Makongoro Mahanga na Chuki binafsi dhidi ya gazeti la Mwananchi?

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Nilikuwa napitia maoni ya wasomaji wa gazeti la Mwananchi kwenye tovuti yao. Moja ya wachangiaji walikuwa Mh Makongoro Mahanga Mbunge wa Segerea. Nanukuu maoni yake hapa chini..

"Hongera sana mbunge mwenzangu Mnyika. Pia hongereni sana gazeti la Mwananchi kwa kutoa vizuri sana stori hii front page yote na kuipamba vizuri. Mngekuwa mnafanya hivi kwa stori zote za aina hii mngeonekana gazeti la maana sana. Hivi tarehe 3 Mei 2012, yale matokeo ya
Segerea mahakamani mliyatoa ukurasa gani? Wa 12? Je, angeshinda Mpendazoe siku ile Mahakamani mngetoa ukurasa gani? Bila shaka ingekuwa kama leo!"

Bila kuathiri haki ya Mheshimiwa Mahanga ya kutoa maoni yake je hakuna cha kujifunza hapa hasa tukizingatia kuwa Mwandishi wa Mwananchi alikuwa miongoni mwa mashahidi wa ndugu Fred Mpendazoe. Najaribu tu kudadisi kama ni kweli gazeti la Mwananchi lina chuki binafsi dhidi ya Mh Mbunge.
 
mwananchi wangeripoti issue ya makongoro kama ya mnyika ujue gazeti kwa cku ile lingekosa mvuto kwan thief is thief...
 
unajua biashara ya magazeti ni ngumu sana kwa sababu kinachouza gazeti ni kichwa cha habari!Inawezekana habari ya mhe. makongoro isiuze gazeti lkn ya mnyika ikauza sana!Nadhani ndicho kilichotokea!ila ni kwann,mimi cjui!Mh. Makongoro uwasamehe tu!
 
Nilikuwa napitia maoni ya wasomaji wa gazeti la Mwananchi kwenye tovuti yao. Moja ya wachangiaji walikuwa Mh Makongoro Mahanga Mbunge wa Segerea. Nanukuu maoni yake hapa chini..

"Hongera sana mbunge mwenzangu Mnyika. Pia hongereni sana gazeti la Mwananchi kwa kutoa vizuri sana stori hii front page yote na kuipamba vizuri. Mngekuwa mnafanya hivi kwa stori zote za aina hii mngeonekana gazeti la maana sana. Hivi tarehe 3 Mei 2012, yale matokeo ya
Segerea mahakamani mliyatoa ukurasa gani? Wa 12? Je, angeshinda Mpendazoe siku ile Mahakamani mngetoa ukurasa gani? Bila shaka ingekuwa kama leo!"

Bila kuathiri haki ya Mheshimiwa Mahanga ya kutoa maoni yake je hakuna cha kujifunza hapa hasa tukizingatia kuwa Mwandishi wa Mwananchi alikuwa miongoni mwa mashahidi wa ndugu Fred Mpendazoe. Najaribu tu kudadisi kama ni kweli gazeti la Mwananchi lina chuki binafsi dhidi ya Mh Mbunge.
Kwa yake mahanga, kama wangemuweka Mahanga ukurasa wa mbele kashinda unadhani nani angelinunua hili gazeti? Kwani mahanga hajijui alipendelewa?? Mwananchi hawawezi kujihusisha na kitu ambacho kitaharibu biashara yao.
 
Back
Top Bottom