Makosa 10 aliyotenda Mungu

Ukiwa mwema au mouvu kifo kipo pale pale

Alichojaribu kuonyesha mtoa mada ni makosa ya mungu ambayo mungu ndio mwenye makosa mpaka anasababisha uovu duniani kote
Na hapo ndipo utakapoona, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hayupo.

Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao viumbe wake wanakufa kila siku.

Kuumba hivyo, wakati anaweza kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani, ingekuwa kuwafanyia viumbe wake roho mbaya.

Na Mungu huyo, by definition, hana roho mbaya.
 
Na hapo ndipo unapoona huyu mungu ni wa kutungwa tu maana kwa Dunia ilipifika Leo kwa watu kuua kukaba kudhulumu kuiba ili bidi aingilie kati lakini yeye yupo kimya
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Hii thread imejaa hoja na maswali ambayo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sana. Ni kama.uliandika mawazo yangu.

Nchi za wenzetu walipoanza kugundua kuwa hakuna Mungu wakaachana na huu utumwa wa kuabudu hewa( vitu vya kufikirika) ndipo walipoanza kupata maendeleo ta kimwili na kiroho.
 
Sasa kama Mungu aliituumba pure,,,,dhambi ilituingia kwa mechanism gani???
Na kwa nini aliumba kiumbe ambacho ji dhaifu kiasi cha kuaingiliwa na dhambi? Je uwezo huo hakuwa nao, kama alikuwa nao kosa ni la nani?

Maana mimi nimeumbwa na udhaifu, siwezi kuresist dhambi na aliyeniumba hivyo yupo.
 
Na hapo ndipo unapoona huyu mungu ni wa kutungwa tu maana kwa Dunia ilipifika Leo kwa watu kuua kukaba kudhulumu kuiba ili bidi aingilie kati lakini yeye yupo kimya
Angekuwepo, asingehitaji hata kuingikia kati.

Angeumba ulimwengu ambao hayo yote hayawezi hata kutokea.

Sasa kwa nini watu wanaukubali uongo huu?
 
Hii thread imejaa hoja na maswali ambayo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sana. Ni kama.uliandika mawazo yangu.

Nchi za wenzetu walipoanza kugundua kuwa hakuna Mungu wakaachana na huu utumwa wa kuabudu hewa( vitu vya kufikirika) ndipo walipoanza kupata maendeleo ta kimwili na kiroho.
Ukiamini Mungu wa uongo huyu hata maendeleo ni vigumu kupata.

Wanasiasa waongo watakuchezea akili.

Watakwambia wao ni "chaguo la Mungu".

Na ukiamini hilo, hata kuwahoji utashindwa.

Watakupiga maisha yote, wakikuambia utalipwa peponi.

Huku hata wao wakijua hakuna pepo.

Ndicho kinachoendelea sehemu nyingi sana duniani.
 
dunia ya watu kutokufa itakuja ila hii ya sasa lazima kila mtu kila kitu akiwamo na shetani na washiraka wake wafe wote
 
dunia ya watu kutokufa itakuja ila hii ya sasa lazima kila mtu kila kitu akiwamo na shetani na washiraka wake wafe wote

Kwa niniMungu atubanie tungoje wakatiangeweza kutupa raha muda wote?

Unaweza kuhakikisha itakuja na kwamba hizo habari za itakuja si stories za uongo tu?
 
Mtoa uzi yuko sawa hata mimi nilihoji kwa nini tunakufa wakati mungu hauwi wakanambia ahadi ya mtu ikifika anakufa nikahoji vp watoto wadogo wanaokufa na wale wanaozama baharini na wanaopotea inakuaje kwa sababu niliambiwa ukifa ukizikwa kuna malaika anakuja kukuuliza maswali ukishindwa kujibu anakuadhibu sasa hapo ndio hoja yangu ikaanzia hapo kwa kweli kama binadam si dhambi kutaka kujua historia yako
 
Moja ya sababu tunakufa nikutokanana ukweli kwamba hakuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezowote na upendo wote.

Mungu huyoangekuwepo, kwanini asingeumba ulimwengu ambao hauna kifowalaubaya wowote?

Uwezo angekuwa nao, ujuzi angekuwa nao, upendo angekuwa nao, kitu gani kingemzuia asiumbe ulimwengu ambao mabaya yoyote hayawezekani?

Kama angeweza kuwa na kitu kinachomzuia, je nikweli angekuwa na uwezo wote, mbona kungekuwa na kitu kinamzuia kuumba ulimwengu bora kabisa?

Kama hakuna ambacho kilimzuia, hakutaka tu, je, Mungu ambaye anaweza kutupotezea kirahisi hivyo, kutubania bila sababu, anaweza kuwa Mungu mwenye upendo wote? Mbona atubanie hivyo?

Ukichunguza sana unaona kuwa, Mungu huyo hayupo.

Ila watu wengi washakubalishwa yupo, wanafuata mapokeao tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom