Makongoro Mahanga: Rais kavunja katiba kuteua wabunge wa kiume 6, inataka wawe wanawake angalau 5

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Akiandika katika ukurasa wake wa Facebook, Makongoro Mahanga amedai kwamba Rais Magufuli kavunja kifungu cha 66(e) cha katiba kwa kuteua wabunge wa kiume sita.

Mbunge huyo na waziri wa zamani amesema katiba ililenga zaidi kuwasaidia wanawake na si wanaume na anasema katiba imevunjwa.

N.B: Kuna ukweli, ukipitia katiba kifungu cha 66(e) kinataka wabunge wa kuteuliwa wawe sawa,wanawake watano,na wanaume watano.Mahanga anasema tayari wanaume wamefika sita,hivyo katiba imevunjwa.

Tunatokaje hapa? Rais anaweza kumpiga chini mbunge mmoja wa kiume?sheria inaruhusu rais kumuondoa? Je mbunge akijiuzuru ili kuondoa kadhia hii,itakuwa na maana gani? Google katiba ukiangalie kifungu hicho,halafu hesabu wabunge waliokwisha teuliwa na jinsia zao.

Wabunge wa kiume walioteliwa na Rais:
  1. Abdallah Posi
  2. Abdallah Bulembo
  3. Palamagamba Kabudi
  4. Philip Mpango
  5. Augustine Mahiga
  6. Makame Mbarawa
*Nikikosea katika hayo majina nikosoe.

ANGALIZO: Nataraji miongozo ya spika itaibuliwa kabla ya hawa wabunge kuapishwa ili bunge lijue. Je "litabariki" yaliyofanyika?
=====

Tazama mjadala huu ulivyosomwa ktk kipindi cha Jamii Leo

=====

Anaandika Dk. Makongoro Milton Mahanga..

MTIHANI MKUBWA WA KIKATIBA KWA SPIKA NDUGAI MWEZI HUU

Nimefuatilia majadiliano mazito kwenye mitandao ya kijamii, hasa FB, JF na WhatsApp kuhusu andiko langu la jana kwenye ukurasa wangu wa FB kuhusu Rais kutoshauriwa vizuri na hivyo kuvunja Katiba Ibara ya 66 (1) (e) kwa kuteua wabunge wanaume zaidi ya inavyoruhusiwa na Katiba.

Mpaka sasa Rais ameteua wabunge wanaume sita na wanawake wawili. Hata hivyo ambao wamekwishaapishwa ni wabunge wanaume wanne na wanawake wawili. Wabunge wawili wanaume walioteuliwa hivi majuzi hawajaapishwa na Spika wa Bunge. Uapishaji wa wateule hao wawili unatarajiwa kufanywa na Spika tarehe 31 mwezi huu.

Kwa hiyo tarehe 31 Januari 2017, Spika ana mtihani mkubwa wa ama naye kushiriki kuvunja Katiba (ambayo na yeye aliapa kutoivunja) ama kukataa kushiriki kuvunja Katiba kwa kuwaapisha wanaume wawili zaidi kuwa wabunge walioteuliwa na Rais kwa mujibu wa wa Ibara ya 66 (1)(e) ya Katiba ya JMT.

Mtu mwingine anayetakiwa kushiriki au kutoshiriki tena kwenye uvunjaji huu wa Katiba ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anategemewa asirudie kosa la uvunjifu wa Katiba kwa kushindwa kutoa ushauri wa kisheria na kikatiba . Kama alishindwa kumshauri Rais asiteue wanaume kwa idadi inayovunja Katiba, basi angalau aingilie kati sasa na kushauri kwamba Prof. Palamagamba Kabudi na Alhaji Abdallah Bulembo (wote marafiki zangu), mmoja asiapishwe kama mbunge ili idadi ya wabunge wanaume wateule wa Rais isizidi watano kinyume na Katiba.

Rais bado anaweza kushauriwa kwamba kabla ya tarehe ya Spika kuwaapisha wateule hao wawili Bungeni, Rais atengue uteuzi wa mmoja wao na amteue kwenye nafasi nyingine yoyote (ziko nyingi - ubalozi, ukuu wa mkoa n.k.). Ili Spika amwapishe mmoja tu kuwa mbunge, na baada ya hapo Rais akumbushwe kwamba nafasi tatu zinazobaki (kama atafikisha idadi ya wateule 10) zote aje kuteua wanawake. Hapo suala hili litakuwa limesawazishwa vizuri kikatiba.

Lakini nitamshangaa sana Spika Ndugai kama tarehe 31 Januari 2017 atakubali kushiriki kuvunja Katiba Ibara ya 66 (1) (e) kwa kuwaapisha wanaume wawili kuwa wabunge walioteuliwa na Rais na hivyo idadi ya wanaume wateule kufikia 6.

Kwanza ni kinyume cha Katiba, lakini pia Mhe. Spika Job Ndugai anakumbuka sana mwaka 2005 mimi na yeye tukiwa wabunge wa kawaida (back benchers) tena tukikaa majirani kwenye Ukumbi wa Msekwa, tulivyojadili sana Kifungu hicho cha Katiba na kuirekebisha kuwapa wanawake nafasi tano, wakati Bunge tunafanya marekebisho ya mwisho ya Katiba. Naamini Spika Ndugai hajasahau mjadala ule na maafikiano tuliyoyafikia na kuwapa akina mama nafasi zisizopungua 5 kwenye kipengele hicho.

Kwa kukumbusha tu, Katiba kwa Kiswahili imeandikwa kama ifuatavyo kuhusu kipengele hicho:... " 66 (1)(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za Ibara ya 67 (1) na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa wanawake;"...

Na Katiba kwa Kiingereza ikisema... "66 (1)(e)..Not more than ten members appointed by the President from amongst persons with qualifications specified under paragraphs (a) and (c) of subarticle (1) of Article 67 and, at least five members amongst them shall be women;"...

Kwa wale waliojadili hoja yangu ya jana kwa woga, unafiki, kisiasa, chuki binafsi, kutofahamu au kwa kujitoa tu ufahamu, wajue kwamba maneno "wasiopungua", "at least" na "shall" kwenye Ibara hiyo yanamlazimisha Rais kuteua wanawake 5 au zaidi.

Kazi kwako rafiki yangu Mhe. Job Ndugai, Spika wa Bunge la JMT. Fanya hima kukaa na Mwanasheria wako wa Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwanasheria wa Rais kurekebisha suala hili la kikatiba kabla ya kuwaapisha wanaume wawili tarehe 31 Januari 2017 kuwa wabunge walioteuliwa na Rais.... Kila la heri.


Na Dr. Milton Makongoro Mahanga.
 
Masaju atatusaidia hapa
Mkuu, muhimu ni kupata idadi kamili na majina ya wabunge wateule wa rais ili tujue kama rais ana mshauri wa kisheria au hana!

66(e) not more than ten members appointed by the President from
amongst persons with qualifications specified under paragraphs (a)
and (c) of subarticle (1) of Article 67 and, at least five members
amongst them
shall be women;

 
Mkuu, muhimu ni kupata idadi kamili na majina ya wabunge wateule wa rais ili tujue kama rais ana mshauri wa kisheria au hana!

66(e) not more than ten members appointed by the President from
amongst persons with qualifications specified under paragraphs (a)
and (c) of subarticle (1) of Article 67 and, at least five members
amongst them shall be women;
Cheki hapo juu
 
Hivi huyu mahanga bado yupo chadema?alinishangaza eti anahama ccm kisa hakuwa i kuchapandishwa cheo na JK kutoka unaibu waziri kuwa waziri kamili kama wenzie..hayuko sawa upstairs!BTW kwenye hili wataalamu wa katiba watusaidie.
Yule ni mwananchi mwanasiasa anaangalia Maslahi yake havunji katiba yetu. Ila hoja hapo ni rais kuvunja katiba
 
Back
Top Bottom