoyote makini ataona walinzi wake wanarudia makosa yaleyale yeye akiwa amekaa ansubiri eti half time!
Sina nia ya kukupangia, lakini hii timu ni yetu sote, so pokea hii feedback. Tukishindwa mwaka huu basi tena