Makongoro Nyerere jifunze kutoka kwa Chalamila, punguza Masihara

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,090
Brother Mako

Najua wewe ni mtu wa masihara na utani utani mwiiingi. Utani hoye!

Najua wewe ndivyo ulivyo toka long time kitambo.

Ila nataka nikueleze kitu, Kuwa makini sana na utani wako usifikie hatua ya kuharibu haiba na taswira ya taasisi ya Urais au rais mwenyewe!. Namaanisha ukimtaja rais mtaje si katika muktadha wa masihara masihara, bali mtaje ukiwa serious na kwa vitu serious. Kama unataka kumtania rais basi acha hiyo kazi aliyokuteua, njoo JF tumtanie na tumchane kwelikweli akizingua!

Chalamila leo katumbuliwa, naamini sababu kubwa haswa ni ile clip aliyosikika akisema kuwa kwenye ziara ya rais huko Mwanza watu wanaweza kubeba mabango yoyote yale hata kama ni matusi! Naamini kabisa from the bottom of my heart kuwa Chalamila hakumaanisha kuwa watu wanaweza kubeba mabango ya Kumtukana rais, Bali alimaanisha kuwa watu kama wanahisi wana hasira dhidi ya utendaji wa mkoa wa Mwanza basi hata kubeba mabango ya kuwatukana viongozi wa mkoa huo mbele ya rais basi sawa tu!

Ukizingatia kuwa clip ya Chalamila imekatwa, watu wanaweza kushindwa kujua nini logic ya kauli yake. Hata hivyo Chalamila naye ameshindwa kutumia busara kwa kushindwa kujua kuwa kauli yake inaweza kutafsirika vibaya kuwa

1. Anacheza shere agizo la rais la kuruhusu watu kubeba mabango kwenye ziara zake.

2. Kwamba anamchukulia poa rais kwa kutoa kauli za mizahamizaha

Sasa ndugu Mako, kuwa Makini na mizahamizaha hasa juu ya maagizo ya rais. Mzaha ni bora uende vizuri ila ukienda vibaya, na wabaya wako wakaikatakata clip yako ili kukuchongea, hutaeleweka vizuri.

Nakushauri ndugu Mako, Fanya Mzaha 1% ila piga kazi 99%. Na mzaha wako usiinvolve jina la rais kabisa kwa sababu ukikosea pale utapata tabu sana.

Kumbuka busara za bungeni kwa nini kuna kanuni ya kutolitumia jina la rais kwa njia za mizaha ili kujipatia uhalali wa hoja.
 
Kwa lugha rahisi unataka Makongoro aishi kama yuko Jela.

Maisha hayawezi kusimama kwakuwa eti mtu siyo mkuu wa mkoa.

Acheni kuabudu TEUZI.

Makongoro siku zote yuko hivyo, leo ana miaka karibu 60 ndio unategemea kwasababu umemteua Mkuu wa mkoa ndio atabadilika.
 
Afadhali Mako anaujua utani, huyu alikuwa analazimisha !Kuchekesha watiu no kipajicha kutumia maneno kwa ufundi!

Hata Marehemu Magufuli alikuwa anapenda utani, lakini Mara nyingi alitania kwa namna ambayo inakera, pegine kuumiza .

Kwa Bwana Chalamila yeye kwa kweli utani wake mmmmhh!

Fikiria Mkuu wa Mkoa umekaa nawazee unaanza hubiri pombe,tenakwa mwalekeo wa kuwashangaa /kuwabeza wasio kunywa, hapohapo kuna Maaskofu, Masheikh na walokole😃
 
Samia ni Magufuli.

Samia aliteuliwa na Magufuli kama alivyoteuliwa Sabaya, Hapi, Majaliwa,Mpango etc

Acha wanafunzi wa Magufuli waumane
Muone Mataga anajipa moyo! Mkija kushtuka, mtajikuta wote mko barabarani mnauza madafu! Kama ulikua hujui, huu ndiyo ukweli mchungu! Samia ni JK! Na wala siyo Magufuli kama unavyo ota.

Magufuli wako aliwapiga zengwe akina Amos Makala na Batilda Burhan (Team JK), Mama kawarudisha kundini! Halafu hao Team Magufuli wenzako ndiyo anawatumbua tu mmoja baada ya mwingine! Kuanzia Bashiru Ali, Sabaya, Chalamila! List bado inaendelea! Mpaka Mataga wote muishe!
 
Back
Top Bottom