Makosa makubwa ya kiitifaki katika suala la tuzo za miaka 50; je Ikulu watakiri?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makosa makubwa ya kiitifaki katika suala la tuzo za miaka 50; je Ikulu watakiri??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Dec 15, 2011.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,527
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  Katika utawala huu wa awamu ya nne imekuwa si jambo la ajabu tena kwa watanzania kusikia kuwa taasisi ya ikulu wamefanya makosa ya kiutendaji......kilichobaki kuwa kigumu sana kwao ikulu kwasasa ni kukiri kuwa kuna wakati wanafanya makosa ya kiutendaji.....hili tumeliona na tunazidi kuliona kila kukicha.......

  Tujikumbushe kidogo......

  • Kuna wakati ikulu(kwa kupitia rais)walitoa gari ya Longido kwenda Loliondo......na baadae kukiri kuwa kweli makosa yalifanyika.
  • Hivi majuzi Jairo na washirika wake kafuja hela ndefu ya umma(na nashangaa kimya juu ya hatma yao!!)........haohao ikulu(kwa kupitia Luanjo)wakatoka mbele ya watanzania na kumsafisha Jairo........mpaka ikaundwa kamati teule ya bunge iliyofichua uharo tele wa Jairo.......pamoja na kuwa rais alimzuia kurudi kazini mpaka kamati imalize kazi......lakini ikulu (kwa kupitia Luanjo) haikuwahi kukiri kuwa walikosea....
  Nimeanza hivi ili kukaribisha mjadala juu ya taasisi ya ikulu kushindwa kuwa tayari kukiri makosa ya kiutendaji mara yanapotokea....hivi majuzi tumeona jinsi ambavyo itifaki imeshindwa kuzingatiwa ipasavyo kwenye suala la utoaji tuzo za heshima ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika yetu isiyokuwepo......

  • Ebu tujiulize.....hivi kweli (hata kwa logic ndogo) inawezekanaje pasiwepo hata kiongozi mmojawapo(majaji wakuu wastaafu) wa muhimili wa mahakama kwenye tuzo???,mengi yamesemwa juu ya kina Malecela,Lowasa na Sitta kutopewa.....hili linaweza kueleweka ......kwani kwenye mihimili yao kuna waliopata tuzo........hili la majaji wakuu kukosa tuzo kwa kweli linaonekana kabisa kuwa kosa la kiitifaki........hapa ikulu wanatakiwa waje na maelezo kwa kweli...........

  Angalizo: Issue hii ya tuzo watu wanaibeza lakini inaweza kuwa mojawapo ya indicator kubwa sana ya matatizo makubwa ya kiutendaji yaliyopo katika taasisi ya ikulu......ikumbukwe kuwa issue hii ime mark anti climax kubwa sana katika maadhimisho haya ya miaka 50 ya uhuru pamoja na kuandaliwa kwa mbwembwe tele na watawala......
   
 2. R

  Rutatinisibwa Senior Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  hoja zako ni nzuri kama ungekuwa umefanya utafiti kidogo kujua kama unayoongea ni kweli maana kuna sehemu unakili kuwa HUKUSIKILIZA (kwa maana nyingine huna uhakika na unachokiandika), sasa kama hivyo ndivyo mbona unaanza kulaumu kabla ya kujua ukweli ulivyo! mm nafikiri kwa kuwa ili jukwaa ni chombo muhimu cha kuelimisha jamii ni vyema post zifanyiwe kazi kwanza ili kuondoa maswali mengi yasiyo na msingi!
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  hivi huu ni utawala wa awamu ya pili au ya nne?? nipeni jibu tafadhali!!
   
 4. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuzo anayopewa Anna Makinda hastahili kupewa mtu wa maana. Huu ni muendelezo wa ufisadi na ubinafsi unaowapumbaza wakuu wetu wa nchi. Hawana la kujivunia wanabakia kupeana matuzo feki.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hivi tuzo na nishan ni sawa?
   
 6. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa namna ile ile Mh.Dokta alivyopata nishani ya Udaktari ndio ametoa nishani hizi kwa wenzake ambao na yeye anaona wana vigezo kama vile yeye alivyokuwa navyo mpk leo hii amekuwa Mh. Dokta. Sidhani kama zinahusiana na competency ya mtu, and that is why hata Mh. Mama asiyejua kuwa Dodoma hawaishi wabunge peke yao amepewa moja.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hii nchi sasa inaendeshwa kisegemnege, si katika suala hili la tuzo tu, bali uongozi wa nchi kwa ujumla wake, hali ni mbaya sana
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  With no research, you have no right to speak.... naungana na wewe, mleta mada akajipange upya.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Anazungumzia awamu ya pili ..... hii ilikuwa ni ya mzee ruksa. Lakini mbona mambo yaliyomo ni ya juzi.... japo nazo hazikuwa tuzo... zilikuwa nishani. Nina mashaka na uelewa wako NDERI - NGOSHA. Hebu rekebisha bana ili tutoe michango ya kukuelimisha.
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wakuu wa JWTZ wastaafu walipewa isipokuwa George Waitara pekee. Sababu zinaeleweka hata kabla ya kunyimwa. Wale wazee 17 waliotajwa ndio walionishangaza zaidi. Walipaswa kukumbukwa tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka 2004 ambapo TANU ilitimiza miaka 50.
   
 11. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,527
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  One of a big problems with tanzanians like you,OSOKONI,Rutasinibwa and VGL.. is that....you always give simple answers to big issues.(just like your president).....that's why the only problem you see is a petty issue of time difference in tz leadership and 'tuzo not nishani issue' in this thread.....only these are of concern to you as tanzanians......(ignoring the bigger picture..)......what a bunch of ignorants you are eh!!!........
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Speaker Ana Makinda Samamba aka mama kiroborobo anaweza kufua dafu kwa Chifu Adam Sapi Mkwawa aliyekuwa speaker wa bunge letu kwa miongo kadhaa hadi alipostaafu? Kwa nini Kikwete anakumbatia sana mama kiroborobo? Hayati Adam Sapi hakustahiili tuzo? Edwin Mtei aliyetetea mfumo wa kiuchumi tulio nao sasa enzi za Nyerere hakustahili? Licha ya majaji hao kuna wengine wengi tu waliostahili na badala yake amewapa tuzo waliohujumu nchi kama akina Nzee Nkapa.
   
 13. D

  Deo JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,191
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kwanza tujiulize kwanini walifanya kisirisiri?

  Tuzo hilo lilitakiwa litolewe pale uwanjani mbele ya kadamnasi ya watanzania wote.
   
 14. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Sio ili awe mpole kwenye hoja kali zenye kuidhalilisha serikali? Aitetee bungeni.
   
 15. P

  Panda Kapesi JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 284
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Swala la tuzo ya kutukuka kltaifa lilitakiwa liwe la kitaifa na lishirikishe wananchi katika mchahakato wake sio watu wachache wajifungie maliwatoni na kuchaguana kwa sifa za nani ana sushuzi wenye harufu mbaya zaidi na nani mwenye kikwapa kinachochefua zaidi. Kigezo cka utukuka wao kilitakiwa kiwe utumishi wao kwa wananchi na ilitakiwa iangalie nyanja zote hata ikiwa na viongozi wa dini na hata watu wa kawaida wa mtaani. Wapo watu wa kawaida kabisa mitaani na vijijini ambao wamefanyia mengi kwa taifa hili ambao wanastahili kukumbukwa kwa nini wachaguane wao tu?
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Unategemea nini kama orodha ya wapewa tuzo iilitayarishwa na Salva Rweyemamu na Premy Kibanga?
   
 17. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pumba.
   
 18. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,527
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  u'r ass
   
 19. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Napata taabu kuelewa unapoandika kwenye Ttle "Makosa makubwa ya kiitifaki..." Halafu ndani ya uzi ukaeleza vitu tofauti. Hebu anza kwa kufafanua maana ya neno Itifaki kama ulivyolitumia hapo. Au limekupendeza tu?
   
 20. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapa sina cha kuchangia
   
Loading...