Makongoro Nyerere Na Project Rejesha Jimbo la Arusha Mjini!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
​Moja kati ya makumi ya wasaka urais kupitia CCM waliojadiliwa sana ni Makongoro Nyerere! Wapo wanaoamini kwamba Makongoro atapitishwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM! Niseme tu kwamba hakuna kitu kama hicho isipokuwa Makongoro ni Project Rejesha Jimbo la Arusha Mjini mikononi mwa CCM! Makongoro amekuwa kimya kwa muda mrefu na hivyo walichofanya CCM ni kumshawishi kutafuta nafasi ya kugombea urais wakati malengo ya ndani ya CCM ni kumpa publicity na kuwaandaa kisaikolojia wana-Arusha Mjini kwamba, mwana CCM mwenye sifa za kuwa Rais anarudi jimboni Arusha kutafuta ridhaa ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo hilo bungeni! Kutokana na hilo, UKAWA, hususani CHADEMA tayari wamesharahisishiwa kazi za kufahamu ni nani wanatapambana nae Arusha Mjini kwa hiyo, wanaweza kuanza mikakati mapema kwa kuwa tayari wanamfahamu hasimu wao!

Mtu mwingine aliye kwenye project sawa na hii ni Dr. Augustino Mahiga! Huyu nae hakuna cha urais wala nini bali CCM wametaka kumpa publicity hasa ukizingatia, nature ya kazi ambazo amepata kuzifanya basi kuna uwezekano hata huko jimboni kwao kwa asili hafahamiki vizuri! Kutokana na hilo, hapa pia UKAWA wanatakiwa kufahamu Mahiga ni mtu wa wapi na ikiwa wanafahamu basi kuna uwezekano mkubwa kwamba huyu ndie atakuwa mpinzani wao jimboni!

Wakati Makongoro anatakiwa kwenda kulinasua jimbo la Arusha Mjini, Mahiga anatakiwa ili aje kushika nafasi ya Bernard Membe endapo CCM itarudi madarakani! CCM kama sio JK wanafahamu kwamba miongoni mwa wagombea wote, ukimtoa Membe na Mahiga, hakuna mwingine mwenye uelewa na uzoefu kwenye masuala ya kimataifa kwahiyo endapo atateuliwa mtu yeyote basi awe na waziri wa mambo ya nje ambae ni mzoefu katika masuala ya kimataifa!

Hao wawili ni official projects zinazolenga kutoa publicity ili wawe wabunge! And don't forget, ikiwa watu wanaamini kwamba Makongoro anafaa kuwa rais basi msishangae hitimisho la project husika ni kupewa u-PM endapo atashinda na CCM kuingia madarakani!

Wapo pia wengine kama akina Jacob Tesha na wengine kama hao ambao pia wapo kwenye project ubunge tofauti tu ni kwamba, wakati Makongoro na Mahiga ni official undercover projects; watu kama akina Jacob Tesha ni personal projects za kutafuta publicity ili baadae wakatafute nafasi ya kugombea ubunge! Mpinzani wenu mwingine ni huyo hapo wana-UKAWA!
 
kwa hapa Arusha hata Kinana hawezi pamoja na kuwa ni mzawa wa Arusha, kama wakitumia kuonga pesa zinaliwa lakini kura kwa Lema
 
Acha hadaa wewe yaani aache ubunge wa EAC aje Arusha?

Mako ndio next president.
 
hakuna kitu kama hicho, huyo makongoro hawezi kwenda arusha zama hizi,mleta mada unafikiri nani atapitishwa?
 
hakuna kitu kama hicho, huyo makongoro hawezi kwenda arusha zama hizi,mleta mada unafikiri nani atapitishwa?
Atapitishwa nani kwenye uchaguzi upi? Na kwanini unadhani hawezi kwenda Arusha zama hizi ndugu malokola?
 
Last edited by a moderator:
haa haa labda arusha ya ruvuma....
Kwa maana? Kama wewe sio mwana CCM, don't underestimate him!!! Na labda nikukumbushe, CCM safari hawatakurupuka kuteua mtu wa kugombea Arusha... lazima watajipanga kimkakati ili kujaribu kulinyakua jimbo hilo! Ingawaje majimbo yote yana equal administrative power lakini kwa CHADEMA Arusha ni jimbo mkakati na kuwanyang'anya itakuwa ni sawa na kuwatoa nishai ya mwaka! Naamini hata leo kama mtu ataamua kufanya utafiti kuangalia ni jambo gani linasubiriwa matokeo yake kwa hamu; bila shaka Arusha Mjini... mimi nasubiria sana Arusha Mjini kuliko jimbo lolote lile; wewe je?
 
Kwanini asipewe project ya rejesha Jimbo la Musoma Mjini ambalo yeye anaishi na linashikiliwa na Vicent Nyerere wa CDM? Au ndugu kwa ndugu hawaumani!.

Membe na Mahiga ndiyo wana uzoefu na mambo ya kimataifa! Vipi Dr. Asha Rose Migiro maana ndiye aliyem mentor Membe akiwa deputy wake MoF, lakini pia Dr Migiro amefanya UN.
 

...ukimtoa Membe na Mahiga,hakuna mgombea mwingine mwenye uzoefu na uelewa juu ya masuala ya kimataifa...


Hivi anatafutwa rais wa Tanzania au rais wa kimataifa?

Yaani mtu anayeyaelewa vyema masuala ya nchi yake hafai mnamtaka anayeyaelewa masuala ya nchi nyingine ili awe MATONYA MZURI au?

Kwa nini hao wenye uzoefu wa kimataifa wasiwe mawiziri wa foreign affairs ili rais awe mwenye kuelewa vyema masuala ya nchi yake?

Any way,Kikwete nae alinadiwa hivihivi kwa hoja hizihizi lakini sote tunafahamu kilichotokea.

Man,get out of the box!!
 
unajifariji eeeeh!!! jiandae kisaikolojia....mwisho wenu wa ajira kwa edo ni leo...majina matano hayooo
 
Rudisha arusha mjini? Mnachekesha! Kwa taarifa yenu tu hata mumfufue mwalimu nyerere na sokoine hawawezi irudisha arusha mikononi mwa walanguzi wa gesi na rasilimali zetu.. Pambaff zenu wote mnaoshabikia ccm na mafisadi wake
 
Back
Top Bottom