Makosa makubwa haya: Werema aitwisha CCM 'mzigo' wa mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makosa makubwa haya: Werema aitwisha CCM 'mzigo' wa mafuta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Jul 3, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jul 3, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Frederick Werema amesema suala la kuyaondoa mambo ya mafuta kwenye muungano ni lazima lianzie ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa ndicho chenye Serikali inayotawala kwa sasa.

  Werema amesema, suala hilo litaanzia kwenye chama hicho kwa vile ni suala la sera, hivyo akasema hata kama kuna makubaliano ya marais Jakaya Kikwete na Amani Abeid Karume wa Zanzibar ni lazima suala hilo lipitie katika chama chao.


  “Hapo ndipo mchakato utakapoanzia kabla ya kufikishwa bungeni,” amesema Werema wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jang’ombe, Mohamed Rajab Soud (CCM).


  Mbunge huyo alitaka kufahamu kwa kuwa tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ilishatoa tamko lake katika Baraza la Wawakilishi ni lini Serikali ya Muungano itatoa tamko lake kuhusu suala hilo la mafuta.


  Werema amesema,utaratibu huo alioueleza ndiyo ambao watanzania wamejiwekea bila kutegemea ukubwa wa kambare na sharubu zake.


  Awali Mbunge wa Dimani, Hafidh Ali Tahir (CCM) alihoji kama matamshi ya Rais Karume aliyoyatoa kwenye sherehe za mapinduzi huko visiwani kuwa wamekubaliana na Rais Kikwete suala hilo la mafuta liondolewe kwenye Muungano kama kauli hiyo haikiuki Katiba ya nchi.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mohamed Seif Khatib, amesema, kwa mujibu wa Katiba,wote hao wanasema tu, kwa kuwa suala hilo lazima liende bungeni na si kuamriwa na viongozi wa juu wa nchi.


  Akijibu swali la msingi la Mbunge huyo, Khatib alisema Serikali inatambua kuwa suala la mafuta na petroli bado ni la Muungano hadi itakapoamuliwa vinginevyo.


  Amesema, kiutaratibu Muungano huu ni wa ubia na wa hiyari linalotakiwa kufanyika ni kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuiandikia Serikali ya muungano rasmi kuonesha dhamira ya kuliondoa jambo hilo katika orodha ya mambo ya muungano.


  Khatib amesema, iwapo Serikali ya Muungano itaafiki, itabidi jambo hilo lipelekwe bungeni ili watoe baraka zao kwa kura kwa mujibu wa taratibu.


  “Endapo wabunge wa pande zote watakubali kila upande theluthi mbili yake jambo hilo litandolewa katika orodha ya mambo ya Muungano,” alisema Khatib.


  Kwa muda sasa, suala la mafuta ambayo hata hivyo hayajapatikana, limeibua malumbano hasa kwa upande wa Zanzibar unaotaka endapo nishati hiyo itapatikana, iwe mali ya Zanzibar pekee, na kamwe yasiingizwe katika masuala ya Muungano.


  My Take:
  Tanzania bado tuna njia ndefu sana kama hata mwanasheria Mkuu wa serikali naye anasukumiza mambo ya serikali yakaamuliwe na vikao vya CCM ambavyo siamini kuwa vinatambuliwa na katiba ya nchi.

  Hi ni dalili ya ushabiki wa kisiasa unaofanywa na mwanasheria mkuu.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hakuna ha mwanasheria wa serikali kwa CCM.....kila kitu ni siasa ndo maana hata issue ya mgombea binafsi imekuwa handled kisiasa.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Jul 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kichuguu,
  The all statement ya mwanasheria mkuu, ni sawa na kuwa - Wapo watu au chombo ambacho ni Above the LAW!
   
 4. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kule Zenji nako kuna Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Karume ambae anashindwa kumshauri ipasavyo Karume katika hili suala na Werema hali kadhalika hawezi kumsahuri ipasavyo JK kwenye suala hili kwa upande wa Bara (Serikali ya Muungano).

  Karume hawezi kusimami akasema wamezungumza na JK kana kwamba jambo hili la kikatiba ni suala la kutolewa maamuzi kirahisi kihivyo na hawa wakulu (JK- Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano na Karume - M/Mwenyekiti wa CCM na Rais wa SMZ). Kama Werema anasema chama ndio Serikali, kwa Upande inamaanisha yeye kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mwanasheria Mkuu pia wa CCM. Hivyo hawezi kulitupa suala hili kwa CCM kana kwamba pale alipo hatekelezi ilani ya CCM.
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Mijitu yenyewe si iliteuliwa ili ilinnde maslahi fisadi ya chama?
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Jul 3, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,768
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..Jaji Werema aache ubabaishaji. suala hili lilipofikia halihitaji kupitia kwenye chama.

  ..labda wanaogopa, kwasababu tuko karibu na uchaguzi, mambo yatakayoibuka ktk mjadala wa kupitisha mswada wa kuondoa mafuta kwenye masuala ya muungano. they may end up opening a can of worms
   
 7. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  That's their destination!
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kiboko wa sakata hili ni MAALIM Seif SHARRIF HAMADI ,hatuna mwengine ambae anaweza kulimaliza tena kiurahisi kabisa ,kwa hawa wa Chama Cha Mafisadi kila siku itakuwa kusukumiziana kila mmoja anamsogezea mwenziwe na mwengine huchokonoa ,akijua kuna wenzao wataganda na kuumbuana.

  Yaani uyo kibaka atamjua ni nani Kambale mwenye Shakubu kubwa.
   
 9. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  halafu mafuta mengi yanaweza kuwepo bongo kuliko Zenj
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu Mwiba, yaani bado tu hujakata tamaa na huyu jamaa, kweli imani sio mchezo, ukiweka imani kwa mtu hata ukiambiwa sio wewe huwezi amini, huyo bwana hakuna kitu wamebakia kuchukua fedha za RA tu, na juzi wamepewa gari mpya pale nzega
   
 11. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #11
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  He is not 100%, wrong by the way!!
   
 12. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwamlaumu huyu mwanazuoni bila ya sababu za msingi. Muungano wetu uko kisiasa zaidi kuliko kiserikali ndio maana hata siku moja hujawahi sikia wana CCM wa Visiwani wanatofautiana na wana CCM wa Bara (mwanasheria/wakili mkuu wa CCM ni mmoja!). Tatizo linakuja pale tunapoanza kuzungumzia mambo ya kiserikali (mf., mafuta, ushuru n.k.).

  Mytake:
  Ili muungano uwe thabiti inatakiwa tuungane kwa kila kitu sio wizara nne tu zilizopo kwa sasa. Status ya ZNZ inachanganya wengi kwa sasa maana haijulikani kama ni province, state au a country.

  Ni ka-mtego!!
   
 13. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  kamkoa tu aisee!
   
 14. Dx and Rx

  Dx and Rx JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2017
  Joined: Jul 16, 2017
  Messages: 873
  Likes Received: 2,309
  Trophy Points: 180
  Nakuona unanyapia nyapia makombora ya humu jamvini, Mshauri mkulu kama ulivyokuwa unafanya kipindi bado hujakaribishwa keti ya Taifa, usiache Taifa liangamie kisa wewe ushapata cha kuingiza kinywani
   
 15. Mwifwa

  Mwifwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2017
  Joined: Apr 3, 2017
  Messages: 15,213
  Likes Received: 36,262
  Trophy Points: 280
  Uzi wa kitambo sana
   
Loading...