Makosa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili, kwanini yanashamiri?

Grahnman

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
1,673
2,000
Habari za asubuhi wana JF?

Kumekuwa na tatizo la kiuandishi kwa watu wengi kuanzia humu JF mpaka kwingineko kote kwenye mitandao ya kijamii mwanzo nilidhani ni kujisahau lakini sasa naona kama imezoeleka na kuonekana kama ni maneno ya kawaida kwenye kiswahili na watu wala hawastuki kuona kama ni makosa,yaani makosa yakirudiwa rudiwa mara nyingi huzoeleka na kuonekana ni usahihi

Naomba nitoe mifano michache ya hayo maneno hapa chini;
Nisamee badala ya Nisamehe
Eshima badala ya Heshima
Asubui badala ya Asubuhi
Mdogo angu badala ya Mdogo wangu
Kiac badala ya kiasi
Awez badala ya Hawezi
Ujaacha badala ya Hujaacha
Uendelei badala ya Huendelei
Utamsikia Mtangazaji anasema Nyimbo hii badala ya kusema wimbo huu

Yako maneno mengi sana yanayopotoshwa na wadau wengi humu ndani,ombi langu tu ndugu zangu tubadilike tuandike maneno kwa usahihi wake kwa sababu humu ndani panapitiwa na wanafunzi kuanzia Shule za Msingi,Sekondari na hata Vyuo wanajifunza nini juu ya tunayoyaandika humu?

Eti hapo ndio tunawadharau Wakenya hawajui Kiswahili hawajui kiswahili wakati sisi wenyewe ndio tunavuruga tu.

Ni hayo tu wadau muwe na Jumapili njema

Asante!
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,154
2,000
Pole na uzalendo, hii nchi elimu elisha haribika sanaa utaumia bure, kama una watoto bora ucheza nao usipoteze mda wako.
 
SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
7,971
2,000
Kweli kabisa Mzee kifimbocheza.

Hayo pia yanaiharibu lugha yetu.
Pia kuna vijimaneno vya wanawake lakini cha ajabu waweza kukuta mtoto wa kiume anayatumia.
 
carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,877
2,000
Mkuu lengo kuu la kuwa na lugha ni kisaidia mawasiliano.
Kwahio basi as long as tukiongea tunaelewana basi hio lugha ni sahihi.

Sisi ni binadamu kwahio kamusi zinatakiwa kutufwata sisi na sio sisi kuzifwata kamusi..
 
pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
3,978
2,000
Wengi sana huchanganya matumizi ya maneno jinsi na jinsia.

Tunapotaka kumaanisha mtu ni "ke" au "me" tunazungumzia jinsi yake. Sio jinsia yake.
 
Tika

Member
Apr 16, 2012
38
95
Mkuu lengo kuu la kuwa na lugha ni kisaidia mawasiliano.
Kwahio basi as long as tukiongea tunaelewana basi hio lugha ni sahihi.

Sisi ni binadamu kwahio kamusi zinatakiwa kutufwata sisi na sio sisi kuzifwata kamusi..
Hio badala ya hiyo.
 
Oct 29, 2018
5
20
Habari za asubuhi wana JF?

Kumekuwa na tatizo la kiuandishi kwa watu wengi kuanzia humu JF mpaka kwingineko kote kwenye mitandao ya kijamii mwanzo nilidhani ni kujisahau lakini sasa naona kama imezoeleka na kuonekana kama ni maneno ya kawaida kwenye kiswahili na watu wala hawastuki kuona kama ni makosa,yaani makosa yakirudiwa rudiwa mara nyingi huzoeleka na kuonekana ni usahihi

Naomba nitoe mifano michache ya hayo maneno hapa chini;
Nisamee badala ya Nisamehe
Eshima badala ya Heshima
Asubui badala ya Asubuhi
Mdogo angu badala ya Mdogo wangu
Kiac badala ya kiasi
Awez badala ya Hawezi
Ujaacha badala ya Hujaacha
Uendelei badala ya Huendelei
Utamsikia Mtangazaji anasema Nyimbo hii badala ya kusema wimbo huu

Yako maneno mengi sana yanayopotoshwa na wadau wengi humu ndani,ombi langu tu ndugu zangu tubadilike tuandike maneno kwa usahihi wake kwa sababu humu ndani panapitiwa na wanafunzi kuanzia Shule za Msingi,Sekondari na hata Vyuo wanajifunza nini juu ya tunayoyaandika humu?

Eti hapo ndio tunawadharau Wakenya hawajui Kiswahili hawajui kiswahili wakati sisi wenyewe ndio tunavuruga tu.

Ni hayo tu wadau muwe na Jumapili njema

Asante!
Hili chimbuko lake limeanzia mashuleni(shule za msingi na sekondari). Mfumo wa elimu haitujengi kuwa wazungumaji wazuri wa lugha ya kiswahili wala lugha ya kiingereza. Hivyo basi watu hawajali kama wanaongea sahihi au laa
 
chagonjam

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
354
500
hizo ni slang mkuu. kuna lugha rasmi, kuna lugha ya mtaani na kwa sasa mitandao ya kijamii imekuja na utamaduni wake wa jinsi ya kuwasiliana. kuna wakati ukisoma ujumbe mfupi wa simu unaweza usielewe utadhani kilichoandikwa si Kiswahili.
 
Anithape

Senior Member
Nov 14, 2018
128
250
Wasukuma wanafika milioni 6 nchi hii, kwahiyo tuwasamehe tuu na kiswahili cha kisukuma.
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,167
2,000
hizo ni slang mkuu. kuna lugha rasmi, kuna lugha ya mtaani na kwa sasa mitandao ya kijamii imekuja na utamaduni wake wa jinsi ya kuwasiliana. kuna wakati ukisoma ujumbe mfupi wa simu unaweza usielewe utadhani kilichoandikwa si Kiswahili.

Kuna mwenzetu mmoja hapa aitwa Faiza Foxy yeye aliamua kujitolea kabisa kurekebisha maneno mabovu kwenye maandishi kutoka kwa baadhi ya wana JF.

Ni tatizo ambalo likiachiwa basi Kiswahili kitapoteza ule ubora wake.

Nikisema ubora namaanisha Kiswahili sanifu na fasaha.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,131
2,000
Kuna maneno kwa kweli yanaudhi, sio tu kuyasikia bali hata kuyasoma!

Halafu kuna neno aghalabu! Neno hili watumiaji wengi wa Kiswahili hupindua tafsiri yake, kutoka mara nyingi na kudhani ni (huzani?) ni mara chache!! Aidha, mara nyingi matumizi ya neno "tegemea" huacha ukakasi mwingi nyuma yake.

Yote tisa, donda ndugu lipo kwenye "r" na "l". Inakera sana kuona mtu anatamka au kuandika "naludi saa tano manake mala kwa mala huo ndio muda wangu wa kuludi kazini!"

Tusisahau pia neno saa linapotamkwa au kuandikwa kwa wingi kwamba masaa! Hapa utakuta hata Waandishi wa Habari wakisema "Waziri Mkuu alihutubia kwa masaa matatu!

Nilisahau! Ingawaje maneno yapo mengi mno kiasi kwamba siwezi kuyataja japo robo yake lakini wacha tu nilizungumzie hili neno "aidha."

Watumiaji wengi wa Kiswahili wanalitumia neno "aidha" kama "either" la Kiingereza, wakati tafsiri ya neno "aidha" ni "vile vile", "pia" au neno lolote lenye tafsiri sawa na hayo. Hivyo basi, badala ya kusema mathalani, "natarajia kuhamishiwa aidha Morogoro au Dodoma", hapo ulitakiwa kusema "natarajia kuhamishiwa ama Morogoro au Dodoma!"

Lakini mleta mada, nawe unatakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya utenganishi wa maneno. Inaleta ukakasi kuona unaandika maneno zaidi ya thelathini na hakuna kituo pahala popote pale kwenye tungo husika.

Kwavile umehusisha matumizi mabaya ya Kiswahili na uandishi, basi pia tukumbushane uandishi sahihi ni pamoja na matumizi sahihi ya utenganishi wa maneno; yaani punctuation.
 
Bakariforever

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
410
500
Hapo umeelezea makosa ya kimaneno, ila pia kuna makosa ya sentensi, mfano nilikwenda nikamkuta hayupo, Juma huwa anakujaga hapa kila siku, bwana harusi alipokelewa kwa matarumbeta, sijampa kwa sababu nilikuwa sina, naomba nikopeshe elfu tano wakati kumbe hitaji la elfu tano unahitaji wewe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom