Makongoro Mahanga naye kasema haya , wewe umeyasikia ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makongoro Mahanga naye kasema haya , wewe umeyasikia ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Oct 22, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  SERIKALI imesema inachukua hatua mbalimbali za kukuza uwekezaji wa ndani kwa lengo la kuongeza nafasi za ajira kwa vijana.
  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Milton Mahanga aliyasema hayo Dar es Salaam alipofanya ziara katika Kampuni ya Dar es Salaam GlassWorks inayoshughulika na utengenezaji wa vioo.
  Dk. Mahanga alisema katika ukuzaji huo wa uwekezaji wa ndani, serikali imeanza kuchukua hatua za kuziunga mkono na kuzipa ushirikiano wa kila aina kampuni za ndani ili kuziwezesha kupata zabuni kubwa katika manunuzi ya serikali.
  Alisema ingawa kampuni nyingi za ndani zinatengeneza bidhaa zisizo na ubora mkubwa kama inavyopendekezwa na Shirika la Viwanga Tanzania (TBS) , serikali itaendelea kuzipa ushirikiano kampuni hizo ili ziweze kuzalisha bidhaa zitakazoweza kuleta ushindani katika soko la kimataifa.
  “Lengo letu ni kuona kuwa kampuni za ndani zinapiga hatua kubwa katika uzalishaji na uwekezaji hatua itakayosaidia kukuza soko la ajira kwa vijana wetu ambao wanahitimu katika vyuo vya elimu ya juu na vyuo vya kada ya kati,” alisema Dk. Mahanga.
  Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Shiraz Jessa alisema kampuni hiyo inayojishughulisha na utengenezaji wa vioo na aluminium imepata mafanikio makubwa katika kuboresha bidhaa inayozalisha na kuleta ushindani kwa soko la nje.
  “Changamoto kubwa tunazokabiliana ni kampuni na wakandarasi wa kigeni kutumia zaidi wahandisi na mafundi kutoka nje ya nchi badala ya kuwatumia wa ndani.Wakati Tanzania ina wataalamu wenye uwezo mkubwa hasa kutoka katika kampuni yetu lakini hawatumiki na hivyo
  kuwakosesha ajira na kazi za kutosha Watanzania.
  “Tunaomba Wizara ya Kazi na Ajira iweze kulinda soko la ajira la ndani kwa kuhamasisha matumizi ya wataalamu wa ndani na si wa nje kwa kuwabana makandarasi wa nje kutotumia wataalamu na wahandisi wa kigeni,” alisema Jessa.
  Miongoni mwa majengo ya kisasa yaliyojengwa kutokana na bidhaa za kampuni hiyo ni majengo makubwa ya PPF Tower, PPF House, TCCA, Tanesco, Twiga House, NSSF Mwanza, Airtel, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Barclays, Citbank, NBC, Exim, CRDB na Habib Benki.
   
Loading...