Makongoro Mahanga, Kata ya Kimanga umeisusa?

jabali gumu

JF-Expert Member
Aug 18, 2013
229
45
Hapa Kimanga kuna kipande kidogo cha Barabara maarufu kituo cha Don hali ni mbaya mno. Barabara haipitiki Leo siku ya tatu madaladala yanaishia Don hayafiki kituoni kutokana na ubovu wa Barbara. Hivyo namuuliza Mbunge wetu, Makongoro umetususa? Maana hii kero ni ya muda mrefu.
 
Ni mateso makubwa kwa wana Tabata Kimanga, maana daladala zimemua kuishia kama kilometa moja kutoka kituo cha kimanga barabara ni mbovu na kituo cha magari ni tope tu hivo abiria inabidi kuuchapa mguu kufuata daladala japo magari mengine yanapita kwenye hiyo barabara, tunaomba mamlaka zinazohusika kuliangalia jambo hili kwa ukaribu maana watu wanateseka sana.
 
Wananchi wa Tabata Kimanga wanateseka Kwa kadhia hii Leo ni siku ya tatu Magari hayafiki kituoni sisi wananchi tulikwenda mpaka Kwa Mkurugenzi na barua ipo mezani Kwa Mkurugenzi yapata mwezi mmoja sasa lakini kimya.
 
Alishasemaga kuwa kimanga hamkipa kura hata moja na mnaonyesha chuki za wazi wazi juu yake sasa amesema mtakiona cha moto. Yeye yupo busy kuwagudumia wana segerea kule kwake pamoja na kukarabati ile barabara ya vingunguti. Mara baada ya kupata ubunge wake wa wizi wa kura alisema kata ya kimanga yeye sio mbunge wenu. Muda umefika sasa wa kuhakikisha Makongoro mahanga harudi tena bungeni kwani huyu kwetu ni mzigo.
 
Back
Top Bottom