Makosa ambayo watu wengi hufanya katika kujenga au kujibu hoja humu jukwaani

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,815
11,541
Kupitia mijadala mingi humu jukwaani,nimegundua watu wengi hawajui kujadiliana na mara nyingi hoja zao huwa na makosa,kasoro au upotofu.
Ni tofauti na mijadala ya Quora au reddit inavyoenda.

Kasoro za kimantiki ni makosa yanayotokea wakati hoja au maelezo yanayotolewa hayafuati misingi ya mantiki au yanatumika kwa njia isiyofaa. Makosa haya yanaweza kuongoza kwenye hitimisho lisilo sahihi au kufanya hoja zisizokubalika.

Haya hapa baadhi ya makosa ambayo watu wengi huyafanya,ni vizuri tujifunze ili kuyaepuka

  1. Kukurupuka (Hasty Generalization) - Hii ni kasoro ya kimantiki inayotokea wakati mtu anafanya hitimisho kwa haraka bila ushahidi wa kutosha. Kwa mfano, kusema kwamba wanaume wote ni waongo kwa sababu mmoja alimdanganya rafiki yako. Au wanyaturu ni malaya kwasababu mnyaturu uliyekutana naye alikuwa malaya
  2. Kumshambulia mtoa hoja (Ad Hominem) - Hii ni kasoro ya kimantiki inayotokea wakati badala ya kutoa hoja sahihi, mtu anashambulia tabia ya mtu mwingine. Kwa mfano, kudai kwamba hoja ya mtu haifai kwa sababu mtu huyo ni muongo. Au tusisikilize hoja za zembwela kwakuwa ni mvuta bangi
  3. Kujisahaulisha Hoja (Straw Man) - Hii ni kasoro ya kimantiki inayotokea pale mtu anatengeneza hoja kwa upande mwingine ambayo haipo, kisha kuishambulia hoja hiyo. Kwa mfano: Mtu aseme ‘‘Nampenda Samia kwakuwa amejenga madarasa…’’ halafu mwingine amjibu ‘’weee unamchukia Magufuli tu kwakuwa hakuwa mtu wa pwani’’ Hapo mtu wa kwanza hakusema anamchukia magufuli,ila ametengenezewa hiyo hoja mpya feki na kushambuliwa.
  4. Mzunguko (Circular Reasoning) - Hii ni kasoro ya kimantiki ambapo mtu anatumia hitimisho kama msingi wa hoja. Kwa mfano, kusema kwamba kitu ni sahihi kwa sababu kinapaswa kuwa sahihi. Au kusema Quran ni kitabu cha Mungu kwakuwa ilishushwa kutoka kwa Mungu.
  5. Kupotosha (False Dilemma) - Hii ni kasoro ya kimantiki inayotokea wakati mtu anadai kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kufanya kitu isipokuwa njia mbili zilizopendekezwa, wakati kuna njia nyingine zaidi ya kufanya kitu. Kwa mfano, kudai kwamba unaunga mkono serikali au unapinga taasisi ya serikali. Kama hupingi ushoga basi unasapoti ushoga. Kama hausapoti CCM basi wewe ni mpinzani (unaweza usiwe mpinzani na usiisapoti CCM)
  6. Kasoro ya kutumia hoja ya mamlaka (Appeal to Authority) ni kasoro ya kimantiki ambapo mtu anatumia jina au mamlaka ya mtu au kikundi cha watu au kitabu flani ili kujaribu kuthibitisha hoja yake, badala ya kutumia ushahidi wa kutosha. Hii inaweza kuwa ni kosa kwa sababu hata wataalamu na watu wenye mamlaka wanaweza kufanya makosa na kuwa na maoni yasiyofaa..mfano Kuoa mtoto wa miaka 6 ni sawa kwasababu kitabu flani kimesema
  7. Kasoro ya Red Herring (Kasoro ya Kipepeo) ni kasoro ya kimantiki ambapo mtu anapotosha au kuelekeza mazungumzo katika mwelekeo tofauti na suala kuu la mjadala kwa lengo la kujaribu kuepuka hoja ngumu au kutafuta njia ya kushawishi watu kufikiria kwa njia fulani tofauti.
    Kwa mfano, katika mjadala wa kisiasa kuhusu sera za afya, mmoja wa wanasiasa anaweza kuanza kuzungumzia jinsi alivyochangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya sekta ya elimu wakati huo huo akiacha kuzungumzia suala la sera za afya. Hii ni mfano wa kasoro ya Red Herring, kwa sababu anajaribu kuelekeza mazungumzo kwenye suala tofauti na linalojadiliwa ili kuepuka hoja ngumu au kutafuta njia ya kushawishi watu kufikiria kwa njia fulani.
  8. Kasoro ya "Slippery Slope" ni kasoro ya kimantiki ambayo inajumuisha kutumia hoja ya kufikiria kwamba ikiwa kitendo kimoja kitafanyika, basi hatimaye kitasababisha athari mbaya zaidi zinazoendelea kutokea bila kuthibitisha hoja hii kwa ushahidi wa kutosha. Kwa maneno mengine, mtu anasema kwamba jambo moja litasababisha jambo baya zaidi kutokea bila sababu halisi.

    Kwa mfano, mtu anaweza kudai kwamba kama bangi itaruhusiwa basi kila mtu ataanza kuivuta na watu wataacha kufanya kazi ili wavute bangi. Hapo ni kasoro kwakuwa hakuna ushahidi kuwa bangi ikiruhusiwa kila mtu ataivuta.

    Kasoro ya "Slippery Slope" inaweza kutumiwa kwa kusudi la kuogopesha watu au kuwashawishi watu kufikiria kwa njia fulani. Ni muhimu kuzingatia ushahidi wa kutosha na kutafuta sababu halisi za athari zinazoweza kutokea badala ya kuamini hoja hii isiyo na msingi
 
Ulichofanikiwa ni kupachika vineno vya kingereza ilimradi uhadae raia waone umeandika vitu vya maana kumbe ni pumba 90%
Elezea basi, sio kuishia kusema pumba tu bila hoja yoyote… ni ombi lakini
 
Utakufa kabla ya siku zako wewe... (Nimeapply hoja namba 1 na 2)

Mapema tu nimekugundua lengo lako kwenye hoja namba 4 na 6. Kwa bahati mbaya humchafui mtu utajichafia mwenyewe
 
Kazi kwerikweri.....

Ili watu wayatambue makosa ya kimantiki inabidi wawe watu wa mantiki to begin with.
 
Back
Top Bottom