Makontena 50 ya saruji yaingizwa Z`bar bila kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makontena 50 ya saruji yaingizwa Z`bar bila kodi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini.  Makontena 50 ya saruji yenye thamani ya Sh. milioni 114.8 yameingizwa Zanzibar yakitokea nchini Pakistan bila kulipiwa kodi kupitia Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.
  Uchunguzi wa Nipashe umegundua kuwa makontena hayo yaliingizwa visiwani humu kufuatia msamaha wa kodi uliotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini.
  Kibali cha msamaha wa kodi kimetolewa Mei 12, mwaka huu chenye kumbukumbu namba WF/EXEMPT/TA/2010/VOL.II/NO.2 akitakiwa Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kanda ya Zanzibar kutotoza kodi ya ushuru wa forodha mzigo huo.
  Shehena hiyo ya Saruji ililetwa Zanzibar na meli ya mizigo ya MV Concord ikitokea Karachi nchini Pakistan na kuwasili Zanzibar wiki iliyopita. Nyaraka za usafirishaji mzigo huo yenye kumbukumbu namba Karzan-091 ya Aprili 24, mwaka huu, inaonyesha makontena hayo yaliletwa na kampuni ya uwakala wa mizigo ya Abdul Enterprises C/F Company ya Darajani mjini Zanzibar.
  Kampuni hiyo imepewa kazi ya kuingiza saruji hiyo na Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ.
  Kwa mujibu wa msamaha wa kibali cha msamaha wa kodi cha waziri saruji hiyo haitakiwi kutozwa ushuru wa forodha pamoja na Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT)
  Hata hivyo, saruji hiyo imeanza kuingia katika soko la ndani la Zanzibar na kuuzwa katika maduka ya rejareja. Mzigo huo wa saruji uliingizwa nchini kwa kutumia nyaraka za usafirishaji zenye namba 20100425CON703ZNZ ya Aprili 25, mwaka huu. Uchunguzi wa Nipashe imebaini saruji inathamani ya dola za Marekani 84,000 Aprili 10, mwaka huu kutoka kampuni ya uwakala ya HMG International Agencies yenye makao makuu yake Karachi, Pakistan.
  Naibu Kamishina wa TRA Kanda ya Zanzibar, Hassan Mcha, alithibitisha jana makontena hayo kutolewa bila ya kulipiwa kodi kutokana na msamaha wa kodi uotolewa na Waziri wa Fedha Zanzibar.
  Akizungumza na Nipashe Dk. Makame alithibitisha kutoa msamaha huo lakini alisema hana taarifa kama saruji hiyo imeanza kuingizwa katika soko la ndani la Zanzibar.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. K

  Kikambala Senior Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kwa mtindo huu maendeleo yatakuja kweli au ndio harakati za chama chetu kukusanya billion 50 za uchaguzi ?.bora hao wazungu waliiositisha baadhi ya pesa maana huu ni uhayawani,ubazazi na uzandiki mtupu .nambar one msije juta baadae mtakapo kuwa watazamaji wa serikali hii
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sa ndo vizuri watu wajenge nyumba kwa bei nafuu
  saruji si haijalipiwa kodi?
   
Loading...