Makontena Mawili Yakiwa na Pembe za Ndovu Yakamatwa Zanzibar!

Zanzibar ina rais na intellegensia inayofanya kazi.

Ile habari ya wanyama kutoroshwa wamejaribu kupata mafuta, sasa hii watasemaje?
 
Hapo utashangaa ripoti itakayotolewa!!! Ni mohogo ilikuwa inatolewa Bagamoyo...WaTz bwana, tunaelekea kuwazidi wa-nigeria kwa fix
 
Makontena hayo mawili yamekamatwa ktk bandari ya Zanzibar yakiwa na pembe za ndovu zilizokuwa zimefichwa ndani ya magunia ya dagaa. Shehena hiyo ya Dagaa imetokea Mwanza na imepakiliwa ktk boti ikitokea bandari ya Dar es Salaam. Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana mmoja wao ni nahodha wa boti hiyo.
Souce: ITV BREAKING NEWS.. Saa 10 jioni.

Hiyo ni kama ka-ajali tu. Kuna mmoja hakutosheka na mgao. Wewe subiri itaishia hewani kama kawaida
 
Back
Top Bottom