Makosa makubwa kutengua matokeo ya Ubunge kwa ushahidi wa kusikia-Jaji Moses

Ficha upumbavu wako na onyesha hekima yako

Tafuta sababu za kutupwa kesi ya Ally Mley mgombea ubunge CHADEMA kigoma Mjini na ndio utaelewa kati ya mimi na wewe nani mpumbavu.

Bora mjinga kama hajui anasema hajui na kujifunza, wakati mpumbavu anajifanya anajua huku hajui.
 
Tafuta sababu za kutupwa kesi ya Ally Mley mgombea ubunge CHADEMA kigoma Mjini na ndio utaelewa kati ya mimi na wewe nani mpumbavu.

Bora mjinga kama hajui anasema hajui na kujifunza, wakati mpumbavu anajifanya anajua huku hajui.

Hela unayolipwa kutetea upuuzi hapa JF ndio kitanzi chako wananchi watakapokombolewa.
 
Hivi majaji km huyu wanafika 10 tz?.....ingekuwa hivyo basi ccm ingenyooka na isingesubiri rungu la mahakama kuiadhibu cdm.......mungu mkubwa kwenye msafara wa mamba na kenge wamo pia

Huyu ni mwana Kamanda
 
Mkuu kusikia tu bila vielelezo vya ulichosikia tutaamini vipi?

Mkuu hebu nisaidie: Hivi X akimtukana Y na mashahidi A, B, na C walikuwepo kwenye tukio hakuna kesi hapo? Ni vielelezo gani tena vinatakiwa zaidi ya ushahidi wao? Picha labda?

Kama walisikia wao wenyewe kwa vyovyote ushahidi wao utakuwa consistent; na consistence kwenye ushahidi ndicho kilelezo namba moja.

Vinginevyo kama ni ushahidi wa "kuambiwa", "kutunga", au "kufundishwa" ni lazima watajipinga wenyewe.
 
Si likuwa hamna imani na ahakama nyinyi? vipi? kumbuka, huu ni wakati wa Kikwete, haonewi mtu. Lema kachuma alichokipanda kwa ushahidi kamili na Lissu nae achunge sana, asifate maneno ya watu ambao hawajenda shule kama Lema, yatampeleka pabaya, mwenzake yule ana profession nyingine kwa hiyo hana wasiwasi, wewe Lissu unaetegemea kazi za kuhukumiwa kwanza siku ya siku, inabidi uchunge sana nyendo zako.
 
Hongera na asante sana mh: Jaji Moses.Wanabodi tusibweteke kwa lolote mahakama zetu (nyingi) na kwa sehemu kubwa ni mbovu na hazitendi haki. Hili la Lissu na Jaji Moses ni kitu cha nadra kutoka mhimili dhailfu wa dola uitwao mahakama.Nampongeza sana mh Jaji Moses kwa uwezo na juhudi zake binafsi za kusimamia maadili ya taaluma yake na kutenda haki ktk mazingira magumu haya lakini yenye uhitaji mkubwa wa watu wa haiba yake. Be blessed Judge Moses
 
Hongera na asante sana mh: Jaji Moses.Wanabodi tusibweteke kwa lolote mahakama zetu (nyingi) na kwa sehemu kubwa ni mbovu na hazitendi haki. Hili la Lissu na Jaji Moses ni kitu cha nadra kutoka mhimili dhailfu wa dola uitwao mahakama.Nampongeza sana mh Jaji Moses kwa uwezo na juhudi zake binafsi za kusimamia maadili ya taaluma yake na kutenda haki ktk mazingira magumu haya lakini yenye uhitaji mkubwa wa watu wa haiba yake. Be blessed Judge Moses

Well said mkuu
 
jaji anayesikiliza na atakayehukumu kesi ya Mpendazoe(CDM) dhidi ya Dr.Mahanga(CCM)
tarehe 02/05/2012 anaitwa nani?
 
hawa ndiyo majaji tunao wahitaji wenye weledi wa kweli na kazi zao,,,,,,,,,,,,,,,,,,jaji huyu anastahili kuwa jaji mkuu wa nchi hii ili arudishe hadhi ya mahakama. congrats kwa ujasiri huo mungu akulinde kwa kutenda haki.
 
hawa ndiyo majaji tunao wahitaji wenye weledi wa kweli na kazi zao,,,,,,,,,,,,,,,,,,jaji huyu anastahili kuwa jaji mkuu wa nchi hii ili arudishe hadhi ya mahakama. congrats kwa ujasiri huo mungu akulinde kwa kutenda haki.

Wakuu muwe pia makini kwenye kutoa pongezi maana magamba ni wivu kinoma! Wana donge la kufa mtu hawakawii kufanya mambo ya ajabu kama mlivyosikia huko Usa River. Otherwise, Mungu amlinde.
 
hawa ndiyo majaji tunao wahitaji wenye weledi wa kweli na kazi zao,,,,,,,,,,,,,,,,,,jaji huyu anastahili kuwa jaji mkuu wa nchi hii ili arudishe hadhi ya mahakama. congrats kwa ujasiri huo mungu akulinde kwa kutenda haki.

Naunga mkono hoja %100.
 

wakuu muwe pia makini kwenye kutoa pongezi maana magamba ni wivu kinoma! Wana donge la kufa mtu hawakawii kufanya mambo ya ajabu kama mlivyosikia huko usa river. Otherwise, mungu amlinde.
usijali ndugu kwani wataua wangapi? Damu inayomwajika haitamwajika bure lazima italipwa,,,,,,,,,,,,,,,mungu yu pamoja nasi makamanda tusikate tamaa.........
 
isijekuwa sababu hizi zinaandaliwa kwa matumizi ya segerea, sumbawanga, kigoma ..
 
Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia bila kutoa vielelezo dhahiri vunavyoonyesha tukio husika.

Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.

Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika.


Source:Mwananchi Jumamosi

mkuu molemo,
naikubali thread yako ila kwa mimi mwanafunzi wa law ndo napata exp through mambo km haya. rekebisha heading kwenye neno jaji moses, andika jaji mzuna j, sbb hilo ndo official, ili wadau wengine wasiofuatilia mambo wajue ni jaji yupi aliyetoa hukumu. moses wengi.
 
HONGERA IDARA YA MAHAKAMA KUJIREJESHEA JAPO KA-THELUTHI YA HESHIMA KWA UMMA WA TANZANIA KUPITIA KWA JAJI MUSA MZUNA KULE SINGIDA:

Hakika nchi hii laiti tungekua na wanasheria mahiri na wenye FIKRA HURU, walau 10 tu, ambao ni fanania yake huyu Jaji Musa Mzuna wa Singida na wengine kama yule Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, ki-ukweli Tanzania hii hata sisi MASIKINI japo kidogo tu tungebahatika kuelewa NINI MAANA YA HAKI inayoelekezwa na Katiba yetu kuwa itolewe Mahakamani.

Kwa mtaji wa kile kilichotokea Singida na kuiletea Heshima Kuu Idara ya Mahakama machoni mwetu Umma wa Tanzania, kinyume kabisa na hukumu ya Arusha iliocha uchachu hata katika midomo yaa wataalaam wenyewe wa sheria ndani ya nchi hii, napenda nitoe rai yangu kwenu wakubwa zetu kwamba ENYI WAJUMBE MLIOTUKUKA 'KAMATI KAMATI YA KATIBA', KATIBA MPYA IJAYO ITAFUTE KUREJESHA (1) HAKI, HESHMA NA UTU WA MTANZANIA WA KAWAIDA, (2) ULINZI IMARA WA RASILMALI ZA TAIFA, NA (3) KUWEKA NJIA KIBAO ZA UWAJIBIKAJI KATIKA KILA NGAZI YA UTAWALA .

Hakika kwa walalahoi tuliowengi, wala si jambo la huzuni tena kwetu sisi kutokufahamu nini maana halisi ya HAKI KWA WOTE MAHAKAMANI; ukweli ni kwamba wengi tumefika mahali tunajionea tu jambo la kawaida kwa bidhaa hii ya 'HAKI MAHAKAMANI' kuwani miliki yao tu (1) WaTanzania wachache wenye VIJISENTI pamoja na (2) tabaka dogo la watawala, ndugu na marafiki zao.

Kwangu mie, ushindi wa Mhe Tundu Lissu kule Singida ni sawa tu na kusema ni USHINDI KWA IDARA YA MAHAKAMA kujichagulia, kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi saana, KUJIRUDISHIA JAAPO KA-CHEMBE CHA HESHIMA tuliobaki nayo akina kabwela wa nchi hii.

Naam, ni matumaaini yangu kwamba safari hii hawajafanya kazi zao kwa maelekezo ya simu kutoka Magogoni ya kujitafutia umwamba na kukomoana na mwisho wa siku kujikuta tuliokomolewa zaidi ni wapiga kura na wala si Mbunge mlengwa wa hila zote hizo.

Kwa kuhitimisha tu, kutokana na somo tunayoipata kutoka katika Mahakama zetu za Arusha, Singida na ukweli juu ya jinsi gani 'HAKI MAHAKAMANI' ilivyogeuka kuwa ni msamiati mgumu ajabu kwa WaTanzania masikini ambao ni zaidi ya asilimia 80% ya watu wote hapa nchini, ni wazi kwamba huyu Jaji Musa Mzuna kaatushangaza mno kwa ujasiri wake wa aina yake, baada ya miaka mingi sisi kutofahamu kitu haki nje ya vile waonavyo waatawala, kwa kutoa hukumu unaoegemea weledi wake tu na wala si vinginevyo!!

Kutokna na mshangao huo aliotupiga nayo huyu Mtanzania mwenzetu, nje kabisa ya mazoea tulivyokua tukiyasubiria, napenda nichukue fursa hii nikatume SALAMU ZENYE UPEKEE kwa magwiji wa sheria mnaoheshimika sana nchini na tena kubahatika kuingia katika Tume ya Katiba ya nchi yetu (Mzee Jaji Sinde Warioba, Mzee Jaji Augustino Ramadhani, Prof Mwesiga Baregu, Dr Sengondo Mvungi,na Mhe Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar) kwamba fanyeni yote juu ya yote kuunda katiba mpya ya nchi yetu kwa KUTUFANYA SISI WANANCHI WA KAWAIDA MITAANI NDIO TUWE KWELI ndio wenye nchi Kiutawala na maamuzi yote muhimu na wala si tu wana wa nchi tunaosukumwa kiholelaholela na watawala wachache na wenye hela.

Ndio, nasema mnalo jukumu lisilokwepeka Mzee Warioba wa kutufanya katika hiyo KATIBA MPYA, sisi tujihisi, kuonekana na kusomeka 'WAFALME NA WENYE USEMI WA MWISHO JUU YA MAMBO KIBAO yenye mustakabali mzima wa nchi yetu BILA KUWEKA REHANI MATUMAINI YETU YA BAADAYE KAMA NCHI mikononi mwao watawala wachache' kwa kutegemea eti siku gani watakua wameamka vipi au wake zao watakua wamefurahi au wamenuna.

Ndio, kwa hao vingunge wa sheria tunaowaheshimu sana nchini
(bila kusahau Prof Shivji, Jaji Bomani, Tundu Lissu na Prof Peter Maina), nasema KATIBA MPYA haitokua na maana yoyote kwangu mpaka pale ambapo FARAJA YANGU ITAKAMILIKA TU PALE AMBAPO LENGO KUU YA KUWEKA CHECKS AND BALANCES KIBAO YENYE LENGO LA KUFANYA bidhaa hii adimu ya 'HAKI MAHAKAMANI' kuwa ni bidhaa inayoweza ikapatikana hata kwa Mzee Matonya tu Barabarani dhidi ya Mzee Makamba katika ofisi ya Ukuu wa Mkoa - Bila kuingiliwa hata kidogo na 'Tawi la Pili la Kutoa HAKI MAHAKAMANI kupitia simu na vi-memo kutoka Magogoni.

Kwa lugha rahisi tu, ukitaka kuelewa ninachosema hapa ni kwamba jiulize kama haitokua
KICHEKESHO CHA KARNE kusikia eti Mzee Matonya kampeleka mahakamani yule Mzee Makamba kwa madai ya kuingilia uhuru wake wa kikatiba kutembelea popote, kukaa popote na kufanya shughuli zake popote BILA KUBUGHUDHIWA na mtu wala chombo chochote ILMRADI HAVUNJI SHERIA?

Kesi kama hii, kwa misingi ya Katiba ya sasa na mfumo uliopo, wala sio siri kwamba WaTanzania tunaweza hata tukakuambia kwamba hukumu itatoka vipi hata kabla kesi haijaanza. Ni kero, unafiki, na uzabizabina (Rweyemamu et al, 2011 - Kurugenzi za Mawasiliano Magogoni) endapo safari hii mtaendelea tena kuifanya Sheria na Katiba zote ziwe ni vyombo vinavyompendelea MHESHIMIWA MTAWALA pamoja na yule mwingine mwenye 'enzi' yote MHESHIMIWA MWENYE PESA.

Napenda nikuhakikishieni kwamba endapo kutazaliwa tena KATIBA isiompa UKUU MWANANCHI WA KAWAIDA ambaye ndiye uhalali wote wa kutawala inakamiswa kutoka kwetu, basi ninaweza kuwahakikishieni kwamba mnaweza kunihesabu mapema kuwa mstari wa mbele sana tu katika kutumia ushawishi wangu wote (UWEZO TUNAO) kuhakikisha kwamba marudio ya UDHALIMU NDANI YA KATIBA tunauangusha kwenye kura ya maoni bila ajizi.

Jaji Moses Mzuna aliyetupilia mbali kesi dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema ni makosa makubwa kwa mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi kwa ushahidi wa kusikia bila kutoa vielelezo dhahiri vunavyoonyesha tukio husika.

Jaji huyo amesema ili kutengua matokeo ni lazima kuwe na ushahidi ulio wazi tena wa vielelezo visivyotia shaka.Jaji huyo ameendelea kusema ni kosa kubwa kumuondoa kiongozi wa wananchi kwa ushahidi wa hovyo hovyo.

Jaji huyo pia amesema wanaofungua kesi za uchaguzi wanapaswa kujua kesi za kupinga matokeo si za mchezo mchezo.

Amesema kwa njia hii ndipo mahakama zetu zitakapoheshimika.


Source:Mwananchi Jumamosi
 
Back
Top Bottom