Makosa 5 Wajasiriamali Wanafanya Katika Mtandao wa Facebook na Instagram

Dr. Said

Senior Member
Nov 16, 2010
109
497
Kama wewe ni mjasiriamali unayetafuta wateja kupitia mtandao wa Facebook na Instagram lakini unahangaika basi inawezekana unafanya makosa yafuatayo:

  1. Unatangaza bidhaa / huduma unazotoa: Mitandao ya kijamii (tofauti na e-commerce) hayakutengenezwa kwa ajili ya watumiaji kununua bidhaa / huduma yoyote. Facebook na Instagram ni vijiwe vya watu kukutana, kuchat na kufuatilia umbea.

  2. Unatumia ma group ya Facebook kutangaza bidhaa/huduma zako: Japokuwa Facebook wana ma group ya biashara haimanishi kuwa ukitumia group hizo utapata wanunuzi wa kununu bidhaa huduma unazotoa. Tatizo kubwa la ma group ya Facebook ni kuwa wauzaji ni wengi kuliko wanunuzi. Utajikuta unaingia katika competition bila ya sababu yoyote.

  3. Unatangaza Biashara Yako Katika Kurasa Binafsi: Badala ya kutumia Facebook business page, unatumia personal page (kurasa binafsi) kutangaza bidhaa na huduma unazotoa.

  4. Huwekezi katika matangazo: Kwa vile wajasiriamali wengi wanaogopa kupoteza pesa (na kuona pesa za matangazo kama matumizi badala ya uwekezaji) wengi hawathubutu kutumia pesa zao kutangaza. Kosa kubwa.

  5. Una boost matangazo: Najua unaweza kushanga kwanini ninasema ku boost matangazo ni kosa. Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa ku boost matangazo yanaleta tija kwa muda mfupi sana na baada hapo gharama za matangazo yanakuwa juu. Cha kufanya ni kuweka matangazo yako katika Facebook Ads Manager (Se connecter à Facebook | Facebook). Matangazo yatakuwa rahisi na kila ukiongeza bajeti yako matangazo yako yataonekana kwa watu wengi na kukuletea matunda makubwa zaidi.
Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Mtandao wa Facebook na Instagram Kunasa wateja na jinsi nilivyoweza kutengeneza hadi Tshs. 945,000 kwa siku bofya hapa.

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,

Dr. Said Said
 
Unaambiwa shiriki somo la ujasiliamali kwa shilingi elfu kumi ili uje kuwa milionea.
Kwanza kabla ya kushiriki unatakiwa ujiulize kwa huyo anayekufundisha huo ujasiliamli ameshakua milionea?

Kama jibu ni No basi ujue kapata fursa nae anaitumia.
 
Asante said nimesoma na kuelewa nakuwa mwanafunz soon wakat najaza nikishindwa kuelewa utanielekeza
 
mkuu ile ads account/ fb ads manager unapotaka kuiweka active unajaza zile kadi za bank zinazosurpot online business, swali je, ninapotaka kupromote page/kuboost post natumia pesa halali au ni yale ma namba namba ya USD yaliyomo kwenye huyo ads account??
 
mkuu ile ads account/ fb ads manager unapotaka kuiweka active unajaza zile kadi za bank zinazosurpot online business, swali je, ninapotaka kupromote page/kuboost post natumia pesa halali au ni yale ma namba namba ya USD yaliyomo kwenye huyo ads account??
Pesa za namba namba ya USD ndio zipi hizo? Kwani hiyo USD sio pesa halali?

Sijakuelewa hapo
 
Back
Top Bottom