Makongoro Nyerere: Lowassa nisamehe sana, ila ni Lazima tukuvue gamba haraka!

wakati Makongoro atataka kumvua gamba lowasa kitu naona hapa ni kwamba''Gamba hili litaondoka na nyama na kuacha mifupa ndani ya mwili wa ccm. Subiri uone!!
 
Mkapa-kiwira,simu2000,nbc,mgololo,netgroup, JK-Iptl,rites,buzwagi,miradi yote hiyo ya kifisadi haina tija kwa mtanzania
 
Huyo makongoro mwenyewe ni mpinzani tangu 1995 nafikiri hajarudisha kadi ya NCCR- mageuzi after all who is he..?! Chama siyo Mali ya familia yao ni cha watanzania wote.
Hapana, yeye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara mtu mkubwa sana katika chama hivyo hupaswi kumbeza hivyo.
 
Mtu akisimamia ukweli mnasema ana witu tu, akinyamaza mtamuita majina mengine, sasa afanyeje? Na hata huo wivu anaomuonea Lowassa ni upi? Makongoro anakula jasho lake thru Uenyekiti wa CCM Mkoa (Mara) na si ajabu akawa anamegewa kafungu from Mwil's pension BUT Lowassa anakula vya ufisadi maana hata pension ya Uwaziri Mkuu Mstaafu hayuko eligible.
 
hey jf kumekucha,

hali si shwari kati ya kapteni makongoro nyerere na edward lowassa. Taarifa za kina zinaeleza vuta nikuvute hiyo imezidi kupamba moto huku safari hii makongoro akiamua kuvunja ukimya na kuweka bayana maamuzi yaliyofikiwa na nec ya kumvua gamba lowassa ni lazima yafanyike mara moja pasipo kusita.

Taarifa zaidi ambazo tumezinasa kwa njia ya simu kutoka huko dar es salaam maeneo ya kinondoni biafra kutoka kwa mwandishi mmoja wa gazeti la dira ya mtanzania zinabainisha kuwa ni makongoro nyerere ndiye aliyeanika taarifa za lowassa kutaka kuyaanika maovu ya kikwete wiki moja iliyopita na huku wiki hii makongoro huyohuyo akiibuka na madai mengine mazito kuhusu azma ya kikwete kuwakingia kifua lowassa na chenge ili wasitemwe kwenye kikao kijacho, makongoro amekaririwa akisema "hata kama kiwete akitaka amlinde huyu lowassa, kweli kaka yangu lowassa atatusamehe ni lazima tumng'oe bila kusita, itabidi tupinge hoja za kikwete kwa maana hana ubavu wa kutulazimisha"



amani his past is over lets give him second chance
 
Mimi nauliza ni kosa au jambo gani alilofanya Lowassa ambalo CCM wengine hawakufanya??????????

CCM wenzake wamefanya makosa kama/zaidi ya kwake. Tofauti ya EL na mafisadi wengine yeye ufisadi wake ULIKICHAFUA chama. Hawa wengine ufisadi wao haujaibuliwa kiasi cha kukichafua chama chao.
 
Mr. Richard

Hapo unapotoka , si kweli kuwa wote ndani ya CCM ni wachafu wapo watu waadilifu kama katika vyamma vingine. Hivi kwa akili yako vyama vya upinzani ndo vina wasafi wote?
wapo wazuri sana CCM, ila kwa sasa ni vigumu kupata nafasi hata ya kusikika! Upinzani pia kuna wabovu ila nao hawajapata nafasi ya kusikika!
 
wapo wazuri sana CCM, ila kwa sasa ni vigumu kupata nafasi hata ya kusikika! Upinzani pia kuna wabovu ila nao hawajapata nafasi ya kusikika!

WAZO LA LEO
"kutafuta mgombea safi wa urais kutoka CCM ni sawa na kutafuta bikra wodi ya wazazi katika waliojifungua..."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom