Makongoro Nyerere ajidhalilisha kwa kumpigia magoti Magufuli..........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
mako-omba-kura.jpg

Mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (kulia) akimwinamia Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli wakati akimwomba ampigie kura iliaweze kuchukuwa nafasi hiyo kwa wagombea kutoka Tanzania Bara, Bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
 
Makongoro ampigia Magufuli magoti
Mgombea Charles Makongoro Nyerere (CCM) jana alitoa mpya baada ya kumpigia magoti Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli akimsihi ampe kura yake tukio ambalo lilivuta hisia za wabunge na wageni.
Tukio hilo lilitokea jana asubuhi kabla ya kuanza kwa Kikao cha Tano cha Mkutano wa Saba wa Bunge baada ya Makongoro kukutana na Dk Magufuli katika lango la kuingilia wabunge kuelekea ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Jamani tunajua Makongoro Nyerere yuko kijiweni kwa muda mrefu lakini thamani ya utu wake haiwezi kushushwa kiasi hicho........eti kisa anapalilia mkate..............................aibu kwa viongozi wa nchi hii kuendekeza utamaduni wa namna hii........kama ni kutumikia wananchi sidhani hii ndiyo njia.............yaelekea malengo ni kujinufaisha wenyewe tu.....
 
Umetoa mada, bado ukaona haijaitikiwa ukaamua kuanza kuchangia mwenyewe. Usiwe desperate mzee wa mvi, watakuja tu kuwa na subira
 
Kwani umwenyekiti wa Thithiem mkoa wa Mara alishaacha? Kupiga magoti anamaanisha ana shida sana jambo ambalo si kweli. Mke wake Aisha Nyerere kwa sasa ni Jaji na yuko huku Arusha mbona angetulia tu ashirikiane na mkewe kuishi maisha mazuri? Tatizo lake anajidai kijogoo wakati hata kuwika inamshinda>
 
Pengine ni watani...siwezi ku conclude moja kwa moja kwamba anajishusha utu mpaka nijue the other side of the story.
 
Kwani umwenyekiti wa Thithiem mkoa wa Mara alishaacha? Kupiga magoti anamaanisha ana shida sana jambo ambalo si kweli. Mke wake Aisha Nyerere kwa sasa ni Jaji na yuko huku Arusha mbona angetulia tu ashirikiane na mkewe kuishi maisha mazuri? Tatizo lake anajidai kijogoo wakati hata kuwika inamshinda>

Mkuu, njaa haina subira. Umesahau mgombea aliyewapigia magoti wanafunzi akiomba kura zao? Tatizo letu ni kuifanya siasa ndiyo njia ya kuleta mkate wa kila siku. Matatizo yake ni uporaji na ufisadi wa kila aina. Tutaona mengi sana.
 
Kwa wana CCM hili si jambo la kushangaza kabisa, mbona wapo wanaopiga magoti kwa watoto wadogo na kuwapa shikamoo?
 
Hebu tuingie ndani zaidi watu muwajuao wenyeji wa Butiama na Kule Chato huo ni moja ya ustaarabu wao kati ya hayo makabila mawili au?
 
kwenye ukoo wa Nyerere Jembe ni VICENT KIBOKO NYERERE, hawa wengine wasanii tu

Wewe huo ni unafiki,unamwita jembe kwakuwa yupo CDM, hata milliya utamwita jembe kwa kuhamia CDM
Hebu tuache fikra mgando

Kwakuwa nduguzako hawapo CDM je nao utawaitaji?
 
mako-omba-kura.jpg

Mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (kulia) akimwinamia Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli wakati akimwomba ampigie kura iliaweze kuchukuwa nafasi hiyo kwa wagombea kutoka Tanzania Bara, Bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

vingine sio kuvijadil kihvo huo ni utan baina yao .nyie mmepelekea kuweka mawazo tofauti na utani wao
 
Back
Top Bottom