Elections 2015 Makosa makubwa waliofanya Wapinzani baada ya Uchaguzi Mkuu 2015

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,988
Sehemu ya kwanza

03.11.2019


Kutoka nje wakati Rais wa jamhuri wa Muungano anahutubia bunge kwa mara ya kwanza hii ilikuwa ni dharau kubwa kwa Kiongozi wa Nchi. Bahati mbaya walikuwa wanatikisa kiberiti huku hawajui namna ya kuzima. Unamfanyia dharau kiongozi wa Nchi Halafu bado unarudi unaomba siasa za kistaarabu! How? Mbona nyie hamkuonyesha ustaarabu mlipotakiwa kuonyesha ustaarabu?

Kuita utendaji wa Rais ni nguvu ya soda. Rais alipoingia madarakani kila hatua alizokuwa akichukua Rais Magufuli wapinzani walikuwa wakibeza kwa dharau kubwa mno ati ni nguvu ya soda. Hapa kwa wabunge wenye maarifa na wenye kuona mbali wangeunga mkono juhudi za Rais, wangemkosoa baada ya kushindwa.

Kubeza Serikali kuhamia Dodoma. Wabunge Wengi walisikika wakimdhihaki Rais kwamba wao hawawezi wakahamia Dodoma watabaki Dar es Salaam, kana kwamba Dodoma hapafai kuishi watu.

Kumwita Rais dikteta huku wakijua sio Kweli, unashangaa mbunge anaita waandishi wa Habari kwa ajili ya kumtukana Rais. Mara Rais dikteta, mara Rais hivi ila ukiangalia Hakuna logical kabisa. Wabunge wenye akili wangekaa chini kuangalia namna gani ya kufanya kazi na Rais mwenye itikadi za uzalendo badala ya kumtukana majukwaani.

Nimefatilia Wabunge wengi duniani sijawahi kuona mbunge anaitisha mkutano kwa ajili ya kumtukana Rais. Hata huko Marekani wanakosema Ndio kitovu cha demokrasia Sijawahi kuona mbunge anamtukana Rais. Nenda Urusi huwezi kusikia mbunge anamtukana Rais. Ila baadhi ya wabunge wa upinzani Tanzania walitaka walifanye hili ni jambo la kawaida.

Wapinzani kupinga maendeleo. Hawa jamaa walikuwa wanasema inakuaje Nchi kubwa kama Tanzania inakosa shirika la ndege wakati Rwanda Nchi dogo inamiliki shirika la ndege. Sasa hivi wanasema ndege za kazi Gani!

Walikuwa wanakesha bungeni kupigia kelele ufisadi na mafisadi. Baada ya Magufuli kuanza kuyashughulikia mafisadi sasa wamebadilika wanasema mafisadi wanateseka mno kukaa gerezani.

Walilamikia madawa ya kulevya yanavyoharibu vijana ila baada ya wauza madawa ya kulevya kuanza kushughulikiwa wakaanza kuwatetea.

Nakumbuka kabla ya 2015 ilikuwa kila baada ya hatua kadhaa unakutana na teja linadondosha mate au linasinzia barabarani lakini Sasa hivi sio rahisi unaweza kukaa hata mwezi bila kukumbana na teja.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja, rais alishajibu hoja ya kuitwa yeye diktekta?

Rais Magufuli Ni Mwanademokrasia,Ndio maana ameitisha Uchaguzi wa Serkali za Mitaa

Sio kila ujinga unaoibuliwa dhidi ya Rais unatakiwa kujibiwa mengine unayapuuzia tu
tuwe na adabu na heshima kwa viongozi wetu la sivyo tutaishia kwenye mikono ya sheria.
 
Manunuzi ya ndege yalipitishwa na bunge?

CAG anafahamu ni kiasi gani kimetumika katika manunuzi haya?


Kwahiyo wewe unajua zaidi kuliko CAG?

Mbona yeye hajawahi kulalamika

Tuache kumlisha CAG uwongo usiokuwepo

Ndege zimenunuliwa kwa kufuata taratibu
 
Hutaki aitwe dikteta?
Kaangalie series moja inaitwa Jack Ryan Season 2 ipo amazon primevideo utaona jinsi rais wa Venezuela alivyo na tabia sawa na Rais Magufuli. Mbele ya watu anaonekana mwema sana, anafukuza so called mabeberu, ila nyuma ya pazia anateka watu wanaompinga anawaweka kwenye prison camp flani msituni au wengine wanauawa. Alafu rudi jiulize akina Ben Saanane wako wapi au Lissu alifanywa nini. Na tabia za kupondea foreign investors hata wasiohusika ili kujionyesha kuwa kazi kweli inafanyika.

Jamaa anajua sana kuwacheseshea show coz anajua Watanzania wengi vilaza na washika dini mno, so akinunua ndege kibao ambazo zinaingiza hasara mnafurahi mno. Halafu ambao hawafurahi anaenda tu kanisani na camera kibao kuonyesha akiimba na kubeba kikapu anakusanya sadaka anashika karibia watu wa dini wote coz anaonekana mcha Mungu,

waliobaki anajifanya kufukuzafukuza na kucharukia makampuni alafu anafukuza anaweka kampuni zilizo chini ya majina ya ndugu zake hela zote anapiga. Ila watanzania hamjui. Mnachezeshewa show tu daily mnafurahi mnamuona malaika safi kabisa.
 
Vyote vifanyike swadakta lakini vifuate kanuni na taratibu za manunuzi na CAG apate taarifa.Tunahitaji barabara, maji, hospitali, Treni, Ndege na mazingira mazuri ya biashara na Kilimo.
 
Rais Magufuli Ni mwanademokrasia,Ndio maana ameitisha Uchaguzi wa serkali za mitaa

Sio kila ujinga unaoibuliwa dhidi ya Rais unatakiwa kujibiwa mengine unayapuuzia tu
Tuwe na adabu na heshima kwa viongozi wetu la sivyo tutaishia kwenye mikono ya sheria
Hapa ndio patamu hapa. Katiba si kipaumbele chetu, Mimi ndio nimepiga marufuku bunge live lakini kila nifanyalo munirushe live wananchi wangu waone. Hakuna mikutano ya hadhara isiyo ya kibunge nje ya jimbo la mbunge, wala maandamano hata kama katiba na sheria vinaruhusu-lakini mimi kwa sababu nimechaguliwa na watanzania wote basi nitakuwa na mikutano ya hadhara nchi nzima na kwenye mikutano hiyo nitasema maendeleo hayana chama. Hapo hapo nitawaambia wale waliochagua vyama vingine wamekosea na wasiniombe miradi. etc etc. Hivi mkuu kwa nini unataka kutufanya sisi mafala? Inapokuja kwenye demokrasia na utawala bora jamaa yetu ni dhaifu.
 
Rais Magufuli Ni Mwanademokrasia,Ndio maana ameitisha Uchaguzi wa Serkali za Mitaa

Sio kila ujinga unaoibuliwa dhidi ya Rais unatakiwa kujibiwa mengine unayapuuzia tu
tuwe na adabu na heshima kwa viongozi wetu la sivyo tutaishia kwenye mikono ya sheria.

Inaonekana kwako rais ni sheria na kwa haraka zaidi ni Mungu. Rais alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi, je jeshi lina mahusiano na siasa kikatiba? Je ni hatua gani ya kisheria alichukuliwa rais kwa kuvunja katiba kwa kuingiza siasa ndani ya jeshi?
 
Rais Magufuli Ni Mwanademokrasia,Ndio maana ameitisha Uchaguzi wa Serkali za Mitaa

Sio kila ujinga unaoibuliwa dhidi ya Rais unatakiwa kujibiwa mengine unayapuuzia tu
tuwe na adabu na heshima kwa viongozi wetu la sivyo tutaishia kwenye mikono ya sheria.

Demokrasia sio kuitisha uchaguzi tu, bali ni kutii sheria na kanuni za huo uchaguzi. Huenda hujui demokrasia ni nini ndio maana unatapika tu hapa kama shehe aliyekula kitimoto.
 
Mi Nadhani wapinzani wamekosa uzalendo
Wameamua kutanguliza matumbo mbele kwa kutumika na Mabeberu
 
Back
Top Bottom