Makosa 4 aliyoyafanya Harmonize mpaka sasa

Kuna jambo kubwa hamjajua siri yote anayo Petro Magoti wa Kigamboni anakaa sana pale Ikulu, ni jamaa kibiongo fulani hivi

Harmonize kiburi kapata Kwa Polepole Humphrey, kaahidiwa Mengi na CCM kwenye makampeni, pia ameshasaini Mkataba wa Bilion kadhaa na Kampuni ya Uganda kuputia Winnie Nwagi , kwake mashari ya Mikataba mipya ilikuwa lazima awe independent,

Britannica
 
inaweza ikawa kama watu wana hisi ni jambo la kawaida lakini ukiangalia kwa makini alichofanya harmonize ni moja kati ya worst move kibiashara..uwa tuna jiachia taratibu taratibu huku tukiendelea kumfilisi boss kuliko kuamka na kwenda kuanza maisha mapya akati unalala nyumba ya ofisi na gari la ofisi..
nime sema wampe namba ya ebitoke au mkali wenu maana wana akisi mfano halisi wa kuwa hakuna msanii mkubwa kuliko lebo kabla hawaja jitoa timamu tv walikuwa ni moja kati ya top comedian lakini hakuna mtu aliyekuwa anatilia manani nafas ya timoth conrad katika ukuaji wa majina yao.walipotoka kwenye lebo nazan mnaona kinachoendelea
na kama harmonize asipokuwa
makini nazan na yeye mtamsahau af mtasema karogwa
 
Hii yote imechangiwa na said fella huyu jamaa inaonesha ana roho ya kinyonyaji c mnakumbuka yamoto band alivyokuwa anawanyonya mpaka watoto wakamkimbia sasa kaingia wasafi nahuko kazi ni hiyo hiyo tena huko kakutana na mafisadi wenzake tale na sallam,

Hapo anayefuatia kukimbia ni rayvany atafuata hako katoto sjui wanakaita lava lava ambacho juz nilikaona mitandaoni kanamshika shika uwoya then wcb itabaki na mondi pekee na hao mafisadi. Nao watoe vibao vyao tuone. Aiseeee
 
Umeandika kwa chuki sana mkuu na ningependa kukujibu kwa reference hai lkn muda hauniruhusu. Kabla ya kukujibu nataka ufuatilie hatua kubwa waliyofikia vijana Ferre Gola, Fally Ipupa,Heritier Watanabe na wakongwe JB Mpiana na Werrason. Ukitaka mafanikio usipende kubebwa.
 
Hii imeandikwa na Ali Kamwe umeshindwa kumpa credit zake..

Ukiitwa mwizi usikatae
 
Apambane tu.... !!

Ila afahamu tu .. 'Sikio halizidi kichwa'
 
Kwa kukurekebisha harmonize huwezi kumfananisha na Kiba!

Kwa hapa Tz ukitoka kwa mond anakuja harmonize alafu ndio nyumbu wengine wanafuatia!
 
1: Kuruhusu upande wa WCB kutangulia kueleza tofauti yao.

Baada ya Salam SK, kuongea, asilimia kubwa imeshaamini kua Harmo anaondoka WCB kwa jeuri. Kiburi, kujisikia na amekosa fadhila. Itamchukua muda sana kulifuta hili kwenye safari yake. Ukweli hua hauzungumzwi mara mbili.

2: Kumfolow Ali Kiba.
Bila shaka kichwani Harmonize anawaza ukubwa wake utakavyokua baada ya kuondoka WCB. Kwa vyovyote vile ili aupate ukubwa huo ni lazima apambane kusimama juu ya au kufika pale walipo Kiba na Diamond

Kufika hapo si kwa idadi ya watu wanaosikiliza ngoma zako ila ni kua na idadi kubwa ya watu wako wanaokuamini. Wasanii wengi wameua carear zao kwa kukosa uvumilivu wa kutengeneza mashabiki wao, wengi wamenasa kwenye mtego wa Kiba na Mondi. Ref Baraka da Prince, Rich Mavoko.

Kumfolow Kiba sasa ni ishara ya kutafuta huruma ya upande wa pili. Upande ambao unapambana na upande wa Diamond. Huku anaweza kupata nusu watakaomsapoti lakini lazima ajue kwa upande wa mashabiki wa WCB hakuna atakaemsapoti tena. Ameiweka rehani biashara yake!

3: Kujaribu kuacha 'kivuli chake WCB.' .
.
Ni vyema kuonekana bado anaipenda WCB, lakini kwa faida ya kazi yake na aina ya mashabiki tulionao, Harmo hatakiwi kuihusisha kazi yake na WCB. Kufanya hivyo huenda hili likawa kaburi lake kimuziki.

Kuna dhana ya unafki itaanza kumtafuna. Kama alifuta ile kusainiwa WCB, hakukuwa na ulazima wa kuacha neno WCB for Life kwenye Bio yake. Kwa lugha ya Salam SK, Harmo alianza kuivimvimbia menegament yake kabla ya kutoka. Hakuna anayejua nyuma ya kicheko cha Diamond, kuna nini.
.
.
4: Kutaka kuachia wimbo mpya haraka
Hili ni kosa kubwa sana. Saa chache baada ya Salam SK kuongea, Harmo amepost cover kua yuko mbioni kuachia ngoma. Hii ni tension mbaya sana anaitengeneza.
Kwa sababu ya presha ya hivi sasa, wako watakaoichukia kazi yake. Haijalishi ubora wake, Liko sikio litamkataa tu kwa kuonekana ana kiburi cha kushindana.

Iko dhana ya 'KIKI' pia inaweza kuingia. Akaonekana mtu wa drama za mitandao. Hii ni mbaya sana.

NB: Pengine Harmo hajajua kua ni ngumu kuitofautisha WCB na Diamond. Ajipange kwa yote.
Kakimbia ushirikina pale WASAFI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom