Makontena mawili yakamatwa bandari kavu AMI Dar na madawa ya kulevya

Tiger One

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
568
310
Katika hali ya kushangaza makontena mawili yamekamatwa bandari kavu AMI Dsm yakiwa na material zakutengenezea madawa ya kulevya yaliyoagizwa na kupakiwa toka india kwa meli za CMA. Maajabu ni kwamba makontena hayo yamepitaje bandari zote mbili, India na Dsm bila kuonekana kwenye vifaa vya kitaalam bandarini humo?
 
Aisee! kuna rafiki mwingine ataambiwa anapendwa ila ajitathimini na barua ya utenguzi nafuata..
 
Nchi ya hovyo sana hii, sasa kama scanner zilishindwa kuona mataruma ya reli yaliyofichwa kwenye mchanga ndio zitaona dawa?! Bado tuna safari ndefu sana kuzuia magendo hapo bandarini.
 
Ni moja ya maigizo yanayoendelea nchini

Kwanini hivi kila kitu huwa tunakimbilia tu kusema ni Maigizo? Hili ingekuwa ni Bomu la kuiangamiza Tanzania nzima limetegwa na kuteguliwa ungekuja na huu Upupu / Upuuzi wako na kusema kuwa ni mambo tu ya Maigizo? au hilo Kontena ulitaka liibuliwe na Wapinzani wako unaowashabikia pengine ndipo ungeamini kuwa ni kweli? Nasikitika tu kwamba badala ya Siasa zetu hizi za Vyama Vingi zitujenge hasa Kifikra, Kiumoja, Kiuzalendo na Kimtizamo wa Mama Tanzania sasa zimetufanya tuwe Wapumbavu na wa hovyo hovyo tu.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania.
 
Watu wa madawa wanazo mbinu nyingi sana, na hiyo ni moja wapo tu ya mbinu elfu walizonazo kusafirishia madawa. Kazi nzuri, wakakutane na mkono wa sheria sasa.
 
Katika hali ya kushangaza makontena mawili yamekamatwa bandari kavu AMI Dsm yakiwa na material zakutengenezea madawa ya kulevya yaliyoagizwa na kupakiwa toka india kwa meli za CMA. Maajabu ni kwamba makontena hayo yamepitaje bandari zote mbili, India na Dsm bila kuonekana kwenye vifaa vya kitaalam bandarini humo?
Ni hali ya kushangaza kweli mkuu. Dah!
 
Back
Top Bottom