Makontena ya meno ya Tembo yakamatwa Zanzibar

Radi

Member
May 22, 2010
94
16
Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar vimekamata shehena ya meno ya Tembo iliyokuwa imefichwa kwenye makontena mawili yaliyokuwa na dagaa katika Bandari ya Zanzibar.

Mkuu wa Bandari ya Malindi, Martin Lissu, alisema makontena hayo yalikamatwa jana mchana na kuongeza kuwa yalitokea Tanzania Bara yakidaiwa yalikuwa njiani kuelekea Malyasia.

Lisu alisema ndani ya makontena hayo kulikuwa na magunia ya dagaa ambapo kila gunia lilikuwa na vipande kati ya 8-10.

Alisema shehena hiyo iliwasili mjini Zanzibar wiki mbili zilizopita kwa Meli ya MV Break iliyotokea Tanzania Bara.

Taarifa kutoka Bandari ya Zanzibar zilisema watu wawili wanashikiliwa pamoja na wakala aliyepokea mzigo huo kutoka Bara.

Alisema baada ya kuwasili visiwani humo mzigo huo ulihifadhiwa eneo la Mwanakwelekwe ambapo kila moja lilikuwa na urefu wa mita 20.

Makontena hayo yalikuwa na magunia 135 ya dagaa ambayo inadaiwa yalitokea jijini Mwanza, lakini kabla hayajaondoka visiwani humo yalidakwa na vikosi vya usalama.

Taarifa zinasema mzigo huo ulikuwa unasafirishwa na raia wa China na kwamba watu waliokuwa wakisafirisha walikuwa wanatumiwa.
CHANZO: NIPASHE

My take:Amakweli Tanzania sasa ni shamba la bibi .Tutafika kweli jamani?
 
Wachina watatumaliza, ngoja tusubiri tuone kama wachina hao watapiga watu marisasi kama ilivyotokea huko Sumbawanga.
 
Natamani uchunguzi ufanyike mara moja alafu nipate suprise lingine kama la Jairo.
Hawakawii kukanusha na kutuambia zilikuwa pembe za ng'ombe.
 
Hapo lazima kutakua na kiongozi mmoja wa serikali anashiriki biashara hiyo.
Tazania imekua Shamba la kuchota mali na wajanja,hivyo vipande vyote vya meno ya tembo ni sawa na ndovu wangapi? naomba mnisaidie kujua.
 
..........Leo jioni, mida ya saa kumi na moja vyombo vya Dola Unguja wamekamata container mbili zilizoingia ZNZ kwa boti kama mizigo ya Dagaa kutoka Mwanza, ikipita kuelekea "On transit" Malaysia. Baada ya kuzistukia na kuzikagua, wamebaini kuwa hayo maguni ya dagaa ndani ya container yalikuwa yamejaa Pembe za Ndovu. Unaweza kung'amua nani yuko makini kati ya Dola ya Bara na ile ya Visiwani. Hili pia linaongeza matumaini kwa Serikali iliyoko madarakani.

Heko Wa-ZNZ.
 
si hami nchi hii, napenda sana kusikia vioja hivi kila siku na serikali kama haipo vile
 
Natamani uchunguzi ufanyike mara moja alafu nipate suprise lingine kama la Jairo.
Hawakawii kukanusha na kutuambia zilikuwa pembe za ng'ombe.
Tunaomba ripoti hiyo asipewe Luhanjo, majibu ya uchunguzi yatakuwa ni kichekesho. " Haikuwa pembe za ndovu isipokuwa ni Dagaa walioharibika kisha wakagandiana kutokana na kukosa hewa".
 
Nchi nzuuuuuriiii tanzaniaaaaaa Jina lako nitamu sanaaaaaaa! Sintoweza kusahau mimi maajabu ya kwetu kabiiiiiiiiiisaaaaa tanzania tanzaniaaaaaa nakupenda kwa moyoo wooooteee!
Nilalapo nakuota wewee niamkapo ni heri mama weee. Tanzania tanzania nakupenda kwa moyooo wooooteeee.
 
Back
Top Bottom