Makongoro Nyerere aapa kuwaning'iniza mafisadi CCM

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Makongoro Nyerere aapa kuwaning'iniza mafisadi CCM
Send to a friend
Monday, 05 September 2011 20:41


makongoro%20nyerere1.jpg
Makongoro Nyerere

Christopher Maregesi, Bunda
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere ametangaza kusudio la kuwasilisha hoja binafsi katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho(Nec), kuhoji sababu za watuhumiwa wa ufisadi kushindwa kujiuzulu hadi sasa huku akimtaka Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kuachana na watuhumiwa hao.

Msimamo huo wa Makongoro ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere unakuja kipindi ambacho kikao cha Nec ya CCM kinatarajiwa kufanyika mwezi huu baada ya kile cha Kamati Kuu (CC) kilichoketi Mjini Dodoma mwezi uliopita kutoa muda zaidi kwa watuhumiwa hao kujipima hadi mkutano huo wa Nec.

Akifungua mkutano maalumu wa Nec ya CCM wilayani Bunda, Makongoro alisema kilichopo sasa ni kama mchezo wa kuigiza ambao hauingii akilini, hivyo akasema ni vyema akawasilisha hoja kwenye kikao hicho kuhoji uhalali wa watuhumiwa hao kuendelea kubaki na nyadhifa zao ndani ya chama.

Uamuzi wa kuwataka watuhumiwa hao kujivua gamba uliamuliwa na Nec iliyoketi mjini Dodoma Aprili, ambako pia CC iliyokuwapo ilijiuzulu na kuundwa upya huku Sekretarieti iliyokuwa chini ya Katibu Mkuu, Yusuph Makamba ikivunjwa na kuundwa upya kama mwanzo wa kujenga mwelekeo mpya wa chama.

Tangu wakati huo, mpango wa kujivua gamba umekuwa ukipigwa danadana kwani awali, ilielezwa kwamba watuhumiwa walipewa siku 90 baada ya kutakiwa kupima tuhuma dhidi yao lakini baadaye CCM ikakanusha na hadi sasa wengi wao wanaendelea na nyadhifa zao.

Makongoro akizungumzia zaidi danadana hizo, alisema huenda kinachowatia kiburi kugoma kung'oka kwenye nyadhifa zao ni uhusiano wa karibu walionayo na Rais Kikwete.

Alimtaka Kikwete kuachana nao na kusimamia kikamilifu uamuzi uliofikiwa na CC ili kukijengea heshima chama hicho.
Alisema kutowajibika kwa wanachama hao kunakitia doa chama hicho mbele ya jamii ambayo imekuwa ikikiamini kutokana na historia yake ya uadilifu.

“Nasema mbele yenu; sifurahishwi na watuhumiwa hao kuendelea kubakia ndani ya chama. Nitawasilisha hoja mbele ya kikao cha halmashauri kuu kuhoji kwa nini bado wamo huku wakikichafua chama?”

Makongoro ambaye aliwataja watuhumiwa hao kwa majina, alisema kuendelea kuwamo ndani ya chama hicho kunakifanya kikose mvuto na mashiko kwa jamii.

Katika kikao cha Nec Aprili, mwaka huu Makongoro alikuwa mwiba kwa watuhumiwa hao huku akihoji mantiki ya mwenyekiti wake kuwanadi majukwaani wakati wa kampeni za urais wa mwaka jana.

Makongoro ambaye aliwasilisha hoja kwa aina yake akitumia neno 'site' kuwakilisha vijiwe vya wanachama, alisema mwenyekiti alivyowanadi watuhumiwa hao katika uchaguzi wa mwaka jana: “site walihoji sasa ndiyo nini?”

Mpango wa kujivua gamba ulitangazwa na Rais Kikwete wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM mjini Dodoma, akisema lengo ni kukihuisha chama na kukirejesha katika misingi yake ya TANU na CCM ya mwaka 1977.

 
Tusibiri lakini nijuavyo mimi M/kiti wao na EL hawakukutana barabarani na watavushana hadi uchaguzi wa 2015
 
hivi huyu braza tangu alipohama arusha alishaacha kupiga kile kitu??
 
makongoro mwenyewe ni GAMBA ajivue kwanza yeye,hakuna aliye msafi ndani ya ccm,ukiwa rafiki na mwizi hata wewe utakua mwizi.
 
Uzuri wa huyu jamaa ni kwamba haogopi mtu.Sina wasi wasi naye kwani najua atafanya kweli kama alivyoahidi na hawawezi kumziba mdomo.
 
LOL Alikuwa wapi wakati wa Utawala wa Rais Mwinyi? Na wakati huo alikuwa NCCR Mageuzi hakuwaona hao Mafisadi?

Haya kama kweli ameamua kuanza basi aende pake Ikulu akamuulize Rizwani ni nani haswa anaiyeitaka UDA?
 
Makongoro amekosea strategy ya kuwatahadhalisha mafisadi nia yake ya kuwalipua hivyo lazima watamshuhulikia; alitakiwa akae kimya mpaka kwemye kikao ndio awalipue kama alivyomlipua mkweree kwenye Nec iliyopita, hata hivyo mimi huyu jamaa namuaminia atawafanyizia hawa mapacha kwani ni jasiri na hamuogopi mkweree.
 
hahaha watu wengi bana,eti anatafuta mshiko na kashaishiwa subiri tu maana kila kitu kinafanyika na kinakuwa recorded kwa wananchi,atasema ukweli wake na wananchi watasikia na pole pole ndio mwendo ikifika hapo 2015 hayo yote yataonekana......
 
makongoro mwenyewe ni GAMBA ajivue kwanza yeye,hakuna aliye msafi ndani ya ccm,ukiwa rafiki na mwizi hata wewe utakua mwizi.

Kweli ndugu yangu,

Sina hakika kama anajua analoliongea...Na kama kweli analijua basi angetambua kuwa hakuna anayepaswa kubaki ndani ya CCM labda wakawachukue wale wazee wanaovaa kandambili za mwaka 1955 (enzi za TANU) ili waje wakachukue chama chao.

Hawa watu wanatakiwa kujua kuwa CCM haipo tena...ilishakufa siku nyingi tu...Labda wamesahau kubadili login name na avatar!!
 
Christopher Maregesi, Bunda

Makongoro ambaye aliwataja watuhumiwa hao kwa majina, alisema

Nani?

Magazeti yetu jamani ni magumashi kupita maelezo. Kama Makongoro mwenyewe amewataja kwa majina, Nape ameshawataja kwa majina, mwandishi anaogopa nini kutaja ambacho source ya habari, Makongoro, tayari ameshawarahisishia?
 
"Kwa upande wake, Nyerere alisema akifanikiwa katika kinyang’anyiro hicho, ataanza kushughulika na kukiimarisha chama ili kiweze kurudi katika misingi yake"

SWALI:

Makongoro anataka kugombea uraisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi?

Nauliza hivyo kwakuwa toka awali ajenda yake kubwa ni kuleta nidhamu ndani ya chama na kukirudisha kwa wananchi. Sijawahi kumsikia akisema atafanya nini kwa watanzania akiwa Rais, ila namsikia na kumkariri atafanya nini akiwa mwenyekiti wa chama.

Tatizo la watanzania sio chama, ni mmonyoko wa maadili, rushwa, ufisadi, uwajibikaji, na uwazi ndani ya serikali. Mengine ni huduma mbovu za kijamii (elimu, afya, maji, n.k). Sasa ajaribu kujikita kuelezea atashughulikia vipi matatizo kama hayo yanayowakabili watanzania.

NB: Ikumbukwe kuwa sio lazima Rais anayetokana na CCM awe mwenyekiti pia wa CCM, ni utamaduni tu uliojengeka ndani ya Chama.

CC: Zakumi
 
Tunachohitaji ni uzalendo kulinda mali na wananchi kujisikia ni wazawa. Sio lugha za malimao zenye dalili ya kutenga mtu.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom