Makongoro Nyerere jifunze kutoka kwa Chalamila, punguza Masihara

Brother Mako

Najua wewe ni mtu wa masihara na utani utani mwiiingi. Utani hoye!

Najua wewe ndivyo ulivyo toka long time kitambo.

Ila nataka nikueleze kitu, Kuwa makini sana na utani wako usifikie hatua ya kuharibu haiba na taswira ya taasisi ya Urais au rais mwenyewe!. Namaanisha ukimtaja rais mtaje si katika muktadha wa masihara masihara, bali mtaje ukiwa serious na kwa vitu serious. Kama unataka kumtania rais basi acha hiyo kazi aliyokuteua, njoo JF tumtanie na tumchane kwelikweli akizingua!

Chalamila leo katumbuliwa, naamini sababu kubwa haswa ni ile clip aliyosikika akisema kuwa kwenye ziara ya rais huko Mwanza watu wanaweza kubeba mabango yoyote yale hata kama ni matusi! Naamini kabisa from the bottom of my heart kuwa Chalamila hakumaanisha kuwa watu wanaweza kubeba mabango ya Kumtukana rais, Bali alimaanisha kuwa watu kama wanahisi wana hasira dhidi ya utendaji wa mkoa wa Mwanza basi hata kubeba mabango ya kuwatukana viongozi wa mkoa huo mbele ya rais basi sawa tu!

Ukizingatia kuwa clip ya Chalamila imekatwa, watu wanaweza kushindwa kujua nini logic ya kauli yake. Hata hivyo Chalamila naye ameshindwa kutumia busara kwa kushindwa kujua kuwa kauli yake inaweza kutafsirika vibaya kuwa

1. Anacheza shere agizo la rais la kuruhusu watu kubeba mabango kwenye ziara zake.

2. Kwamba anamchukulia poa rais kwa kutoa kauli za mizahamizaha

Sasa ndugu Mako, kuwa Makini na mizahamizaha hasa juu ya maagizo ya rais. Mzaha ni bora uende vizuri ila ukienda vibaya, na wabaya wako wakaikatakata clip yako ili kukuchongea, hutaeleweka vizuri.

Nakushauri ndugu Mako, Fanya Mzaha 1% ila piga kazi 99%. Na mzaha wako usiinvolve jina la rais kabisa kwa sababu ukikosea pale utapata tabu sana.

Kumbuka busara za bungeni kwa nini kuna kanuni ya kutolitumia jina la rais kwa njia za mizaha ili kujipatia uhalali wa hoja.
Mako ndo alivyo!! Ukitaka awe unavo taka atakuwa kichekesho zaidi.
Mizaha we ndo unaiona mizaha hivyo!! lkn siyo sisi wengine upo.

Km atatumbuliwa sababu ya haiba yake ambayo weye unaiona ni mizaha huyo ni sawa tu atafanya kazi nyingine!! Afanyeje sasa ajiue???

Nasema hivi Yeye ndo alivyo ki haiba km baba yake usimpangie!!mara ngapi jk kachekesha umma??
Acha udodoma huo wewe......
 
Ilikuwa ni nadra Nyerere kumaliza hotuba bila watu kucheka, haiba nyingine ni za kurithi....hata alivyokuwa anaomba kura bungeni kuteuliwa kuwa mbunge wa East Africa wabunge walikuwa wanaangua kicheko tangu anaanza kuongea na zile gestures kama baba yake...
 
Makongoro ndivyo alivyo, hata kwenye vijiwe yuko hivyo hivyo....hanaga mambo ya ukuda

Sijui nikuweke ndani, kufokea watu

Mpka sasa wafanyakazi huko manyara wanamkubali sana

Ova
Yule angekua mwalimu tena wa maths, wallah wanafunzi wangefaulu kuliko kawaida,
 
Ahahahahha nilikutana naye majuzi kati pande za O'bay sema kachoka aisee! Magu aliwagusa wengi sana aisee!
Hivi yuko wapi kwa sasa?? Ila yule binti yake mkubwa ana mashauzi sana yule dada km mdingi wake namtafuta kwa hamu....nikimpata!!!heee
 
Brother Mako

Najua wewe ni mtu wa masihara na utani utani mwiiingi. Utani hoye!

Najua wewe ndivyo ulivyo toka long time kitambo.

Ila nataka nikueleze kitu, Kuwa makini sana na utani wako usifikie hatua ya kuharibu haiba na taswira ya taasisi ya Urais au rais mwenyewe!. Namaanisha ukimtaja rais mtaje si katika muktadha wa masihara masihara, bali mtaje ukiwa serious na kwa vitu serious. Kama unataka kumtania rais basi acha hiyo kazi aliyokuteua, njoo JF tumtanie na tumchane kwelikweli akizingua!

Chalamila leo katumbuliwa, naamini sababu kubwa haswa ni ile clip aliyosikika akisema kuwa kwenye ziara ya rais huko Mwanza watu wanaweza kubeba mabango yoyote yale hata kama ni matusi! Naamini kabisa from the bottom of my heart kuwa Chalamila hakumaanisha kuwa watu wanaweza kubeba mabango ya Kumtukana rais, Bali alimaanisha kuwa watu kama wanahisi wana hasira dhidi ya utendaji wa mkoa wa Mwanza basi hata kubeba mabango ya kuwatukana viongozi wa mkoa huo mbele ya rais basi sawa tu!

Ukizingatia kuwa clip ya Chalamila imekatwa, watu wanaweza kushindwa kujua nini logic ya kauli yake. Hata hivyo Chalamila naye ameshindwa kutumia busara kwa kushindwa kujua kuwa kauli yake inaweza kutafsirika vibaya kuwa

1. Anacheza shere agizo la rais la kuruhusu watu kubeba mabango kwenye ziara zake.

2. Kwamba anamchukulia poa rais kwa kutoa kauli za mizahamizaha

Sasa ndugu Mako, kuwa Makini na mizahamizaha hasa juu ya maagizo ya rais. Mzaha ni bora uende vizuri ila ukienda vibaya, na wabaya wako wakaikatakata clip yako ili kukuchongea, hutaeleweka vizuri.

Nakushauri ndugu Mako, Fanya Mzaha 1% ila piga kazi 99%. Na mzaha wako usiinvolve jina la rais kabisa kwa sababu ukikosea pale utapata tabu sana.

Kumbuka busara za bungeni kwa nini kuna kanuni ya kutolitumia jina la rais kwa njia za mizaha ili kujipatia uhalali wa hoja.
Kilichomtoa Chala si kauli za utani bali uvunjaji wa sheria na msitake tuseme huenda na harufu ya rushwa....
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom